Ukweli kuhusu safari ya jaji mkuu washington DC, maafisa wake na Francis Nyalali

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Tumefanya uchunguzi hapa DSM na huko Washington DC kufuatilia hicho kinachoitwa semina ya majaji
iliyofanyika USA ambayo ilijaza na maafisa wakuu wa mahakama. uchunguzi wetu ulianzia ubalozi wa marekani
hapa dsm eneo la Drive inn kupata ukweli juu ya semina ya majaji hao lakini ktk kitengo chao cha habari kwa
Bw. MOORE akatuambia hakuna kitu kama hicho kuhusu mualiko wowote unaousiana na semina ya majaji au wanasheria uliopita ubalozi huo.

Tukatoka hapo tukawasiliana na ubalozi wa Tanzania uliopo washington DC kupata maelezo yeyote kuhusiana na semina yeyote ya majaji inayoendelea huko ofisa wa ubalozi alisita kwanza lakini baadaye walituambia kuwa hawawezi kushea information kama hizo na sisi kwahiyo tuwasiliane na wausika. Tukaenda kwenye website ya mahakama kuu ya marekani kuona kama kuna tangazo lolote kuhusu semina hakuna kitu kama hicho tumekuta matukio mengine lakini hakuna issue ya semina. Tumewasiliana na wahusika akiwemo jaji mmojawapo kwy ule msafara simu zao zinaita hazipokelewi.

Conclusion yetu

Kulingana na uchunguzi wetu tumeitimisha kuwa jaji mkuu pamoja na maofisa wa mahakama walikwenda Washington DC kwa ajili ya kitu kimoja tu nacho ni kujadili suala zima la issue ya acount ya Escrow na mpaka hivi sasa hakuna ushahidi wowote kuhusiana na uwepo wa semina unless watoe picha zinazoonesha semina hiyo ambayo wahusika walidai walikwenda kuhudhuria na siyo kuonana na JK.

Swali kubwa ambalo inabidi watanzania tujiulize hivi ni kweli mahakama zetu ni huru ?? kwa mujibu wa uchunguzi wetu ni kuna muingiliano wa hali ya juu kati ya mahakama na executive kwa maana ya ikulu. Tunajiuliza kama jaji
mkuu na maofisa wa ngazi ya juu wa mahakama wanaweza kufunga safari kwenda kuonana na Rais kwa ajili kujaribu kupotosha nchi na kulinda mafisadi. Je Rais anapokuwa nyumbani ni mara ngapi jaji mkuu na maofisa wake wanakwenda ikulu kujadili na mkuu wa nchi kuhusu mienendo ya kesi mbali mbali na maswala ya ushahidi??

Hii inatupelekea kuamini kabisa maneno aliyoongea aliyekuwa jaji mkuu wa Tanzania Francis Nyalali kuwa mahakama za Tanzania si huru na zitakuwa huru tu endapo ikulu itakapoacha kuitisha na kuyajadili mafaili ya watuhumiwa ikulu.

Kitendo cha ofisa wa ngazi ya juu wa ikulu Bw.Ombeni Sefue cha kutoa tamko la kutojadiliwa issue ya ESCROW bungeni na kujigeuza messenger wa mahakama na kulitishia bunge kuwa linaingilia amri ya mahakama ni kosa la wazi na linathibitisha jinsi ikulu inapoingilia wazi uhuru siyo wa bunge bali na mahakama zetu.
 
Wizi wa fedha za Escrow akaunti katika hali ya kawaida usingetokea ndani ya nchi yenye uongozi wenye maslahi mapana ya Taifa.Ni wazi kuwa wizi huo umetokea kwa kuwa tu kulikuwa na nia ovu toka Mamlaka kuu za nchi.Ni wakati muafaka kwa Watanzania kwa ujumla wetu kujitafakari na kuangalia kama kweli viongozi tunaowachagua kutuongoza na kusimamia raslimali za Nchi hii wanao uzalendo na dhamira thabiti ya kulinda Taifa hili kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.Inasikitisha,inauma,inaumiza na inakatisha tamaa kuona jambo kama hili lina dalili za wahusika kutoka ofisi kuu ya nchi.
 
Ilishasemwa tangu awali kwamba mtuhumiwa nambari moja wa sakata hili ni Rais Kikwete himself. Sasa zigo lote hilo lipo kichwani pake! ..
 
Ni wakati muuafka wananchi wakachukua hatua za kuadabisha ccm bila hivyo haya mambo yatakuwa yakitokea kila siku. Shime watanzania na tuanze na huu uchaguzi wa serekali za mitaa tuyatoe haya majitu yasiyo na uchungu na sisi.
 
