Ukweli kuhusu teknolojia ya solar

AHAKU

Member
Jan 28, 2010
26
1
Ndugu zangu naomba walio na maarifa kuhusu teknolojia ya umeme wa jua wanipe elimu hivi yawezekana ukawa na umeme wa jua katika nyumba yako na ukatumia umeme kwa vyombo vyote ulivyo navyo kama tunavyofanya kwa umeme wa Tanesco na je gharama zake ni kama Sh ngapi za kibongo?
Nauliza hivi kwani kila siku nikisoma habari za umeme huu nakuta kazi yake ni kuwasha balbu, kuchaji simu na redio pekee.
Nimejenga kibanda changu mahala sasa umeme wa Tanesco nasikia watauleta baada ya miaka mitatu
asanteni. Nipeni desa wataalamu
 
Binafsi natumia solar power kwa miaka miwili sasa na tanesco hata sitaki kuwasikia hata kidogo na nimeshauri marafiki zangu nao wamefunga solar
Solar power inategemea na load utakayo funga
nakushauri ukisie mahitaji yako halafu upost na mie niakupa data zote na contacts numbers za wapi unawaza pata at whole sale prices
 
Ndugu Jubilant Nyumba yangu ina vyumba vitatu vya kulala, sitting na dining, jiko na small library. Sina mpango wa kutumia AC ila wearing ninayoifanya nataka iwe ile itakayoweza kuja kuhimili matumizi ya vitu kama friza kubwa, desktop comp, laptop, Tv tatu, pasi na jiko la umeme. Taa nataraji kuweka zile nyeupe wanaita energy server
Asante
 
Mimi naombeni data wapi nitapata mitambo ya 'wind energy' hapa kwangu kuna upepo mwingi tu 24x7!
 
kuna yule jamaa wa pale External Ubungo nasikia ni mjuzi wa aina hiyo ya umeme
 
Mimi naombeni data wapi nitapata mitambo ya 'wind energy' hapa kwangu kuna upepo mwingi tu 24x7!

NENDA UBUNGO PALE OPPOSITE NA EXTERNAL KATI YA LUCH TIME NA MAMA LAND, Jamaa ni mzuri kwa hayo mautaalamu
 
UDSM ingetakiwa iwe na kitengo kikubwa sana kuhusu solar energy,maana ndio huko tunapokwenda.Jua kali ,mvua azinyeshi kwa hiyo sisi tuna resources za kutosha.

Kutegemea umeme wa maji au generator ni old fashioned.Richmond ,IPTL etc ni ujinga wa hali ya juu.Wazungu wanafikiria Wind,solar power etc.
 
Ndugu zangu naomba walio na maarifa kuhusu teknolojia ya umeme wa jua wanipe elimu hivi yawezekana ukawa na umeme wa jua katika nyumba yako na ukatumia umeme kwa vyombo vyote ulivyo navyo kama tunavyofanya kwa umeme wa Tanesco na je gharama zake ni kama Sh ngapi za kibongo?
Nauliza hivi kwani kila siku nikisoma habari za umeme huu nakuta kazi yake ni kuwasha balbu, kuchaji simu na redio pekee.
Nimejenga kibanda changu mahala sasa umeme wa Tanesco nasikia watauleta baada ya miaka mitatu
asanteni. Nipeni desa wataalamu
Kuna watu wanajiita UMEME JUA wapo karibu na DHL ofisi pale oposity na quality plaza Nyerer road Dar ndiyo wataalamu wazuri wa mambo haya. sina contacts zao, lakini ukienda maeneo niliyoelekeza utawaona tu...... Vile vile wana vifaa vyote vinavyohusu silar systems na ukubwa mbalimbali kutegemeana na wewe utakuwa na vifaa vya uwezo gani kiumeme.
 
Ahaku mahitaji yako na yangu hayana tofauti na ukubwa wa nyumba yako ni sawa na wangu

Kwanza unachotakiwa kufanya kama hujafanya wiring hi kuhakikisha unatumia wire za 2.5mm kwa nyumba nzima hii itaondoa resistance wakati umeme wa dc unapita kwenye wire
pili wirering yako itenganishe kutokana na kila eneo la matumizi
nikimaanisha kutoka kwenye distribution box wire itakayopeleka umeme kwa taa za ndani ijitegemeee na taa za nje ijitegemee na sokets ijitegemee hii itarahisisha kumeneji umeme....

sasa nakujibu swali lako ulilo awali je unaweza kutumia solar kwenye zaidi ya taa na redio?
Ndio unaweza kutumia solar kwa kila kitu kinachotumia umeme

Ziada

solar energy ni mfumo wa kubalilisha neema ya jua aliyotupa Mwenyezi Mungu bure kuipeleka kuwa umeme
unaweza kutumie Solar enegy kwenye kitu chochote utakacho
Zingatio jinsi unakuwa na mahitaji mengi ndivyo solar plant yako itakuwa kubwa

kabla ya kufunga solar inabidi ufanye mahesabu ya total watts utazohitaji kwenye nyumba yako hio itakupatia jibu ni ukubwa gani wa solar unaohitaji..

je nitakuwa nimekusaidi swali lako au una sali la ziada??
asante
 
Ndugu zangu naomba walio na maarifa kuhusu teknolojia ya umeme wa jua wanipe elimu hivi yawezekana ukawa na umeme wa jua katika nyumba yako na ukatumia umeme kwa vyombo vyote ulivyo navyo kama tunavyofanya kwa umeme wa Tanesco na je gharama zake ni kama Sh ngapi za kibongo?
Nauliza hivi kwani kila siku nikisoma habari za umeme huu nakuta kazi yake ni kuwasha balbu, kuchaji simu na redio pekee.
Nimejenga kibanda changu mahala sasa umeme wa Tanesco nasikia watauleta baada ya miaka mitatu
asanteni. Nipeni desa wataalamu

Ni kweli kwanza inabidi ujue watts ngapi unahitaji. Rahisi kukadiria hizi kwa sababu vifaa vyote vya umeme huandikwa watts zake (au Amps na Volts - Ohm's law itakupatia Watts)

Nyumba ndogo inahitaji kama 3KWatt (nakisia hapa inategeme vifaa). Kwa kweli ni gharama kubwa kujitegemea kiumeme. Bila ya grid (Tanesco ) inabidi uwe na mchanganyiko wa solar, windmill na stand-by generator ili likikosekana jua au upepo utategemea generator.
Tatizo kubwa la umeme wa solar (au wind) ni jinsi ya kuuhifadhi umeme wakati unatengenezwa ili siku za mawingu au usiku uchote umeme kutoka kwenye hifadhi yako. Njia rahisi inayotumika kuhifadhi umeme ni kutumia deep-cycle batteries . Kawaida hizo huwa na uwezo wa 12V. Unatakiwa kutengeneza Battery Bank kwa kuzipangilia battery kama 4 mpaka 8 in parallel or series kutokana na mahitaji ya vifaa vyako.

Kwa ufupi vitu unavyohitaji:

1. Solar Panels (ziko aina nyingi hizi - Tahadhari na wabongo wasikuuzie vioo vya kichina)

2. Charge controller (kwa sababu ya kurekebisha umeme unaotoka kwenye panel usizidi na kuharibu battery)

3. Invertor - Kubadilisha umeme wa jua DC kwenda kwenye umeme wa nyumbani AC. Hizi ziko ambazo unaweka ukutani kwenye plug na ina-supply kwenye circuit yako ya nyumbani.

4. Deep cycle batteries ( hizi ziko kama battery za magari )

Ushauri wangu binafsi ni upate kama solar panels 3 au 4 za 250Watts/each na circuit yako iwe inakunywa umeme kwa matumizi ya taa, fans na vifaa vidogo vidogo. Achana na vifaa vikubwa kama vile Oven.

Kwa kweli ukishapata vifaa hivyo (ukimpta mdau akakutolea China bei poa) kufunga ni rahisi sana unahitaji elimu ya darasa la saba tu. Uchawi wa umeme wa jua ukishavifunga vifaa vyote basi unacheka tu kwasababu hamna bili tena na hivi
vitu hudumu kama miaka 30 hivi. Angalia mchoro hapo chini.

sysdiag_1_with12vbulb_400.jpg

¬K
 
Tatizo ningependa kujua hizo batteries ni kama za gari zina kaa mwaka mmoja na inabidi ubadili au inakuaje , je kama unatumai batteries 7 inamaana ubadilishe zote? thanx
 
Kwa kweli kwa Tanzania tuna jua la kutosha tu sioni kwa nini watu wengi hawatumii umeme huu ili kupunguza gharama kubwa za umeme na pia kuachana na umeme wa kubabatiza wa TANESCO, leo uko kesho hauko.
 
