Mkaa Mweupe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 654
- 183
Katika pekua pekua nimekutana na hili ni bora niwashirikishe
Gonga hiyo link hapo chini:
Gonga hiyo link hapo chini:
Last edited by a moderator:
..tatizo la Zenj linatokana na Sultani wa Kiarabu aliyetawala hapo kujihusisha na biashara ya utumwa.
..upumbavu mwingine waliofanya kuacha makazi yao Uarabuni na kuhamia moja kwa moja hapo Zanzibar.
..Waingereza na Wafaransa hawakuhamia moja kwa moja kwenye makoloni na kuzikana nchi zao za asili. hiyo iliwawezesha kujiondoa na kurudi makwao, na kuepusha shari na mauaji pale wenye nchi yao walipoanza kudai uhuru.
..Waarabu na mzao wao wamewakandamiza Waafrika hapo Zenj miaka na miaka na sijui walikuwa wanategemea mwisho wake utakuwa kitu gani.
..binafsi nasikitishwa na kilichotokea wakati wa Mapinduzi, lakini kwa upande mwingine sishangazwi.
Tumaini,
..acha kujidanganya.
..wa-Tanganyika wasingeweza kuingia Zenj na kumfanyia kitu mbaya Sultani bila kushirikishwa na wa-Zenj wenyewe.
..tatizo lenu mnadinganya kufikiria kwamba utawala wa Sultani ulikuwa mzuri sana na kila m-Zenj alipendezwa nao.
..huko Zenj kila uchaguzi uliofanyika ulikuwa na matatizo na malalamiko yasiyokwisha. Mapinduzi ya 1964 siyo vurugu za kwanza za uchaguzi Zenj.
..Waafrika wa Zenj hawakupendezwa na katiba na sheria za uchaguzi zilizolazimishwa na Waingereza ambazo dhahiri zilikuwa zinawapendelea Waarabu.
..ZNP na ZPPP walifanya makosa, kwa kuongozwa na ubaguzi, kwa kuungana kuunda serikali huku wakiwaacha kwenye mataa ASP[Waafrika] ambao walikuwa wamepata kura nyingi na viti vingi.
..naamini ZNP wangekubali kuungana na ASP na Waziri Mkuu atoke ASP shari yote hii isingetokea. badala yake hila na ubaguzi vikawashawishi ZNP kwenda kuungana na ZPPP ilimradi Muafrika asipate kuongoza nchi yake mwenyewe.
NB:
..kama wa-Tanganyika walishiriki Mapinduzi hayo ni kutokana na kukerwa na jinsi ndugu zao walivyokuwa wakidhulumiwa haki zao ndani ya nchi yao.
Kwa mambo kama haya kuna watakatifu makaburi yao tutayafufua kuwauliza waliungana kwasababu gani? I mean karume na Nyerere
Tumaini,
..hao Waarabu hawana tofauti yoyote ile na Okello. they all could trace their way back to their countries of origin.
..kama Mapinduzi hayo yangekuwa hayaungwi mkono na wa-Zenj, haswa wale wanajinasaba na Waafrika, basi yasingedumu hata kidogo.
Tumaini,
..wanajeshi wa Kiarabu walikwenda wapi wakati wa Mapinduzi?
..inawezekana vipi kikundi kidogo cha wahuni kikamuondosha Sultani aliyekuwa akipendwa na wananchi wake kwa urahisi kiasi kile?
NB:
..how popular was the Sultan and his regime among the Zanzibari of African origin?
Sidhani kama kulikuwa na mapigano kati ya majeshi ya sultani na ya mapinduzi, lakini ajabu ni kwamba watu wa kabila moja (waarabu) wanalundikwa na kuua kwa pamoja.
Kulikuwa na haja gani ya kuua watu waliokwisha surrender kama siyo kutaka kufuta jamii hiyo (ethinic cleansing)
Kuna maandishi mengine yanasema waliuuwa wengi wao ni masheik wenye elimu kubwa ya dini ya kiislamu ili kisiwa hicho chenye sifa kemkem kuhus uislamu kibaki tupu..kisiwe na wanazuuoni ..hapo ndipo tunapo connect dots vipi mtakatifu nyerere alivyo husika kwasababu za kidini (chuki zake kwa uislamu)
Anayetaka kuyajua haya akasome historia ya Sheikh Hassan Bin Ameir atayaona kwanini walionekana hawa masheikh walikuwa na nguvu ya ushawishi zanzibar kwasababu jamii iliwakubali kama viongozi (nikifika hapa hutamani hata kulia kwani it is a disgrace kwakweli!!!)
Pateni reference hiyo msome zaidi;
http://victorian.fortunecity.com/portfolio/543/nyerere_and_islam.htm