Ukweli kuhusu mgomo na madai ya madaktari Tanzania

Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitega alitaja madai yaliyowasilishwa katika kamati hiyo kuwa ni:-

1. Hali bora ya mazingira ya utoaji afya nchini,
2. Ongezeko la mishahara,
3. Posho za kufanya kazi katika mazingira magumu,
4. Posho za kufanya kazi katika mazingira hatarishi
5. Posho za kuitwa kazini.

Madaktari wana madai yao makuu 4 tu! Hilo la mazingira bora ya kazi limeingizwa tu kujazia ionekane kama wao wapo for maslahi ya wananchi. Kimsingi hilo la mazingira bora ya kazi nalo linawahusu wao binafsi kwenye mambo kama Kumpatia daktari nyumba , gari, mkopo nk wala haihusu kitanda cha mgonjwa.
 
Madai 12, 10 ni madai ya mshahara na posho! Moja tu ndio kuimarisha huduma za afya
VX moja hainunui CT Scanner,though i believe the govt can afford to buy one in every major hospital.

Hilo la kuboresha mazingira lenyewe halihusu kitanda cha mgonjwa wala CT SCANNER bali ni kumpa daktari gari ,nyumba nk ili aweze kuishi "komfotabo"
 
Unajua sisi wengine husoma vitu tukavipima uzito wake kisha unamtazama mtu usoni na kumkoma nyani giledi. Kinachonishanga hapa janvini ni kwamba watu wengi sana wanapenda kutumia neno kuboresha mazingira ya kazi kama ndio kiungo kikubwa cha madai ya madaktari wakati sio kweli. Jamani madaktari mkisema mnataka mshahara mkubwa zaidi bila hizi hadithi nyingine kuna kosa gani? Hivi mnatufanya sisi hatujui kusoma au wajinga saaana kutufanya vilaza wakati tumesha amka longtime.

Katika orodha ya madai, MAZINGIRA BORA ni ya 11 na kati na madai yote 12, na wala halina uzito kihivyo lakini kila naposoma mnaweka mazingira ya kazi mbele ya kila kitu..Hakuna lolote linalotuhusu hapa wala kuwatazama wagonjwa isipokuwa ni maslahi yenu tu kwa hiyo mnazungusha maneno mengi ya nini?. Majibu ya madaktari kupinga hotuba ya rais jana tu, Madaktari wamesema wazi kwamba swala la kluboresha mazingira ilikuwa USHAURI kwa serikali... Wamesema, nendeni mkaisome tena na tena lakini hapa JF ndio lugha kubwa, hivyo nashindwa kuelewa wanapokuja hapa na kutumia sana neno hili kuboresha mazingira wakati halina uzito kwao ndio nini?

Hakuna dai hata moja linaloitaka serikali iboreshe miundombinu au maendeleo ya sekta hiyo, sioni mahala wakiomba serikali kupiga marufuku madawa feki kutoka China au India, au hata ukosekanaji wa madawa kwa magonjwa fulani, Hizo CT scan zenyewe zinaongwa kama kachumbari kukoleza madai yao lakini hakuna hatab moja linalozungumzia kuboresha huduma ya AFYA nchini aidha kwa kusisitiza fungu kubwa zaidi ktk bajeti ya Afya au upanuzi wa miundombinu na vifaa maana madaktari sasa tunao japokuwa bado hawatoshi..SIONI... Bado hoja zao kubwa ni kuongeza zaidi na zaidi matumizi ya ndani ya kawaida yaani ktk 12 yote kuongeza tu gharama za matumizi ya kawaida sii maendeleo. Na kwa mtu kama miye sioni kabisa faida kwa wmwananchi wala sintokubaliana na maneno ya kwamba Daktari akilipwa vizuri basi huduma nayo itakuwa nzuri.. It's all about YOU!

Mnayo kila haki ya kuweka madai yenu lakini msitafute sympathy ya wananchi wakati mazungumzo na serikali mmeyafanya kisiri siri kiasi kwamba serikali imekubali kuwaongezea mishahara asilimi 15 hadi 20 lakini kumbe nyie hamtaki mnachotaka ni asilimia 35. Mimi nilidhani hamkupewa offer kabisa wala. Kwa hiyo kumbe mazungumzo yapo na mmepewa offer sio kwamba serikali imekataa kabisa ila hamkubaliani kiwango gani cha mshahara kiongezwe. Nani alotudanganya zaidi kama sio nyie kusema serikali haitaki kufikia suluhu, kumbe kuna mambo 7 mlokwisha kubaliana..

Tatu, mambo yote mnayolaani kuhusu Wabunge nashangaa ndiyo mnayataka nanyi pia sasa nashindwa kuelewa kama nyie ndio mnayo haki zaidi ya kupewa mashangingi badala ya kununua Ambulance. Halafu hizi hadithi za kusema mkifukuzwa kazi mtakwenda Rwanda, Egypt na kadhalika sii kigezo kizuri kabisa kwa sababu mmeombwa kuacha kazi hamtaki ila mnaendeleza mgomo nchini wakati Rwanda na Egypt wanawahitaji - NENDNI huko Rwanda na Egypt nasi tutaleta kutoka madaktari kutoka Iran na Kenya kwani hii sii dunia ya utandawazi!. Haya sii maneno kabisa ya mtu alosoma na mwenye kufahamu kazi yake bali vitisho.

Nne, Swala la kutumia mishahara ya nchi nyinginezo sio kigezo kabisa. Ni Ujinga mkubwa sana mnatumia kigezo cha nchi nyingine kwa sababu hao wenzenu walisomea Udaktari kwa kulipa ada kubwa sana ambayo ilifikia Usd 200,000 au zaidi, Je, wewe Mdanganyika ulilipa hizo? Sasa huyu Mwenzako aliyejipinda wazazi wake kulipia ada ya Usd 200,000 awe sawa na wewe ulosomeshwa bure kutokana na mpango wa serikali ktk kufuta adui MARADHI leo umesha sahau na kuwa haki yako wewe? Halafu kibaya zaidi sii tu unataka mshahara mkubwa bali posho, mashangingi na nyumba kama kwamba hata kukusomesha wewe bure ilikuwa kosa kubwa sana kwa serikali.

Jamani ktk nchi za Kiafrika nambieni ni nchi gani Daktari anapokea mshahara mkubwa kuliko mbunge au mwanasiasa?..Hii ni vita mpya ambayo inataka nguvu kubwa ya wananchi na sio kuboresha viwango vya watalaaam viwe sawa au zaidi ya wanasiasa, dawa pekee ni kushusha viwango vya mishahara ya wanasiasa iwe chini ya wataalam ndio pekee Afrika tunaweza kuiona nuru ya maendeleo ya kesho. Bila hivyo tutaendelea kugawana umaskini (kupokonyana) na kutegemea misaada toka nje kama wakimbizi wa Somalia ktk makambi.

Yes, serikali yetu inazembea sehemu zote hata imefikia JK kuitwa mzembe! Lakini binafsi yangu najua fika kwamba JK sio mzembe hata kidogo isipokuwa anajua vema anachokifanya wala sii uzembe. Wananchiu na wanasiasa nchini wamemsoma vibaya sana kiasi kwamba wamechanganyikiwa kama hili swala la Madaktari kwa sababu mnashindwa kutazama ndani au nje ya box. JK ni mwanasiasa ambaye pamoja na marais waliopita wameamua kuifisadi nchi, kuiuza nchi na kujenga matabaka haya ya maskini na matajiri kwa matayarisho ya tanzania mpya ndani ya Ubepari.

Hivyo yeye na familia yake, viongozi wote na wana CCM wapo ktk kazi kubwa ya kuchota utajiri wa nchii hii toka mali ya serikali na kuwa ya watu binafsi (yao) na JK anaifanya kazi hiyo kisawasawa ndio maana anapendwa na chama. Katika transition ya kiuchumi kuna transition pia ya umiliki wa mali za Taifa, hivyo JK anachokifanya sasa hivi ni mpango maalum wa kujitajirisha wao ambao ulianza toka wakati wa Mwinyi hakuna ujenzi wa miundombinu mipya zaidi ya kuficha mashimo -Bongo Tambarare!

