Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
- Asilimia kubwa ya watu wanaounda au kujiunga na vyama vya siasa Tanzania, hawafanyi hivyo kwa sababu ya itikadi, falsafa na sera bali ili kutafuta fursa, mengine ni yatokanayo.
- Wengi wanaoshabikia chama flani hawashabikii au kukiunga mkono chama husika kwa sababu wanaona chama hicho ni bora; bali kwa sababu kuna chama kingine/vingine wanavyodhani si bora.
- Wengi wa wanaohama kwenye vyama vya siasa si kwa sababu ya uzuri au ubaya wa vyama wanavyotoka au wanavyokwenda bali ni kwa sababu;-
- Fursa walizozifuata kwenye chama A, hawajazipata au kuna uwezekano wa fursa zaidi kwenye chama B,
- Wanakimbia watu/mtu flani kwenye chama wanachotoka, kwa bahati mbaya wanayemkimbia naye anaweza kuhamia wanakohamia na huko wakakutana tena.
- Wanafuata mtu, kwa bahati mbaya wanayemfuata anaweza kuwakimbia.kwa bahati mbaya pia anayefuatwa sio kwamba anawapenda au kuwathimini wanaomfuata bali anawalia ‘timing awatumie. Wafuataji wanakuwa hawana uelewa wa wanachokifanya.
- Ukiona mtu anapinga jambo ,bila kujali ni hoja gani anatoa; halipingi kwa kuwa ni baya bali kwa kuwa linahatarisha maslahi yake au kundi lake. Kwa mfano, ukiona mtu anapinga dhuluma, hapingi kwa kuwa anachukia dhuluma bali kwa kuwa yeye anadhulumiwa kwa wakati huo.
- Ukiona mtu anatetea jambo,bila kujali uzito wa hoja zake; hatetei jambo katika uzuri wake, bali kwa sababu jambo hilo linamnufaisha au kunufaisha kundi lake kwa wakati huo.
- Wengi hawako tayari kusema ukweli kwa sababu ni muhimu kusema ukweli, bali kwanza huangalia ukweli huo utamnufaisha nini? Kwa msingi huo, inakuwa ni vigumu kumuamini hata yule asemaye ukweli.
- Kila mtu anaamini chanzo cha hali tajwa hapo juu na matatizo mengine yote msingi wake ni wenzake, sio yeye wala yeye hana la kufanya na wakati huo huo anaaimini ipo siku hizo tabia hapo juu zitabadilika bila kutaka kufikiri kivipi.
Kwa hiyo suala ni kuuvunja huo mzunguko, hata hivyo kazi hiyo si rahisi na ndio maana hadi sasa si tu kwamba mzunguko huo upo bali unakuwa. Ijapokuwa hoja hii imekuwa na itaendelea kuwa ngumu kueleweka; huo unabakia kuwa ukweli ukiwa umeeleweka au bila kueleweka.
Tatizo kubwa linalotukabili watanzania haliko kwenye vitu vya nje bali kwenye vichwa vyetu wenyewe. Kila mtu ana ‘Fake’ huku akishangaa na kulaumu wenzake wanavyo ‘Fake’ huku kwa pamoja tukishangaa matokeo ya ‘Fake political life’ lakini pia tukiamini kuna siku ‘Fake political life’ itatupa ‘genuine results”