Ukweli kuhusu "The Amytville Horrors"

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Umewahi kutazama filamu za "The Amytville Horrors" zipo nyingi, ya mwisho iliachiwa mwaka 2017. Filamu hizo ni zinatokana na stori ya ukweli sema zingine zimeongezewa chumvi ili kuleta ladha kwa watazamaji lakini ya mwaka 1979 ndio inaakisi vyema uhalisia.

Twende sasa; Mwaka 1974, Ronald "Butch" Defeo Jr katika makazi yao huko Amytville aliwaua watu sita kutoka familia yake mwenyewe.

Katika maelezo yake anasema kwamba katika nyumba yao hiyo alikuwa akisikia sauti za familia yake kichwani zikimwambia awaue na yeye akafanya hivyo ukweli.

Mwaka mmoja baadae baada ya tukio hilo familia nyingine ya bwana Lutz ilihamia katika nyumba hiyo lakini ndani ya siku 28 waliikimbia wakidai kuona mauza uza ya ajabu kwenye nyumba hiyo.

Kufuatia hali hiyo Polisi waliamua kuchunguza, walichofanya ni kutegesha Camera umbali kidogo na nyumba hiyo. Camera hizo ni zile zenye uwezo wa kupiga picha ambazo kwa macho ya kawaida huwezi kuona, Ina uwezo wa kupenya hata katika vitu visivyo onekana kirahisi.

Baada ya kuchukua picha nyingi, Mojawapo ya picha waliyoipata ndio hiyo hapo kama unavyoona. Inaaminika kuwa huyo ni John Matthew, Alikuwa ni mtoto mdogo bado wakati anauawa mwaka 74 na kaka yao ambae ni Ronald.

FAHAMUZAIDI
118623601_4313611322014097_145797646652577003_o.jpg
 
Mkuu hii story yako ina ukweli mwingi na chumvi pia. Jamaa alifungwa kwa madai kwamba ana tatizo la akili lakini huenda ni kweli kuna nguvu ilimwingia na kutekeleza mauaji hayo.
 
Mkuu hii story yako ina ukweli mwingi na chumvi pia. Jamaa alifungwa kwa madai kwamba ana tatizo la akili lakini huenda ni kweli kuna nguvu ilimwingia na kutekeleza mauaji hayo.
Nasikia jamaa nadunda mtaani now.
 
Kudadeki watu walivyo wehu wanakubali kulipia.
Si unajua watu wengine hawaamini mpaka waone wenyewe. Unafahamu the mystery murder of room 1046? Mauaji haya natamani kama yangepatiwa ufumbuzi na nani aliyatekeleza. Na kifo cha Elisa Lam, jao polisi walidai ilikuwa accidental death ila kila mtu anaona ni wazi yule dada aliuawa maana physical evidences zote ziko wazi nahisi polisi walikosa explanation.
 
Nilisoma kitabu cha Amtyville Horror miaka ya themanini. Nilipata mshawasha wa kununua video yake na kweli ilikuwa inatisha. Father Mancuso alijitahidi sana katika kuisaidia hiyo familia Ila kushindana na pepo yataka ujasiri.
 
Si unajua watu wengine hawaamini mpaka waone wenyewe. Unafahamu the mystery murder of room 1046? Mauaji haya natamani kama yangepatiwa ufumbuzi na nani aliyatekeleza. Na kifo cha Elisa Lam, jao polisi walidai ilikuwa accidental death ila kila mtu anaona ni wazi yule dada aliuawa maana physical evidences zote ziko wazi nahisi polisi walikosa explanation.
Aisee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom