Ukweli kuhusu MBATIA (NCCR) na Mzigo wa tuhuma anazobebeshwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli kuhusu MBATIA (NCCR) na Mzigo wa tuhuma anazobebeshwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MYAKINIFU, Dec 4, 2011.

 1. M

  MYAKINIFU New Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF,

  Ni imani yangu kuwa wengi mko katika hali nzuri kiafya, kama ni hivyo Inshalah! Kimsingi inasikitisha kuona baadhi ya watu wakishiriki mjadala kupitia tovuti yetu bila kufanya tafiti za kina juu ya mambo mbalimbali kama alivyowahi kutuasa na kutushauri X-Rais wa CHINA, hayati MAO TSETUNG kuwa NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK, Kwa tafsiri rahisi ni kuwa iwapo mtu hujafanya utafifit usizungumzie jambo lolote,inatubidi tuzungumze baada ya kufanya tafiti na tukiwa na data sahihi na za kutosha ndiyo tuweke hadharani ili kuiepusha jamii isipotoke kama baadhi ya wahuni wachache wanavyopotosha ukweli juu mgogoro wa uongozi ndani NCCR- MAGEUZI. Kwa mfano Imekuwa ikiripotiwa kuwa viongozi wa NCCR wa majimbo mbalimbali ya uchaguzi hapa nchini wamekuwa wakikutana mikoani na kutoa matamko kuwa bwana Mbatia ang'oke kabla ya muda wake kumalizika huku wakitoa sababu za KIPUUZI yaani zisizokuwa na uthibitisho.

  Kwanza jinsi mchakato wenyewe ulivyo una kasoro nyingi kwa hoja zifuatazo;

  Kwanza wanaoendesha mchakato huo wa kumng'oa MBATIA (akina KAFULILA nk), wanapotosha watu kuwa vikao vimefanyika na wajumbe kadhaa wameunga mkono kuwa Bwana MBATIA ang'oke jambo ambalo ukilifuatilia utakuta siyo kweli kwa sababu mchakato na vikao vyao haviwaiti viongozi wa Majimbo yote mikoani isipokuwa huwakusanya viongozi wachache sana wanaokubaliana na ajenda yao na wengine wasiokuwa viongozi na wakati mwingine hata watu wa kawaida wasiokuwa na nafasi yoyote ndani ya NCCR MAGEUZI kisha wakifika kwenye kumbi za mikutano huwapatia washiriki karatasi ya mahudhurio na kuwataka waorodheshe majina yao na kutia sahihi na baadaye huwasilisha HOJA YA KUMNG'OA NDG. Mbatia, kisha mjadala huanza.

  Katika mjadala imedhihirika kuwa wengi hupinga ajenda hiyo na kuwataka waanzilishi wa ajenda hiyowaondoke na ajenda yao ya kipuuzi. Baada ya hali hiyo kutokea hutafuta waandishi wa habari na kuwapatia orodha watu wote walioshiriki kikao na kuorodhesha majina yao, kisha huwapotosha waandishi wa habari kuwa Viongozi wa majimbo mkoa fulani wamekutana na kuazimia kuwa MBATIA ang'oke jambo ambalo siyo kweli kwa sababu katika vikao vyao hivyo wamekuwa wanakutana na upinzani mkali na wakati mwingine hata kunusurika kupata kichapo. Hivi sasa baadhi ya viongozi waliwahi kushiriki kwenye vikao hivyo wamelaani tabia ya KAFULILA na wenzake wachache sanaaaaaa ya kutoa taarifa za uongo kuwa wanaunga mkono hoja ya kipuuzi ya kumng'oa Bw. MBATIA huku ikiwa siyo kweli kutokana na ukweli kuwa ushahidi wa orodha ya majina wanayowasilisha kwa wanahabari ni ya mahudhurio tu na siyo ya watu au viongozi wanaounga mkono hoja ya kipuuzi ya kumng'oa MBATIA.

  Kwa mfano hali hiyo ilijitokeza jana tarehe 03/11/2011 mkoani dodoma ambapo Kamishna wa NCCR MAGEUZI mbaye ni MFUASI wa kafulila aliita kikao cha kujadili ajenda yao huku akiwa amewaalika hata watu wasiokuwa viongozi ktk chamacha NCCR mageuzi ili wakubaliane na hoja ya kumng'oa Mbatia hali ikawa tofauti na alivyotarajiwa, alipingwa vikali na kikao kuvunjika yaani hakikuisha kabisa na wakapoiteana ukumbini baadaye mwandishi wa kuandika kuwa DODOMA wameunga mkono kuwa mbatia ajiuzuru uenyekiti huku hali ikiwa ni tofauti na wanavyodai.

  Kwa ushahidi na rejea ya yaliyojiri DODOMA wasiliana na Ndg. CHIDUO ambaye ni mwenyekiti wa NCCR mageuzi Dodoma mjini kwa namba 0752192083 ambaye anaweza kueleza yote kuhusu kutimuliwa kwa Kamishna wa NCCR mkoa wa Dodoma. Hali kama hiyo inafanan sana na yale yaliyoripotiwa kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini, kwa mfano Piga simu kwa Uongozi wa NCCR Kasulu 0753121242(m/kiti wa wilaya), kibondo 07525452259, 0785174480. Utakubaliana nami kuwa yanayoendelea ni mkakati wa kutaka kudhoofisha NCCR-MAGEUZI nchini.

  -Ndugu zangu, mbali na mchakato wa akina Kafulila kuwa mbovu bado hoja zao ni za kipuuzi sababu zifuatazo, tafadhari soma kwa umakini na utakubaliana nami;
  1. Wanataka MBATIA ajiudhuru uenyekiti kwa sababu aliwahi kushindwa ubunge mara mbili yaani 2000 na 2010; Hoja hii ni dahaifu kwa sababu ktk mambo ya demokrasia hususani ktk uchaguzi kuna kushindwa kwa sababu mbalimbali na kushindwa kwa upande mwingine,hii ni kutokana na ukweli kuwa mwisho wa siku ni lazima apatikane mshindi mmoja, hivyo Mbatia kushindwa katika uchaguzi wa ubunge siyo kosa kwa mujibu wa katiba ya nchi na hata ya chama cha NCCR - Mageuzi. Hata hivyo Kafulila amabye ndiye mwanzilishi wa vurugu hizi ndani ya chama pamoja wa wafuasi wake wote wanaonesha udhaufu mkubwa kwa kuwa BIASED kwa sababu wanamtaka mbatia ajiudhuru uenyekiti kwa sababu ya kushindwa Ubunge huku wakiwaacha viongozi wengine ambao waligombea ubunge majimbo mbalimbali hapa nchini kwa mfano;

  Katibu mkuu taifa- Ndg, SAM RUHUZA, Makamu m/kiti Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu TZ Bara,mweka hazina wa NCCR taifa, Makamishna wa mikoa mbalimbali nchini akiwemo wa DODOMA aliyetimuliwa jana jumamosi tarehe 03/12/2011 nk. Ndugu zangu tujiulize hivi hii ni hoja ya kumfanya kiongozi ajiudhuru huku wakijua kuwa ndiye aliyekiwezesha chama leo kupata wabunge wanne (4) na Madiwani zaidi ya 40? Kubwa ni kwamba kwa mujibu wa katiba ya NCCR Magezuzi hakuna kifunge kinachodai kuwa mtu akigombea na kushindwa uchaguzi afukuzwe, lasivyo hata mzee Hashimu Rungwe aliyegombea URAIS mwaka jana angeambiwa jiudhuru uongozi wake ndani ya NCCR MAGEUZI,lakini kwa kuwa ni mtu wao na anautaka uenyekiti kama Kafulila japo anapretend kukanusha hivi sasa wameshindwa kumweleza ajiudhuru ili kuongeza idadi ya viongozi na wajumbe wa Halmashauri kuu taifa ya wapenda migogoro.. TUTAFAKARI PAMOJA na kukubaliana kuwa jamaa zetu wanautaka uenyekiti tu na sio jingine.

  2. Sababu nyingine ya kumng'oa Mbatia ni kuwa eti ameshindwa kukiletea chama MENDELEO,yaani hakiendelezi chama; Ndugu zangu ninyi na mimi ni mashahidi kuwa kwa zaidi ya miaka tisa (9) NCCR-Mageuzi hakikuwa na mbunge hata mmoja, lakini chini ya ndg. MBATIA NCCR kimeweza kupata WABUNGE Wanne(4) akiwemo Mh. Kafulila(mb),Je,hayo siyo maendeleo kwa chama? Vilevile kwa kipindi cha 2005 - 2010 NCCR-Mageuzi Kilikuwa na MADIWANI 19 na sasa wameongezeka hadi kufikia 40 NCHINI. Je, haya siyo maendeleo na mafanikio kwa NCCR- Mageuzi?

  3. Ruzuku ya chama imeongezeka kutoka shilingi 1,200,000 hadi kufikia shilingi takribani 12 milioni chini ya uongozi wa MBATIA. Je,haya yote kafulila na wenzake hawajui? Watafakari na kuweka wazi tu kuwa wana bifu na chuki binafsi na Ndg. Mbatia. Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu.Aidha Baadhi yao wamekuwa wakipotosha kuwa NCCR Kinapata RUZUKU ya sh. 130 milioni kwa mwezi mara wengine milioni 83,wengine 17 milioni na kuwa zotye hizo anakula Ndg. Mbatia, huu ni upotoshaji wa wazi na uaharibifu wa jamii ya Watanzania kwa sababu, unapodanganya umma unaifanya jamii iishi katika mambo ya kutokujua ukweli na matokeo yake ni kusababisha mifarakano isiyokuwa na tija na hatimaye kusababisha jamii kupotoka. JE,mtu anayepotosha wenzake kwa maslahi binafsi ni mtu mzuri kweli kwa jamii ya watu waliostaarabika? Kwangu mimi ni upuuzi mtupu na ilipaswa kuwatenga kabisa.Wewe unasemaje?

  4. Aidha wanadai kuwa Mbatia ajiudhuru uenyekiti eti kwa sababu ni CCM "B" mara WAKALA wa CCM; Wana JF tunapaswa kuondoka katika ulimwengu wa kuishi kwa HISIA(feelings) bila ya kuwa na FACTS kama ninavyoona kuwa hawa ndugu zetu wanakuwa driven na hisia tu, ukiwauliza kuwa wathibitishe u ccm "b" wa mbatia au uwakara utawasikia wakisema kuwa hotuba zake hazina ukali au zinsfia serikali nk. Je, Tanzania tunahitaji wanasiasa wa kuzungumza uwongo au ukweli? Lakini Nakumbuka kuwa nilipata kusikia kuwa Mh. KAFULILA (mb) wa kigoma Kusini, alipata kutamka mkoani kigoma wakati wa ziara ya RAIS kikwete ya kuzindua barabara ya Jimbo la Mh. Zitto Kabwe(MB) samba na daraja la Mto MALAGARASI jimbo la Mh. Kafulila kuwa "Kwa KWELI HAKUNA RAIS KAMA KIKWETE ALIYWWAHI KUUJALI MKOA WA KIGOMA, AMETULETEA BARABARA ZA LAMI nk", JE, ni halali kumtuhumu au kumuita KAFULILA kuwa ni CCM "B" eti kwa sababu alimsfia JK tena mbele yake? Binafsi siwezi kumuita CCM "B" au Wakala wa CCM, kwa sababu siwezi kuthibitisha hilo,namfahamu kuwa mpinzania mwenzangu. Kwa mantiki hiyo inatupasa watu kufanya upembuzi yakinifu katika masuala mbalimbali kabla ya kukurupuka na kuropoka ili mambo ambayo hayana facts. Hata hivyo iwapo Ndugu Kafulila na wenzake wanaweza kuthibisha kuwa Mbatia ni kibaraka wa CCM kiyakinifu, nitakubaliana nao. Kwa sasa sikubaliani nao kwa sababu hawana ushahidi wa hilo, hii ni kwa sababu wanasema. Lakini pia Mwanaharakati mmoja wa nchini MAREKANI alipata kusema kuwa " HISTORY IS A PEOPLE'S MEMORY AND WITHOUT MEMORY MAN IS DEMOTTED TO THE LOWEST ANIMAL", Nashauri turejee kwenye Historia za watu wetu na kuwatendea haki, Wale tunaofuatilia Historia za watu kama MBATIA tutakumbuka kuwa alifukuzwa chuo kikuu Mlimani tarehe 10/02/1992 Siku ya Jumatatu kwa sababu ya kupigania haki za watoto wa wakulima kutochangia katika elimu ya chuo kikuu (COST SHARING), Vilevile walikuwa wanapigania juu ya kuwepo haki na uhuru wa wanavyuo wa vyuo vya ELIMU ya juu kushiriki katika siasa za vyama vingi (Yaani MULTIPARTY DEMOCRACY). Kwa sababu ya msimamo mkali alio nao alifukuzwa chuo kikuuu pamoja na wenzake akiwemo Marehemu Dr. HAROON KIMARO ambaye alikuwa chuo kikuu sehemu ya MUHIMBILI wakati huo (Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amina). Leo kumita Mbatia CCM "B" ni maajabu kwa kuwa hafanani na hivyo amabavyo baadhi wameamua kumuita, na inawezekana kwa mtu yeyote akaundiwa zengwe au kuapachikwa jina lolote lile la kudhalilishwa bila ushahidi wa madai hayo ilimradi mtu au kundi la watu lina ajenda yake ya siri kama inavyotokea hivi sasa kwa ndg. Mbatia. Ukweli anasurubiwa kama yesu bila ya kuwa na hatia. Binafsi siwezi kumuita Kafulila na wenzake kuwa CCM "B" japokuwa najua amewahi kumsifia KIKWETE Kuwa RAIS mzuri sana kwa wana Kigoma. Tumwachie mungu, na nishauri tufanye tafiti za kina ili kuepuka upotoshaji wa jamii,

  Kwa haya machache wale waungwana wanaweza kusahihisha mitazamo yao juu ya Mbatia, na ieleweke kuwa huyu ni mpinzania wa ukweli na wakati mwingine anaweza kuteleza kama ambavyo mtu yeyote anaweza kuteleza na kujikuta amekosea katika kutenda au kutamka. Suruhisho siyo kumfukuza katika taasisi bila kumuita na kukaa chini kwa ajili ya mazungumzo yenye lengo la kuboresha. Kitendo cha kutaka Ndg. Mbatia aondoke ktk uenyekiti wake kabla ya muda tena kwa approach ya vurugu ni uhuni na kinapaswa kulaaniwa na mtu yeyoto anayependa mabadiliko ya kweli na SIYO COSMETIC CHANGE. Baba wa Taifa alipata kusema kuwa TUJISAHIHISHE kwa maslahi ya taifa letu, nami natoa wito wa wapenzi wa siasa za kweli nchini tujisahihishe kwa kukubali kuanza kusema ukweli na kutoa taarifa zilizotafitiwa ili kujenga jamii ya watu waliostaarabika na kuwapuuza watu wachache na upuu wao.

  Kwa hayo machache nawasilisha na kusubili changamoto na mawazo yenye lengo la kujenga taasisi yetu ya NCCR-Mageuzi.

  From:
  Machali Moses(mb)
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Kama Machali ndiye kaandika hii, basi huko ndani mambo hayajatulia.
   
 3. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mheshimiwa Mbunge Moses Machali, ahsante sana kwa kusema ukweli! Badala ya Mweneyekiti halali aliyechaguliwa kikatiba kutoka, mara mia wakaondoka wao kwenye chama.
   
 4. Wizzo

  Wizzo JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  mtajua wenyewe,pganeni mkichoka vuaneni magamba sisi cdm aaaaah bata 2 tunajiandaa kumtoa m2 madarakani 2012
   
 5. engineerm

  engineerm Senior Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona hajajibu hoja ya kwanini Mbatia amemshitaki mpinzani mwenzake(Halima mdee) kama sio ccm-B?
   
 6. ase

  ase Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mbona aliwawekea pingamizi wabunge wa cuf kule zanzibar kama sio ccm b.?
   
 7. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,968
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Kama hamuwezi kuonyesha demokrasia kwa vitendo ndani ya chanu, mnategemea kweli sisi tuje tuwaamini na kuwakabidhi nchi yetu kutuongoza?
  Hivi vyama vinapaswa kujifunza kulea na kukuza demokrasia ya ndani ya vyama vyenyewe. Kama mna utaratibu wenu wa kuchaguana, kwa nini msiufuate huo kwa muda mliojipangia wenyewe?
  Mnataka kuua chama chenu ili mmnufaishe nani?
   
 8. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,135
  Likes Received: 2,166
  Trophy Points: 280
  Hivi Mbatia bado ni David Cameron?
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Mods sioni logic hii thread kutokuwekwa kwenye jukwaa mama la JF(Siasa) ili wadau wengi zaidi watoe maoni yao.haya ni matatizo ya kisiasa kwa chama cha upinzani kikongwe kabisa.tuijadili kwa kutenda haki pande zote wakuu.
   
 10. josefast

  josefast JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Sasa huyo Kafulila si alikuwa CDM akanyea kambi kwenda NCCR hao akina Mbatia sindowaliompokea, leo anataka kuwatoa.
  Na wewe Machali jana live TBC uliahidi wakifanikiwa kumpiga chini Mbatia na Kafulila kuwa mwenyekiti utajiuzulu huo ubunge ulionao na kuwa raia wa kawaida, hivi utaweza kuacha posho hizo zilizo ongezeka huko bungeni.
  Kazi ni kwako siunajua ahadi ni deni.
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  siasa uchwara bana
  kuna nini kipya kutoka kwa mbatia ,lipumba au sharif hamad
  kama sio maslahi yao binafsi!?
   
Loading...