Ukweli kuhusu mazingira ya Shule ya msingi Litingi, jimbo la Mtama

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Picha ya Darasa chakavu lililojengwa kwa udongo na miti linalosambazwa mtandaoni na baadhi ya wanaharakati wa kidai kuwa darasa hilo ni la Shule ya msingi Litingi, kijiji cha Litingi, kata ya Nyangao, jimbo la Mtama, darasa hilo siyo halisi kwa mazingira ya sasa katika eneo hilo. Picha hizo ni ya zamani yaani ni mwaka 2015.

Ukweli ni kwamba Serikali ilishakuchukua hatua madhubuti ya Kujenga madarasa mengine Mapya Manne,matundu ya Choo,Ofisi za walimu na Matanki ya kuvunia maji.

Darasa hilo chakavu lilibomolewa tangu mwaka 2017.

Muonekano wa Shule hiyo Kwa Sasa ni kama inavyoonekana hapa. Tazama picha.

Serikali ipo kazini kuhakikisha inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu ili kuwapatia wanafunzi elimu bora.

1651133007702.png

IMG-20220427-WA0004.jpg
IMG-20220427-WA0005.jpg
IMG-20220427-WA0006.jpg

IMG-20220427-WA0006.jpg


IMG-20220427-WA0004.jpg
 
Itakuwa vizuri kama kuna watoto wanasoma hiyo shule si kwenda madrasat kukariri vitu visivyo na tija maishani mwao. Tunataka watoto wetu wasome waelimike.
 
Kwa nini isimiliki ilhali wewe huzalishi chochote na unakwepa kulipa Kodi!?
Madini ya serikali, milima ya serikali, hifadhi za serikali, mito ya serikali, bahari ya serikali, n.k, n.k lakini bado unaona fahari serikali kuwa na shule za misaada ya COVID-19!!
Nyie akili zenu zimebemendwa sio siri
 
Madini ya serikali, milima ya serikali, hifadhi za serikali, mito ya serikali, bahari ya serikali, n.k, n.k lakini bado unaona fahari serikali kuwa na shule za misaada ya COVID-19!!
Nyie akili zenu zimebemendwa sio siri
Akili yako ndiyo imebemendwa!!!..unadhani Kuna mkuu wa Kaya anaependa kutembeza bakuli!!!..Sasa sema wewe hizo rasilimali ulizozitaja ungepata wapi pesa ya kuzifanya zizalishe!?..na hiyo pesa inayohitajika kuzalisha ni kiasi gani!?
 
Back
Top Bottom