Tatizo ningependa kujua hizo batteries ni kama za gari zina kaa mwaka mmoja na inabidi ubadili au inakuaje , je kama unatumai batteries 7 inamaana ubadilishe zote? thanx

Hapana, hizi ni lead-acid batteries na zinadumu miaka mingi tu. Unatakiwa uzitunze kwa kujaza acid (electrolyte) kila baada ya muda kidogo.
Hizi zinaitwa deep-cycle batteries kidogo tofauti na battery za gari. Tofauti yake ni upana wa plates lakini zinatumia the same chemistry kufanya kazi.

¬K
 
Mimi naombeni data wapi nitapata mitambo ya 'wind energy' hapa kwangu kuna upepo mwingi tu 24x7!

Circuit setup ya solar na wind zipo sawa. Tofauti ni gharama na vipi umeme unazalishwa. Wind turbine inazalisha umeme kutoka kinetic energy ya mzunguko wa turbine. Kama unaishi sehemu yenye speed nzuri ya upepo wind turbine ni bora kuliko solar. Ni rahisi kutengeneza wind turbine kwa kutumia motor kutoka kenye broken treamill, pvc pipe na mbao. Unaweza kuagiza kutoka China pia. Sehemu utayosimamisha wind turbine inafaa isiwe na majumba marefu kwani kusimamisha hiyo turbine juu sana ni ghali mno.

¬K
 
Hapana, hizi ni lead-acid batteries na zinadumu miaka mingi tu. Unatakiwa uzitunze kwa kujaza acid (electrolyte) kila baada ya muda kidogo.
Hizi zinaitwa deep-cycle batteries kidogo tofauti na battery za gari. Tofauti yake ni upana wa plates lakini zinatumia the same chemistry kufanya kazi.

¬K
Asante kwa jibu zuri na dhani nitajiunga kutumia Solar
 
Ni kweli kwanza inabidi ujue watts ngapi unahitaji. Rahisi kukadiria hizi kwa sababu vifaa vyote vya umeme huandikwa watts zake (au Amps na Volts - Ohm's law itakupatia Watts)

Nyumba ndogo inahitaji kama 3KWatt (nakisia hapa inategeme vifaa). Kwa kweli ni gharama kubwa kujitegemea kiumeme. Bila ya grid (Tanesco ) inabidi uwe na mchanganyiko wa solar, windmill na stand-by generator ili likikosekana jua au upepo utategemea generator.
Tatizo kubwa la umeme wa solar (au wind) ni jinsi ya kuuhifadhi umeme wakati unatengenezwa ili siku za mawingu au usiku uchote umeme kutoka kwenye hifadhi yako. Njia rahisi inayotumika kuhifadhi umeme ni kutumia deep-cycle batteries . Kawaida hizo huwa na uwezo wa 12V. Unatakiwa kutengeneza Battery Bank kwa kuzipangilia battery kama 4 mpaka 8 in parallel or series kutokana na mahitaji ya vifaa vyako.

Kwa ufupi vitu unavyohitaji:

1. Solar Panels (ziko aina nyingi hizi - Tahadhari na wabongo wasikuuzie vioo vya kichina)

2. Charge controller (kwa sababu ya kurekebisha umeme unaotoka kwenye panel usizidi na kuharibu battery)

3. Invertor - Kubadilisha umeme wa jua DC kwenda kwenye umeme wa nyumbani AC. Hizi ziko ambazo unaweka ukutani kwenye plug na ina-supply kwenye circuit yako ya nyumbani.

4. Deep cycle batteries ( hizi ziko kama battery za magari )

Ushauri wangu binafsi ni upate kama solar panels 3 au 4 za 250Watts/each na circuit yako iwe inakunywa umeme kwa matumizi ya taa, fans na vifaa vidogo vidogo. Achana na vifaa vikubwa kama vile Oven.

Kwa kweli ukishapata vifaa hivyo (ukimpta mdau akakutolea China bei poa) kufunga ni rahisi sana unahitaji elimu ya darasa la saba tu. Uchawi wa umeme wa jua ukishavifunga vifaa vyote basi unacheka tu kwasababu hamna bili tena na hivi
vitu hudumu kama miaka 30 hivi. Angalia mchoro hapo chini.

sysdiag_1_with12vbulb_400.jpg

¬K
Kwa kuanzia gharama yake yote ya hivyo vikorombwezo hadi umeme jua utumike nyumbani unatakiwa uwe na Tsh ngapi kwa hapa bongo?
 
Kwa kuanzia gharama yake yote ya hivyo vikorombwezo hadi umeme jua utumike nyumbani unatakiwa uwe na Tsh ngapi kwa hapa bongo?

Kwa kweli sina uhakika gharama yote ni Tsh ngapi kwa vile sijawahi kununua hivi vifaa bongo na hivi sasa sipo hapo. Nategemea kuna watu humu wanaweza kukupatia Tsh ngapi.

Mimi nilimwekea mzee wangu mwaka jana lakini vitu vyote nilitoa Marekani ilinigharimu $1,100. Hii niliifanya grid-tied yaani itumie mchanganyiko wa grid(Tanesco) na solar. Mimi sijaweka battery hivyo hutumia solar na ukihitajika umeme wa ziada inavuta kutoka grid. Kwa kweli hii imepunguza sana gharama ya luku.
Kitu ghali katika hii project ni panels(vioo) lakini uzuri wake unaweza kuweka moja au mbili na baadae kuongeza kiurahisi bila kugusa sehemu nyengine (i.e. Solar array is scaleable). Nategemea kwenye miezi michache kumuongezea panels mbili na batteries hopefully in the near future nimuondoe kwenye grid.

¬K
 
Mheshimiwa naona umekata kiu ya wengi japo tulikuwa hatujauliza. Ninatumia solar pia kwa miaka miwili pia kwa taa, radio na tv. Mtaalamu aliniambia kuwa solar energy kwa sababu inaproduce current kidogo isingeweza kutumika kwa pasi au heater.
Je yawezekana habari hii kuwa kweli an fix? Nisaidie ili kama siyo nione uwezekano wa kuitumia kwa pasi pia.
 
Hata mimi pia ni mtumiaji wa umeme huu. Tatizo la umeme huu vifaa vyake ni ghari mno.
sysdiag_1_with12vbulb_400.jpg

Kwa mfano:
Wewe unahitaji kutumia pasi, pasi zilizo nyingi zina 1000Watts, labda unahitaji na jiko dogo la umeme lenye 1500Watts, Tv 100Watts, taa kadhaa zenye jumla ya 400Watts
, Kwa hapa jumla yake ni 3000Watts,

Kwa hiyo umeme wako wa Solar inatakiwa uwe na angalau zaidi ya 3000Watts.

Haya sasa tuje kwenye uwezo wa umeme wenyewe na gharama za vifaa,
Ili umeme huu ufanye kazi unahitaji vifaa vifuatavyo>

1. Inverter
2. Battery
3. Charger controller
4. Solar panel

Ukija upande wa bei. Inverter ya 500Watts inauzwa sh.105,000, ya 300Watts inauzwa sh.85,000. Ili vifaa vilivyotajwa hapo juu viweze kufanya kazi unahitaji inverter ya zaidi ya 3000Watts ambayo sijabahatika kuikuta madukani na sijui bei yake, labda wanaofahamu bei zake watuambie.

Ukija upande wa battery. Kutegemeana na inverter yako. Kwa mfano inverter za chini ya 500Watts unaweza kutumia battery ya N120 hata N150 na N100,
Je Inverter ya watts 3000 na zaidi utatumia battery ya N ngapi? kama siyo N800 au zaidi

Solar panel huwa inafanya kazi ya kuchaji battery, na yenyewe pia itategemeana na saizi ya battery. Kama battery ni kubwa na solar pannel itabidi iwe kubwa au ziongezeke idadi.
 
Back
Top Bottom