Hapa ndipo napopingana na viongozi wa Upinzani iwe hata Chadema ambao wanafikiri kwamba viongozi wa CCM wanajali kelele za mlangoni au pengine wabunge wa CCM wanaitazama picha ile ile wanayoitazama wao ktk ujenzi wa Taifa. Hapana ndugu zangui hakuna tena UZALENDO hivyo kama kifdikra unapingana na uongozi wa JK na kule tunakoelekea basi huna budi pia kupinga yote yatokanayo na utawala huu kwa sababu wanachokitaka madaktari wetu ni ktk kuendeleza ujenzi wa Ulaji nchini badala ya huduma bora hasa ktk vita yetu kubwa ya kuondokana na adui maradhi. Jiunge na mageuzi ya kifikra kwa maana vita yetu kubwa ilikuwa kuondokana na Umaskini, Ujinga na Maradhi na ndio maana vijana wetu walisoma bure leo tuna madaktari karibu 16,000, sasa maadam wametokea vibaraka wanaokwenda kinyume cha malengo basi lazima tuwapige vita wote ipaswavyo.
 
Nne, Swala la kutumia mishahara ya nchi nyinginezo sio kigezo kabisa. Ni Ujinga mkuwba sana mnatumia kwa sababu hao wenzenu walisomea Udaktari kwa kulipa ada kubwa sana ambayo ilifikia Usd 200,000 na zaidi wewe ulilipa hizo? Sasa huyu Mwenzako aliyejipinda kulipia ada ya Usd 200,000 awe sawa na wewe ulosomeshwa bure kwa mpango wa serikali ktk kufuta adui MARADHI? Halafu kibaya zaidi sii tu unataka mshahara balki posho, mashangingi na nyumba kama kwamba hata kukusomesha wewe bure ilikuwa kosa kubwa sana kwa serikali.

Wape habari hawa madaktari wetu, wao wanajua Upanga magharibi tu waende wakapekue wajifunze kidogo.

Uwafahamishe pia kwamba utendaji wao hauridhishi hata kipindi ambacho hamna mgomo hapo Muhimbili mwananchi mvuja jasho anadaiwa rushwa pamoja na mshahara wao wa TZS 900,000. Wakajipange upya kwa kweli tumewastukia na kipindi kile cha Nyerere hawa wangeipata freshi angetimua wote angeleta warusi halafu wasingepata kazi sehemu yeyote wangerudi kuendeleza kilimo kwanza.
 
kama wabunge wanalipwa 7.5M mkopo wa gari 90M bado posho za vikao bado wako kwenye kamati za bunge wanapokea posho bado kama wakina manyanya wanapokea mshahara wa ubunge na ukuu wa mkoa na wabunge wakimaliza miaka yao mitano wana kifuta jasho 60M kwanini kwanini madaktari 3.5M ishindikane?? wabunge wenyewe ndio hao tunaona wanasinzia tu bungeni na kutukana huu si wenda wazimu hata wanyama wataona kuw amadaktari hatuwatendei haki.

Hapo ndipo huwa nawashangaa Watanzania wenzangu! Hivi ni kitu gani kime-spring up suddenly cha kuonyesha kwamba DUNIA ni fani ya udaktari full stop, taluma nyingine hazina mshiko! Nilisha uliza humu kwamba: Hivi madaktari hawa wana habari kwamba kazi zao zina laisishwa kwa kutegemea by 100% vitendea kazi vilivyo vumbuliwa/kuhundwa na wataalamu weledi wa fani nyingine kabisa ambao hawakukimbia (hesabu), si hilo tu vile vile wataalam hao HAWAKO self-cetered, wala hawana hulka za kujaribu kutumia mbinu za kutafuta public sympathy wakati wenyewe hawajali PUBLIC plight katika harakati zao za kudai a tall order kutoka TAIFA lao maskini! Wako tofauti kabisa kama ilivyo mbingu na DUNIA.

Hapa natoa mifano kidogo wa kuonyesha kwamba taluma hizi zinategemeana, hivyo haipendezi kikundi cha watalaam fulani kujiona wenyewe zaidi ndani ya TAIFA letu kwa hiyo watalaam/wafanyakazi wa fani nyingine si lolote si chochote:


  • No. One - Medical Instrumentation ambazo ndio macho ya madaktari na nyigi zimebuniwa/kuhundwa na Electronic Engineers be it CT scans ambazo wanazungumzia kila siku hapa, MRs, X-Rays, Computers -Digital/Analouge na sensor/trasducers zake zote za kuchunguza mwenendo wa moyo, Brain waves na electrical impulses nyigine of interest kwao. Cha ajabu ni kwamba madaktari wanakalishwa chini na ma-Engineers hao kupewa somo jinsi ya ku-interpret wanacho kiona kwenye screen au hard copy print out, je na wenyewe wangekosa UTU wakawanyanganya vitu vyote vilivyo tajwa hapo juu mgemuduje kazi zenu?


