Ukweli kuhusu tukio la tuhuma za rushwa monduli dhidi ya masyaga matiny | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu tukio la tuhuma za rushwa monduli dhidi ya masyaga matiny

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Juma Kilaza, Jun 17, 2012.

 1. J

  Juma Kilaza Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  <meta http-equiv="refresh" content="0;URL=launch?reason=no_js_enabled">

  Watanzania wenzangu,
  Nachukua nafasi hii, kwa masikitiko, kutoaTamko fupi kama kaka wa MASYAGA MATINYI - mdogo wangu anayenifuatia kwa baba namama yetu. Aidha, mimi pia ni mtumiaji wa jina la ubini la "MATINYI" na ndiyomaana baadhi yenu mlihisi kwamba ni mimi niliyekamatwa na TAKUKURU. MASYAGA anamwanasheria wake na itakapobidi atatoa Tamko la kisheria lakini ili kuondoaukungu nimeona ni heri nitoe UFAFANUZI wa tukio zima. Zaidi, ni uzalendo wanguna mapenzi yangu kwa haki, na wanaonifahamu wanalijua hili vema.

  Naomba nirudie: KESI NZIMA YA RUSHWA DHIDIYA MASYAGA NA WENZAKE NI UONGO. Huu si utetezi tu bali pia ni UKWELI wakilichotokea. Hakuna kuficha: TAKUKURU ina tatizo.

  Ipo sababu kwa nini imenichukua muda mrefukulisemea jambo hili. Natamka wazi kwamba nina uhakika na hiki nikisemacho;mwenye hadithi tofauti akawasaidie TAKUKURU mahakamani. Kwa kuzingatia kuwakesi haijaanza kusikilizwa, Tamko hili kamwe si kuingilia uhuru wa mahakama(contempt of court) bali ni kuingilia uovu &#8211; siyo utendaji - wa TAKUKURU.MASYAGA hakuizungumzia rushwa wala hongo; hakuiomba na wala hakuipokea.

  Kwa wanaofuatilia vizuri habari za Tanzania,MASYAGA ni mmoja wa waandishi wa habari mahiri nchini linapokuja suala lakutetea na kulinda maslahi ya taifa letu na anaijua vema sekta yetu yamaliasili. Sisemi hivi kwa kuwa ni mdogo wangu, bali kwa kuwa maandishi yakeyapo kama uthibitisho. Itakumbukwa kwamba wiki moja kabla ya tukio hili alitoahabari nyeti ambayo sitashangaa nikisikia baadaye kwamba ndiyo imemponza.

  MUHTASARI WA AWALI

  Alhamisi Juni 14, 2012, mtandao wa JamiiForum na televisheni ya TBC walisambaza habari duniani na nchini kuhusu tukiola kukamatwa kwa waliowaitwa waandishi wa habari watatu akiwemo MASYAGAMATINYI, Mhariri wa gazeti la Rai. TBC1 walimkariri kamanda wa TAKUKURU wa mkoawa Arusha akidai kwamba akina MASYAGA walimwomba rushwa mtumishi wa Tanescohuko Monduli ya sh. milioni 1.8 na kisha kupokea sh. 200,000 kamakianzio. TBC1 waliinukuu TAKUKURU wakidai eti waandishi hawa walikuwa wakimbanaMtanesko huyo kwa tuhuma kwamba hana sifa za kushika nafasi aliyonayo.

  Ijumaa MASYAGA na wenzake walifikishwamahakamani mjini Arusha na kusomewa mashitaka ya kuomba rushwa ya sh.milioni 1.5 na siyo sh. milioni 1.8 tena na eti walizipokea sh. 200,000.TAKUKURU haikueleza kwa nini kiwango kimebadilika.

  Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ambayo nakalayake ninayo kibindoni, mtuhumiwa wa pili amebambikiziwa kosa la pili lakumchukulia MASYAGA huo mzigo wa rushwa. Watuhumiwa wote watatu, wengine wakiwani MWITA CHOMETE na BORA BIDIGA, wamepata dhamana na kesi yao itatajwa tenaJuni 29, 2012. Tunaishukuru mahakama ya Arusha na mwendesha mashitaka waserikali kwa kuiheshimu haki.

  KILICHOTOKEA

  1...Mtanesko ANDREA MEZAanalalamikiwa na jamii kujihusisha na ufisadi wa magogo ya miti ya stimu nandiyo tatizo lililowapeleka akina MASYAGA kwake pamoja suala la sifa zakezilizompa nafasi ya msimamizi wa mafundi wa TANESCO Monduli.

