Ukweli kuhusu Ndege ya Air Tanzania "kuegeshwa" bila kuruka

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Wakuu salamu,sababu ya tofauti ya majira ya huku nilipo na huko nyumbani,basi kuna mambo yamekuwa yakinipita humu jukwaani,ama ninakuwa usingizini au nakuwa busy na kazi iliyonileta.

Nimekuta msgs nyingi na "mentions" nyingi sana za barafu watu wakibishana kuhusu ndege ya ATCL kuharibika.

Kifupi na kwa taarifa rasmi za kiufundi japo nipo mbali na nyumbani ni kuwa,ndege hiyo ya ATCL haijaharibika na sio kweli kuwa eti mainjinia 50 wameshindwa kuitengeneza.Daah!!Jamani huu uongo na masimango kwa shirika letu la ndege inatoka wapi?

Ni kweli hata mimi kuna mambo sikubaliani na JPM,hasa katika masuala ya bunge kuonekana mubashara na uminywaji wa upinzani,lakini simtakii mabaya wala kuizushia serikali yake uwongo.Yoyote unaemuuliza,wewe umepata wapi taarifa hizo?Atakwambia "Mange kasema"....Huyu anayetajwa ni Mhandisi?

Kwa wale waliofuatilia ujio wa ndege hizi wakati zinaletwa Tanzania,watakumbuka kuwa ndege moja ilitangulia kabla ya nyingine,iliyotangulia ni ile iliyokuja na namba za usajili za Canada za C-FHNF ambapo ilipofika Tanzania ikapewa namba ya 5H-TCB.

Hii 5H-TCB ndio ilianza kufanya kazi mbele ya ile ya pili yenye usajili wa 5H-TCD.Kwa hiyo hata kwa masaa ya kukaa hewani,hii iliyotangulia ya 5H-TCB ndiyo yenye masaa mengi hewani kuliko 5H-TCD iliyokuja baadae na kuanza kufanya kazi.

Ndege iliyoegeshwa kwa muda kwa ajili ya matengenezo madogo ni 5H-TCB,na hii si Tanzania tu,bali dunia nzima.Ndege inapofikisha masaa kadhaa kuwa hewani,let say masaa 12000 hewani,inatakiwa kuwa grounded ili kuweza kubadilishiwa vifaa kadhaa ambavyo masaa yake yanakuwa yamekwisha kwa vyenyewe kutimika.

Hii ni hata kwenye magari,tunashauriwa kutumia matairi ya magari kwa masaa kadhaa,yakipita hayo masaa basi tunapaswa kubadilisha,lakini kiswahili-swahili watu huendesha tu magari mpaka yanawapasukia na kupata ajali.Usafiri wa anga ni tofauti,mambo ya "safety" ni jambo la kwanza na la muhimu.

Kilichotokea kwa ndege moja ya ATCL ni kuwa grounded kwa sababu za kiufundi na kiusalama (safety),ili kufanyiwa "cheki" ya baadhi ya vifaa na kuweza kubadilishwa ili irudi hewani kwa uhakika zaidi.Hii ni kote duniani.

Sisi tunaweza kuona kwa wepesi sababu shirika letu la ATCL lina ndege mbili tu,moja ikienda "hangar" (maintanance area) inakuwa rahisi kujulikana sababu moja tu ndio inabaki ku-operate,lakini jambo hili ni kawaida,leo ukienda Kenya utakuta ndege zilizoegeshwa sbb ya masaa kupita,ukienda KLM,Swiss International,South Africa Airways,Qatar nk.Si jambo la ajabu,kwanini libebwe kama mada?

ATCL ni moja ya kampuni yenye wahandisi wazuri walio wazawa.Na kwa aina ya mkataba wa kampuni ya bombardier,mpaka sasa ATCL imekuwa "attached" na mtaalamu mmoja (Consultant) toka Canada,atakayekuwa kwa muda fulani kama mshauri wa kiufundi moja kwa moja toka kiwandani.

Habari hizo tuzipuuze,si njema kwa mafanikio ya heri ya shirika letu.Tuwatie moyo ATCL,inawasaidia sana watu katika usafiri wa ndani ya nchi.Kwa sasa safari zake za Dodoma,K'njaro,Tabora,Kigoma,Mtwara na Songea zimeokoa muda na kusaidia watu wengi.Safari ya Hahaya-Commoro imekuwa na mafanikio makubwa na yenye faida....Sio kila kitu yule "Binti" akisema kinakuwa na ukweli....

ATCL-The Wings of The Kilimanjaro.......
 
Back
Top Bottom