Ukweli kuhusu mileage

Mmwaminifu

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
1,129
302
Heshima kwenu wakuu!

Kwanza niseme kuwa sio mtaalamu katika mambo ya magari.

Naomba kujua ukweli kuhusu ubora wa gari unavopungua kadri gari inavozidi kutembea. Ni kilometa ngapi ambazo gari ikishafika hiyo gari inakuwa imepoteza ubora wake?

Naomba ushauri hasa kwa gari aina ya Noah.

Natanguliza shukurani!
 
Swala kubwa lipo kwenye Engine..... The distance traveled by car the inefficient of the engine yaani umbali mrefu uliotembelewa na gari ni kupungua uwezo wa engine
 
Heshima kwenu wakuu!

Kwanza niseme kuwa sio mtaalamu katika mambo ya magari.

Naomba kujua ukweli kuhusu ubora wa gari unavopungua kadri gari inavozidi kutembea. Ni kilometa ngapi ambazo gari ikishafika hiyo gari inakuwa imepoteza ubora wake?

Naomba ushauri hasa kwa gari aina ya Noah.

Natanguliza shukurani!
Umbali gari liliotembea sio issue, unavonunua gari kwa Mtanzania angalia/zingatia vitu hivi:

1. Service history. Na wengi hatunaga logbook ya service kabisa. Inabidi uwe na kitabu una record kila kitu ulichofanya/badirisha kwenye gari, tarehe na gharama yake.

2. Wamiliki waliopita. Gari kama imeshapita kwenye mikono zaidi ya 4 hatari sana. Pia ata umri status na jinsia. Magari yaliomilikiwa na vijana mengi sio well maintained na serviced. Wazee wa cheap, gereji za vichochoroni. Ndio maana madalali wetu utasikia gari alikua anatumia mwanamke au muhindi.

3. Angalia accident records. Angalia kama airbags zimewahi kulipuka au mbele chasis kama imenyooshwa. Viajali vingine vya kukwanguana na bodaboda vinavumilika. Ata rangi kama imerudiwa sio mbaya as long iko poa. Dar kurudia rangi kawaida.

4. Wewe angalia exterior na interior ya gari. Icho ndio cha kwanza. Ukiipenda test drive. Ukiridhika na uendeshaji wake, muite fundi makenika acheki sasa technical issues. Hapo jitahidi fundi asije kununuliwa na muuzaji. Wanaishara zao.

5. Gari modifications zikiwa nyingi jiulize mara mbili. Muffler, spoilers, tuned engine etc unless uwe fan au ndio vitu unavovitaka.

Hayo ni baadhi ambayo uwa tunayasahau kuyatilia maanani wakati wa kununua gari. Mengine yashasemwa sana humu.
 
Achana na kuangalia kilomita au plate number, wengi wanafeli hapo wanajikuta wananunua magari mabovu kwa ajili tu kakuta namba mpya au kilometers chache.

Gari inaweza ikawa na kilometers chache au namba mpya lakini ikiwa ni mbovu tu kutokana na matumizi
mabaya.

Kikubwa angalia historia ya hiyo gari kama mdau hapo juu alivyoelezea, na uwe na fundi wako unaemuamini.
 
Ukinunua gari hapa Tz usidanganyike kwa kuangalia distance covered au namba sijui D au C....wabongo ni wapiga dili..
Wengi wamekushauri vizuri lakini naomba niongezee kidogo.
Miaka minne iliyopita niliagiza Nissan japan yenye 118k KM kwenye dashboard mapaka leo hii gari kwenye engine nimewahi kubadili plug tu na rubber boot za ignition coil...kila nikifungua bonnet watu wanaona wivu engine inavyowaka upya.
Nimesafiri nayo safari kadhaa ikiwepo Dar to Arusha na kwendea kazini kila mara.
Gari bado ipo vizuri sana.

Sasa turudi upabde wa pili...kuna watu nawafahamu na IST zao wamezinunua hapa kwenye yard zetu za bongo zikiwa na kilomita 40000 na wengine elfu 60000 lakini lakini zimeshaanza kuwasumbua sana na wameshabadili vitu kibao na wengine wameshafungua engine kwa mafundi.

Hili linatufundisha kuwa wabongo wanachezea mileage za magari ili kuwapumbaza wateja...utakuta gari inasoma km 40000 lakini kiuhalisia imetembea zaidi ya km 160 k..

Nilichojifunza ni bora kununua gari japani lenye 150k kuliko gari lenye mileage ya 60k hapa bongo kama huna uzoefu wa magari.

Ukinunua gari bongo zingatia wadau walivyoshauri...ukikimbilia mileage au registration number eti ni D lazima uliwe
 
Kikubwa ni kuangalia historia ya gari tu, mimi nilikuwa na suzuki vitara namba ABN nimeuza majuzi tu, ilikuwa na kilometer karibu laki 2, lakini chombo kilikuwa mashine haswa, nimesafiri nayo safari za Congo mara 2, Malawi mara 1, mikoani ndio usiseme, nilikuwa naiamini mno kwa safari kutokana na jinsi nilivyokuwa naijali service.
 
Ukinunua gari hapa Tz usidanganyike kwa kuangalia distance covered au namba sijui D au C....wabongo ni wapiga dili..
Wengi wamekushauri vizuri lakini naomba niongezee kidogo.
Miaka minne iliyopita niliagiza Nissan japan yenye 118k KM kwenye dashboard mapaka leo hii gari kwenye engine nimewahi kubadili plug tu na rubber boot za ignition coil...kila nikifungua bonnet watu wanaona wivu engine inavyowaka upya.
Nimesafiri nayo safari kadhaa ikiwepo Dar to Arusha na kwendea kazini kila mara.
Gari bado ipo vizuri sana.

Sasa turudi upabde wa pili...kuna watu nawafahamu na IST zao wamezinunua hapa kwenye yard zetu za bongo zikiwa na kilomita 40000 na wengine elfu 60000 lakini lakini zimeshaanza kuwasumbua sana na wameshabadili vitu kibao na wengine wameshafungua engine kwa mafundi.

Hili linatufundisha kuwa wabongo wanachezea mileage za magari ili kuwapumbaza wateja...utakuta gari inasoma km 40000 lakini kiuhalisia imetembea zaidi ya km 160 k..

Nilichojifunza ni bora kununua gari japani lenye 150k kuliko gari lenye mileage ya 60k hapa bongo kama huna uzoefu wa magari.

Ukinunua gari bongo zingatia wadau walivyoshauri...ukikimbilia mileage au registration number eti ni D lazima uliwe
Ushauri mzuri sana.
 
Back
Top Bottom