  2...Mtuhumiwa wa tatu, BORA, simwandishi bali ndiye aliyemwambia MASYAGA kwamba kuna tatizo Tanesco Monduli.Hata kama MASYAGA angetaka hongo, ni wazi kwamba asingeweza kuomba na kupokeambele ya mtu aliyemstua kuhusu suala hili la mistimu. Hii ni common sensetu.

  3...Tatizo lilianzia kwenyekitimutimu cha Mtanesko ANDREA na watu walioko Arusha ambao walikuwa wakimpigiasimu kumtisha kuhusu mambo yake ya mistimu. Hatimaye aliwatumia sh. 400,000zinazodaiwa kuwa ni za TAKUKURU kwa M-PESA na wakazipokea na kukubaliana kujakubeba zingine Alhamisi asubuhi. Wakati akina MASYAGA wanakwenda ofisini kwakeAlhamisi asubuhi, ANDREA kwa ujuha wake, alifikiri ni watu wale wa Arusha,hivyo, akawaambia TAKUKURU mchezo umekamilika na wenyewe wakarundikana TanescoMonduli kwa ushari bila kujua wanafanya nini.
  Kiongozi wa kundi lao alitokaArusha kuja kufanya operesheni ya kikomandoo.

  4...Kwa staili za ushushushu wasinema za James Bond, TAKUKURU walimpa ANDREA kirekodia sauti na kishawakajificha mahali kininja. Ili kuimarisha ushahidi wakamwambia ANDREAamweke Mtanesko mwingine ofisini mwake. Akina MASYAGA walipofika wakaanzamahojiano na ANDREA huku yule kijana (shahidi) akasisitiza kwamba wamalizemambo kishikaji (lengo likiwa kuwadakisha akina MASYAGA hongo na kupata rekodiya sauti). MASYAGA akasema HAPANA. Kisheria, kumchomokea mtu afanyeuhalifu kama walivyofanya Matakukuru hawa ni uhalifu.

  5...ANDREA na huyu kijana wakewakatoka kuzungumza faragha. Waliporejea yule kijana akamwekea sh. 200,000CHOMETE mfukoni na yeye bila kuchelewa akazitupa nje ya dirisha. Matakukuruzaidi ya sita wakaingia na kutoa kipigo kikali kwa CHOMETE pamoja na matusiyasiyoandikika hapa. Walimpa kipigo kitakatifu na ameishia kutibiwakwa PF3. Hawakujali kwamba wangeweza kuua. Ni matumaini yetu kwamba ataponavema. Kisheria, kumpiga mtuhumiwa ili umshikishe hongo mkononi ni uhalifu.

  6...Matakukuru wakaenda kwenyegari la akina MASYAGA kupekua kinguvu (bila kibali) ili kupata zile laki nne zaM-PESA. Hawakupata kitu. Wakawapeleka Arusha huku wakiamini kuwa MASYAGAameshapokea laki nne. Kwa akili nyepesi tu hili lilishakuwa suala la mistakenidentity lakini Matakukuru wakachagua kuendelea kuwa brutal,unprofessional, unethical, n.k.

  7... Baada tu ya tukio, kamandawao mkubwa akawaita TBC1 na papo hapo habari zikafika Jamii Forumkimazingaombwe na usiku saa 2:00 ikawa ndiyo habari ya kwanza. Hii ni kinyumecha maadili ya kazi za vyombo kama TAKUKURU, Polisi, Uhamiaji, n.k. Ni uhuni. Huwezikutangaza kitu unachokichunguza na tena ambacho kimeshatoa dalili kwamba kinawalakini. Ndiyo maana TBC hawakuelezwa kuhusu zile lakini nne. Kulikuwa naharaka gani wakati "watuhumiwa wao" walishapatikana? Kwa nini waiite TBC1 pekee&#8211; televisheni mbovu ya taifa letu?

  8...Katika hali ya ajabu, TBC1wameishikilia habari hii kuliko wanavyofanya kwenye habari zingine na kuzuamaswali kwamba nini hasa lengo lao. TBC1 walilala na kuamka nayo kwa kadriwalivyomudu. Aidha, Jamii Forum - wao ni nani katika mfumo wa utoaji habari zaTAKUKURU?

  9...TAKUKURU walipofika Arushawakaisikiliza ile rekodi. Haikuwa na sentensi wala robo ya neno la MASYAGAkuomba rushwa. Kwenye statement wakakwepa kukitaja kile kirekodia sautilakini MASYAGA akasema hawezi kusaini mpaka waandike ukweli. Kimsingi alikuwatayari apigwe hadi kufa lakini siyo kusaini uongo. Alitumia ushujaa kuilindahaki yake. Mahojiano yaliisha saa tano usiku na watuhumiwa wakawekwa rumandekusubiri majaliwa ya siku ya pili. Kwa kuheshimu ukweli wa tukio, ni hakika hiiilikuwa unlawful confinement. Huwezi kuwaweka watu ndani baada yakuwasukumia kosa la uongo, tena kwa kipigo, mateso na matusi. Hiyo ndiyoTAKUKURU yetu.

  10...Ijumaa asubuhi TAKUKURUwakawapeleka mahakamani na suala la sh. laki nne wakaliacha. Kwa nini? Aidha,zile sh. milioni 1.8 zikabadilishwa na kuwa sh. milioni 1.5 kwenye hati yamashitaka. Kwa nini? Hata hivyo, gazeti la MAJIRA limechagua kuandika sh.milioni 5; hili ni tatizo jingine kabisa. Si vyombo vingi vya habarivilivyoishadidia habari hii zaidi ya TBC1 kwenye siku ile ya kwanza kutokana naumakini wa wahariri wake.

  11...Kule Jamii Forum kunawahusika wengi walionunua kesi hii huku wakiwa hawajui chochote cha ndani.Upumbavu wetu wa siku zote Watanzania. Jamii Forum walijifanya kwamba hawaijuiTAKUKURU na vioja vyake. Mtanzania mwingine aliyeko Japan naye aliamuakusambaza habari hizi kwa nguvu zake zote kila sehemu aliyoweza; yuko Japanlakini ana kiherehere cha mambo ya Monduli.

  12...Bado kuna maswali kuhusianana kiu hii ya usambazaji na utangazaji huu wa habari hizi kwa nguvu zote iwapoina uhusiano na binadamu walioandikwa na MASYAGA hivi karibuni. Kama tujuavyo,mbuga zetu ni shamba la bibi lakini ni upumbavu kuamua kwamba Watanzaniawote tukae kimya. TAKUKURU walikuwa na shida gani ya kuwasukumia raia wemamambo haya, tena kwa kipigo, uongo, utesaji, utangazaji wa kihuni, n.k.? Kunasiri gani?

  HITIMISHO

  Hizo laki nne ziko wapi? Kwa ninihazizungumziwi tena? TAKUKURU waeleze tangu lini wakawa na haki ya kumshikishamtu pesa kwa kipigo. Matakukuru wakitoe kirekodia sauti walichompa Mtanesko waona kamwe wasiseme eti hakuweza kurekodi vema.

  TAKUKURU waoneshe jinsi MASYAGA alivyopokealaki nne huko M-PESA kwani aliwapa simu zake kwa hiyo wasilikwepe hili na ndlojambo walilolidai baada ya kumkamata. TAKUKURU waeleze ni kivipi MASYAGAangeomba rushwa mbele ya mtu aliyekuwa anamlalamikia Mtanesko huyu.

  TAKUKURUwaeleze mikono ya MASYAGA ilikuwa wapi mpaka ikabidi apokelewe hongo na CHOMETEwakati wote walikuwa hapo hapo?

  TAKUKURU waeleze kwa nini walianza na madaiya sh. milioni 1.8 na kesho yake wakapunguza hadi sh. milioni 1.5?

  TAKUKURU watudokezee tujue uhusiano wao na mwandishi wa TBC1 na mhariri wa TBC1 kwambahata habari ikiwa na mashaka bado itarushwa tu mfululizo kwa siku kibao - wana ubiagani kwenye hili tu?

  TAKUKURU waeleze kwamba wana maslahi gani ya kumlinda mtu anayelalamikiwa na wananchi kwamba anafanya uhalifu?
  Mpenda haki yeyote aelewe kinachoendelea namzushi yeyote aseme lake lakini MAHAKAMA itamaliza mchezo wote.
  Asalam Aleikum!
  MOBHARE MATINYI, Washington DC, Juni 17, 2012.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu ungefanya editing kidogo ili tuweze kuisoma vizuri!
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kuna mtu alishapost hii kitambo soma post za wenzio b4 hujapost
   
 4. g

  gati Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utajuaje kama ana hasira?!, maelezo yake yanazidi kunifumbua macjo kuwa Matinyi aliomba rushwa. Nadhani PCCB walifanya kazi yao vyema.
   
Loading...