Mkuu Politiki,Ikulu hawaingilii bali ni wahusika wakubwa wa Wizi huu na ingekuwa vinginevyo kusingekuwa na hizi blabla unazoziona.Mahakama zetu zina uhuru wa Kuhukumu wezi,wakuku,vitumbua,mayai,viazi vitamu mashambani,mihogo,machungwa na kadhalika.

Hazina uhuru wa kuhukumu watesaji, wa uwaji wa Albino,Mafisadi na wezi wa Mali za Uma na hatakutoa Maamuzi Magumu yenye kusimama upande wa Uma kuna utofauti Mkubwa sana katika ya Majaji wa sasa na wale wazamani Mfano.Lugakingira,Mwesiumo,Mwalusanya,Nyalali nk.Hawa wasasa wengi wamjisahau na kuacha kuwa Majjaji na kujigeuza kuwa Bajaji za watawala.

Hapa ndipo nchi ilipofika na wakulaumiwa siyo Viongozi bali wananchi ambao wengi wao wananunulika kwa bei ya chipsi mayai na kuuza kura zao.Yaani ni gharama kabisa na kubwa kununua Kuku wa Kienyezji kuliko kumnunua Mtanzania.Watu wazima wananunulika kwa sh 5000 kweli hapo kunanchi.Mtu anapewa zawadi za mamibilioni watu wanakenua kenua meno na kufukuzana na tumichango twa kulazimisha ujenzi wa maabara zisizokuwa na wataalamu
wala walimu.

Nchi nizaidi ya tunavyoijua ni Ujuha mwanzo mwisho wa-pu-mba-vu kuonekana wajanja na werevu na huku werevu wanapo jitahidi kuelimisha umwa wanrukiwa na kundi la wa-pu-mba-vu na kupigwa au kudhalilisha.Yote hii inatokana na aina ya Baba tuliyenaye.Tukisafisha Ikulu nchi itasafishika.
 
Ni aibu kubwa muhimili kama mahakama unajiingiza kwenye harakati za uongo kwa masilahi ya wachache. Nchi ikifikia mahali Mahakama inageuzwa kuwa danguro ujue mwisho wa utwala huo umefika ila unalazimishwa kuwepo
 
Ni wakati muuafka wananchi wakachukua hatua za kuadabisha ccm bila hivyo haya mambo yatakuwa yakitokea kila siku. Shime watanzania na tuanze na huu uchaguzi wa serekali za mitaa tuyatoe haya majitu yasiyo na uchungu na sisi.

Sasa ndugu yangu kama majaji wenyewe wanateuliwa huku bado anasoma what is tort unategemea nini hapo?utawala huu wa msafiri ni vituko kila siku
 
Mkuu politiki, japokuwa uzi wako unaweza kuwa 'unconfirmed' lakini umeandika kwa vielelezo ambapo hata sie wenye IQ chini ya 10 tunaweza kuelewa kwa ufasaha kabisa.
Kwa sehemu ulizofuatilia na majibu uliyopata vinayapa nguvu kubwa sana madai yako.
Nyongeza ni kuwa picha walizopiga na rais tumeziona, sasa nao kama wanapita huku basi watuwekee na hizo walizopiga kwenye tukio lililowapeleka tujiridhishe.
Ikidhihirika kuwa wamedanganya malengo ya safari basi ni ufisadi mwingine juu ya ufisadi maana hata hizo nauli na posho walizochukua zingeliongeza nguvu ya madawa pale hospitali ya taifa Muhimbili.
Watanzania hatuipendi nchi yetu, na tuanze sasa kwa kuwawajibisha majambazi wavaa suti!
Kulingana na uchunguzi wetu tumeitimisha kuwa jaji mkuu pamoja na maofisa wa mahakama walikwenda Washington DC kwa ajili ya kitu kimoja tu nacho ni kujadili suala zima la issue ya acount ya Escrow na mpaka hivi sasa hakuna ushahidi wowote kuhusiana na uwepo wa semina unless watoe picha zinazoonesha semina hiyo ambayo wahusika walidai walikwenda kuhudhuria na siyo kuonana na JK.
Ilishasemwa tangu awali kwamba mtuhumiwa nambari moja wa sakata hili ni Rais Kikwete himself. Sasa zigo lote hilo lipo kichwani pake! ..
 
Kwa hiyo ile barua haikutoka mahakamani bali ilito kwa balozi sefue kwa kutumia mgongo wa mahakama? Mmeniacha gizan
 
Ni wakati muuafka wananchi wakachukua hatua za kuadabisha ccm bila hivyo haya mambo yatakuwa yakitokea kila siku. Shime watanzania na tuanze na huu uchaguzi wa serekali za mitaa tuyatoe haya majitu yasiyo na uchungu na sisi.

Kuadabisha CCM kwenye kura is one thing. Lakini kwa sasa kinachotakiwa ni kila mtu kuwajibika kuhusiana na ushiriki wake katika escrow pasipo kujali nafasi yake katika ngazi yo yote.
 
Naamini katika Watanzani milioni 50 lazima kuna mtu mwenye data na uthibitisho usio shaka wa wahusika wa huu wizi.
Tukianza na Mh. Kafulila mwenyewe na 'karatasi zake za kufungia vitumbua' mpaka Mh. Muhongo mwenye 'canter 10' zilizojaa makaratasi ya ushahidi kuwa Escarow si pesa za umma.
Na kwa sababu awamu ya nne ilibase zaidi kwenye kujenga mabillionea binafsi badala ya kujenga chama na sasa chama kimegawanyika, ni swala la muda watatajana tu.
wananchi tubadilike sasa, atakayetajwa tuhakikishe anafikishwa kwenye vyombo vya sheria badala ya kuombwa kurudisha alichopora. Hata kama mahakama zetu zinasimama nyuma ya watuhumiwa basi tuangalia uwezekano wa mahakama kama za EAC au hata ICC ili haki itendeke na kuonekana imetendeka.
 
Kunavitu vingine vya kitoto kweli hivi lini sefue katoa tamko kuwa suala la escrow lisijadiliwe unaweza kuweka ushahidi zaidi.
 
Kuadabisha CCM kwenye kura is one thing. Lakini kwa sasa kinachotakiwa ni kila mtu kuwajibika kuhusiana na ushiriki wake katika escrow pasipo kujali nafasi yake katika ngazi yo yote.
Ha ha ha ha ha kwani zitto naye ni mwanaccm make zitto kashiriki wizi wa hizi pesa na kuhongwa sana.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    123.6 KB · Views: 740
Ni aibu kubwa muhimili kama mahakama unajiingiza kwenye harakati za uongo kwa masilahi ya wachache. Nchi ikifikia mahali Mahakama inageuzwa kuwa danguro ujue mwisho wa utwala huo umefika ila unalazimishwa kuwepo
Ndo ujue Prof Busha alikomtoa Jaji Chande na kumvika taji la Chief Justice,haikuwa bure.
Prof Busha ndiye chanzo cha yote haya.Imekula kwetu.
 
Hili linajulikana. Mimi niliujua ukweli huu bila hata ya kufanya utafiti.

Wanadhani wanaweza kutudanganya lakini tupo tunaoweza kusoma "katikati ya mistari".

Mfano: Jana, Mama Jacqueline Maleko, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE alinukuliwa akizungumzia kuhusu TANTRADE kuwatafutia VIJANA masoko ya mazao yao ya kilimo. "Keyword" hapa ni vijana. Kwa nini?

Takriban wiki mbili zilizopita kulikuwa na Kongamano lililofanyika Dar es Salaam, TANTRADE ikiwa mmoja wa wadau wakuu wa Kongamano hilo, lililoshirikisha kampuni ya ushauri ya Marekani, CMS Consultants.

Kaulimbiu ya Serikali kwenye komgamano hilo ilikuwa "Vijana changamkieni fursa za wawekezaji kutoka Marekani".

Sasa hebu tujiulize, hao VIJANA ni akina nani?

1. Ni vijana wangapi Tanzania wana uwezo wa kuchangamkia fursa hizo?

2. Fursa hizo ni za kuajiriwa au kuwa wabia?

3. Je, vijana hao wameandaliwa kiuchumi kuweza kuchangamkia fursa hizo?

CCM inajua kwamba HAITAPITA mwakani kwa sababu IPTL imeichafua. Wanajaribu kuzima moto kwa mafuta ya petroli. Kwa hiyo mbinu iliyopo, ambayo nayo inatumia mafuta ya taa na wala si mchanga, ni kujaribu kuwadanganya VIJANA kwamba wanatambuliwa, lakini hizi ni SIASA TU!

Mfa maji daima HESHI KUTAPATAPA!
 
  • Thanks
Reactions: 911
Ha ha ha ha ha kwani zitto naye ni mwanaccm make zitto kashiriki wizi wa hizi pesa na kuhongwa sana.
Acha kuwa mtoto, mapenzi yako ka Ccm yanaijengea chuki CCM yako kwa jamii. Jamii ni kubwa kuliko wewe binafsi mchumia tumbo
 
Back
Top Bottom