  • No.Two - Wataalamu wa madawa, bila ya watu muhimu kama hawa nani angepona, labda wote tungeishia kwenye MAOBI au wezee wa UPAKO na madawa ya kienyeji - oh yes back to stone AGE, dot com would have sounded Greek to US!


  • No.Three - Life supporting Machines za aina zote, nani kuhunda/kubuni mashine hizo kama sio ma-Engineers wa Electronics na Mechanical, bila nyenzo kama hizo madaktari wengeweza kweli kumudu kwa ufanisi wagonjwa walio lazwa ICU?


  • No.Four - Mikasi,scapels,nguo za nje na ndani, viatu, groves, surgical instruments and what have you? Vyote hivyo vimetegenezwa na wataalamu ambao si madaktari lakini vina umuhimu wa kipekee katika kazi zenu.

Hapa nimezungumzia kama utani kidogo lakini niko serious, nataka kukumbushia Watanzania wenzangu na nyinyi kwamba utalaamu wenu unategemeana sana na talamu za watu wengine kwa hiyo msije mkajisahau sana. Baada ya kumsikiliza JK alicho kuwa anasema jana nilikumbuka kisa cha Ngamia na Mwarabu nilicho wahi kusoma utotoni - ngamia alimuomba Mwarabu aingize kichwa chake kwenye hema lake kujikinga baridi/mvua (sikumbuki vizuri) Mwarabu wa watu kamkubalia ngamia, baada ya muda Ngamia kasema kuingiza kichwa akutoshi, shingo nalo linasikia baridi ebu nihingize na shingo kabisa; Mwarabu kasita kidogo mwishowe kamjibu ngamia kwamba ingiza shingo kidogo alafu basi hakuna nafasi ya ziada kwenye HEMA, kabla Mwarabu ajakaa vizuri Ngamia kaingia mzima mzima na kumtupa nje ya HEMA kwenye baridi Mwarabu wa watu. Mimi sina shaka mambo ya hapa kwetu yalikuwa yanalenga kuelekea huko huko kwenye KISA CHA MWARABU! Nilishangaa sana mambo Serikali yetu iliyo kuwa inayafanya behind the scene ili kuwa-please madaktari, nini Serikali ilicho pata at the end of the day, baada ya kuonyesha ugwana wote huo aganist all odds!! - Ikawa inawekwa kwenye endless loop (watalaam wa computer wananielewa) inatembezwa fang fang back and forth like a YOYO! are we NORMAL?
 
Cha msingi hapa ni kuangalia je hayo madai yao yanawezekana? Serikali ina uwezo wa kulipa hayo madai yao? Ukiwa na kichwa chepesi" light weight thinking" unaweza kusema kama alivyosema Rais kuwa haiwezekani. Ila kwa watu wanofirikiri sawa sawa bila ubabaishaji watakuambia,ukipewa umuhimu wa dakatari na kile anachodai utaona ni kidogo sana(peanuts). Inawezekanaje basi? Serikali ikihamua kubana matumizi ya anasa hili linawezekana. Hatua za kuchukuwa-:
  1. Moja piga mnada yale mashangi( viwanda vidogo vinavyotembea barabarani na kumeza rasilimali bila kuzalisha) na nunua magari madogo ya kiofisi kama suzuki Vitara
  2. Punguza baraza la mawaziri toka 55 hadi 15 au 18(hapa wamezidi sana).
  3. Unganisha wizara zenye malengo yanayofanafana an uzi-streamline
  4. Futa ofisi za Wakuu wa Wilaya na MDAS zote- abaki mkurugenzi maana ndiye anayefanya kazi na wananchi
  5. Futa ofisi zote za wakuu wa mikoa na ajiriwe Mkurugenzi wa Mkoa moja tu ambaye atafanya kazi za serikali.
  6. Fumua mikataba yote ya madini na kuchukuwa uzoefu wa Bostwana ili tupate mapato mazuri
  7. Ondoa wabunge wa kuteuliwa
  8. Futa posho zote za kipuuzi na uache zile muhimu tu
  9. Futa safari za nje na hasa zile za Rais na mawaziri amabazo hazina tija
  10. Weka bandari ya DAR sawasawa iwe ni mashine ya kutoa hela
  11. Tourist Board ivunjwe na kuundwa upya ipewe hela ya kutosha ya kutangaza utalii na ipewe "benchmark" ya mapato ya Utalii. Kama CEO akichemsha apigwe chini
  12. Ipe kazi TRA ya kufanya utafiti ndani ya miezi sita wa namna ya kuongeza wigo wa kodi na waje na mpango ambao ni wa ukweli.

Je haya machache yakifanyika na kama kweli daktari ana umuhimu kama alivyosema Raisi wetu hatuwezi kuwalipa fedha hiyo na kuboresha mazingira yao ya kufanyia kazi?

Tatizo hapa ni kuwa Tanzania kama taifa hatuna vipau mbele, maana huwezi katika mazingira ya kutaka kutengeneza uchumi wa kati(middle income country) halafu unakuwa na vipau mbele 5 au 8 au zaidi. Haiwezekani. Lazima uchague lipi unaenda nalo hadi mwisho. Mfano chuma kinatumika kila mahali na chuma Tanzania kipo kingi tu, sasa kinachoshindika kuwekeza kwenye chuma halafu kinyanyue sekta nyingine ni nini?

Inawezekana mgomo wa madaktari ni sehemu nzuri ya kuanza kujitafakari upya na kuangalia namana tunavyoendesha mambo yetu.
Kama tukihamua kuacha ubabaishaji,mizengwe,u-mungumtu wa viongozi,dharau na ulimbukeni wa viongozi,ubinafsi,mantiki zilizopinda,ushabiki wa vyama na au watu,siasa za maji taka,kebehi, mawazo na maono yaliyoshindwa kabla hata hayajaanza, kuingiza siasa pale isipohitajika,uvivu wa kufikiri sawasawa na kuzaliwa upya yamkini tutaona kuwa tatizo la madaktari ni dogo sana.

Nadhani udogo wa mawazo yetu ndio unatufanya kufanya haya tunayofanyiana leo. Tunafanyiana ubabe sisi wenyewe, tunakanyagana sisi wenyewe,tanazibiana riziki sisi wenyewe- kwamba mimi nipate yeye asipate. Tunafanyiana hujuma sisi wenyewe. Tunajilipa posho nono wakati wenzetu hawana uhakika ya mia tano ya kununua unga aweze kula ugali jioni. Si vibaya kujilipa posho, ila je umetenda haki? Kazi uliyotumwa kufanya ili yule anaehangaika na mia tano apate 2000 umeifanya? Huu ni udogo wa mawazo tu.

Cha ajabu ni kuwa wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Africa tulitumia fedha nyingi na rasilimali watu kufanikisha azma ya ukombozi wa Waafrika wenzetu. Tanzania ikawa ni taifa linaloheshimika sana barani Africa Sasa kama tuliweza huko kwa nini kwa kutumia nguvu,kasi na "spirit" ilele kuboresha maisha ya madaktari wetu na wananchi wetu? Kwa nini kwa kutumia rasilimali hizi tusiwe mfano wa kuigwa Afrika kwa kabidilisha maisha ya wananchi wetu ikiwa ni pamoja na madaktari? Nadhani udogo wa mawazo,ulimbukeni na ulofa vinatutesa sana

Mgomo wa madktari si jambo zuri maana umuhimu wao kila mtu anaujuwa,ila ni wa muhimu kwa kuwa unatufikirisha ili kuyaona yale ya msingi ya namna ambavyo tunapaswa kuendesha maisha yetu kama Watanzania. Na kama tukifanya yale ya msingi na hasa kufanya matumizi mazuri ya rasilimali fedha,watu na zile tulizopewa na Mungu hakika serikali inaweza kuwalipa madaktari na maisha ya wananchi yanaweza kubadilika kuwa bora sana
 
Mawazo mazuri kwelikweli, lakini bado yanaangalia CCM kwa macho ya matumaini. Matumaini kuwa CCM inaweza kukata tawi iliyokalia bila yenyewe kuanguoa.
 
Back
Top Bottom