Ukweli kuhusu nyota ya mtu kwenye mahusiano na mafanikio.

Tairus

JF-Expert Member
Mar 13, 2013
676
1,055
Nianze kwa kutanguliza salamu

Nina imani kubwa kuwa umesikia kihusu maswala yahusuyo nyota ya binadamu mara nyingi.Swali la msingi apa ni kuwa kuna uhalisia wowote katika hili.

Imani yangu ni kuwa hivi vitu havina uhalisia bali ni sisi binadamu tumejijengea mazoea tuu na mwisho wa siku tunapotea.

Iko ivi watu wanaendekeza ushirikina kwa miavuli ya kusafisha nyota.
Unambiwa nyota yako imechafuka unaamini ni sawa na mtu akikuwambia flani kakuloga bila uthibitisho.

Nyota ni nini..Tunaambiwa ni ule mvuto au nuru binadamu anazaliwa nayo.
Tunaambiwa nuru hii hufifia na kung'aa
Ikififia una hali mbaya na ikingaa una hali nzuri.

Tunaambiwa kuwa kila unapompa mganga nafasi ya kuipitia nyota yako na kuisafisha unampa pia uwezo wa kuichafua kwa maana ya kuamisha baraka zilizokuwa kwa ajili yako na kumuamishia mteja wake mwingine anapokuja.
Kwa hali hiyo kila siku utakuwa unarudi kwa kalumanzira na yeye anafanya kuwapanga tuu.

Pia tuambiwa tuoe wanawake ambao nyota zetu zinaendana lakin bado kila siku watu wanaachana.

Baada ya hayo turudi kwenye mada.
Mganga ni nan na nan kampa uwezo wa kucheza na nyota za watu...je ni kweli ushawai kusafisha nyota na ukafanikiwa.
Kama Mungu alitaka uwe mtu fulani toka mwanzo kwa nin akubal mtu mwingine aharibu.

Utakubaliana na mimi kuwa kinachofanyika ni kiini macho tuu nyota ya mtu ipo na hakuna wa kuisafisha wala kuichafua sababu alipangalo Mungu mwanadamu hawezi pangua.

Nakaribisha wataalamu wa haya maswala kwa uchambuzi zaidi yakinifu.
 
Hakuna uwalisia ni miongoni mwa shirki

Kuwamini mambo hayo humpelekea mja kuingia katika madhambi makubwa

Pia hupelekea kutokuamini katika nguzo ya Qadar(kuwa kila kinachotokea cha kheri au shari hupangwa)
 
Hakuna cha nyota, ni dhana tu ambazo wavivu hutumia kujifariji...utaskia 'baba bakari usimuone vile, ana nyota ya mizani, ndomana duka lake linamlipa vizuri'
 
Ni kama ngonjera za kidini,zote ni ngonjera tu.dini nzuri ni kusoma vizuri na kuwa na elimu nzuri.
 
Binafsi naweza kubali haya mambo ya nyota.

Nilikaa nikajigundua wanawake ninaofanana nao nyota ( yani tuliozaliwa miezi inayofanana ) ninadumu nao sana kwny mahusiano tofaut na wengine..

Kuna mdada niliwai kutana nae mzuri balaaa, nilimsemesha akaitikia wito na namba akanipa. Bdae akawa mpenzi wangu..

Ni bahati mbaya tu alikuwa tayali n mke wa mtu. Ila alinipenda sanaa, aliniforce nimuoe kitu ambacho hakikuwezekana..

Ilikuwa nikiwa nae napata pesa sanaa. Ye pia niliwai mwambia hali hii.

Nilikuja kugundua tunashare tar na mwezi mmoja wa kuzaliwa yani tar11/11.

Kwa hiyo haya mambo yapo wakuu..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom