Ukweli kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar - 1964

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
654
183
Katika pekua pekua nimekutana na hili ni bora niwashirikishe

Gonga hiyo link hapo chini:

Last edited by a moderator:
Yametupa mafundisho, sisi ndio tunajua kiatu kinapobana na jinsi ya kuitatua matatizo tuliyonayo, na juhudi hizi ndio zimeanza
 
Nadhani akina kubwajinga, fundi mchundo na mwanakijiji waangalie ukweli unakuja tu hakuna jengine uongo hufika mahali ukapotea baada ya ukweli kujulikana huyu muitaliano ni kweli alikuwapo wakati wa mapinduzi na katika vitabu vingi walikuwa wanasema haya SMZ ikikanusha haya tizameni muone faida za muungano hizo!!!
 
Kwa mambo kama haya kuna watakatifu makaburi yao tutayafufua kuwauliza waliungana kwasababu gani? I mean karume na Nyerere
 
..tatizo la Zenj linatokana na Sultani wa Kiarabu aliyetawala hapo kujihusisha na biashara ya utumwa.

..upumbavu mwingine waliofanya kuacha makazi yao Uarabuni na kuhamia moja kwa moja hapo Zanzibar.

..Waingereza na Wafaransa hawakuhamia moja kwa moja kwenye makoloni na kuzikana nchi zao za asili. hiyo iliwawezesha kujiondoa na kurudi makwao, na kuepusha shari na mauaji pale wenye nchi yao walipoanza kudai uhuru.

..Waarabu na mzao wao wamewakandamiza Waafrika hapo Zenj miaka na miaka na sijui walikuwa wanategemea mwisho wake utakuwa kitu gani.

..binafsi nasikitishwa na kilichotokea wakati wa Mapinduzi, lakini kwa upande mwingine sishangazwi.
 
Tatizo ni kwamba wauaji si wazanzibar bali watanganyika wakiongozwa na okello?? that is the point
 
Tumaini,

..acha kujidanganya.

..wa-Tanganyika wasingeweza kuingia Zenj na kumfanyia kitu mbaya Sultani bila kushirikishwa na wa-Zenj wenyewe.

..tatizo lenu mnadinganya kufikiria kwamba utawala wa Sultani ulikuwa mzuri sana na kila m-Zenj alipendezwa nao.

..huko Zenj kila uchaguzi uliofanyika ulikuwa na matatizo na malalamiko yasiyokwisha. Mapinduzi ya 1964 siyo vurugu za kwanza za uchaguzi Zenj.

..Waafrika wa Zenj hawakupendezwa na katiba na sheria za uchaguzi zilizolazimishwa na Waingereza ambazo dhahiri zilikuwa zinawapendelea Waarabu.

..ZNP na ZPPP walifanya makosa, kwa kuongozwa na ubaguzi, kwa kuungana kuunda serikali huku wakiwaacha kwenye mataa ASP[Waafrika] ambao walikuwa wamepata kura nyingi na viti vingi.

..naamini ZNP wangekubali kuungana na ASP na Waziri Mkuu atoke ASP shari yote hii isingetokea. badala yake hila na ubaguzi vikawashawishi ZNP kwenda kuungana na ZPPP ilimradi Muafrika asipate kuongoza nchi yake mwenyewe.

NB:

..kama wa-Tanganyika walishiriki Mapinduzi hayo ni kutokana na kukerwa na jinsi ndugu zao walivyokuwa wakidhulumiwa haki zao ndani ya nchi yao.
 
Sio kujidanganya, kama ni kujidanganya unajidanganya wewe kufikiri kwamba watu wengi wa zenj walifanya haya mapinduzi ya kuua wazanzibar wenzao NO!

Ukiangalia hii vidoe vizuri utaona watanganyika wakishirikiana na Okello na kikundi chake waliuua watu wa kabila moja (waarabu)..motives zao hazijawekwa sawa mpaka leo?

Ndio maana reading books of history, naamini haya mapinduzi yalifanywa na karume na nyerere bila matakwa ya wananchi...na ndio maana mpaka leo hawataki kufanya referendum kuhusu muungano..kama mtanganyika nisiyependa kutawala watu wengine au nchi yangu kuwa sehemu ya huo ubabe wafanye referendum tukubaliane mambo ya muungano kwa haki..si ubabe
 
Tumaini,

..hao Waarabu hawana tofauti yoyote ile na Okello. they all could trace their way back to their countries of origin.

..kama Mapinduzi hayo yangekuwa hayaungwi mkono na wa-Zenj, haswa wale wanajinasaba na Waafrika, basi yasingedumu hata kidogo.
 
Ha ha! waarabu waliouwa kwenye hii video hawakuwa wanajeshi, hakuna sehemu inayoonyesha mapambano ni raia tena prisoners wangeshikwa wakapelekwa kambini au kurudishwa kwao hakuna tatizo lakini kuwaua kwasababu ni waarabu ni " totally against humanity and intermational laws of wars"

Malengo yake ni kumaliza kabila la waarabu huko zanzibar what a shame?

Mapinduzi yamedumu au yamedumishwa? kwa nguvu za mtanganyika acha rongorongo

Tupige referendum tuone kama muungano utapata fursa hata huku bara kama hatujafanya ovehaul of its structure..

siwezi kuwa sehemu ya jamii inayodhuluma watu haki kwa misingi ya race shame.
 
Tumaini,

..wanajeshi wa Kiarabu walikwenda wapi wakati wa Mapinduzi?

..inawezekana vipi kikundi kidogo cha wahuni kikamuondosha Sultani aliyekuwa akipendwa na wananchi wake kwa urahisi kiasi kile?

NB:

..how popular was the Sultan and his regime among the Zanzibari of African origin?
 
Sidhani kama kulikuwa na mapigano kati ya majeshi ya sultani na ya mapinduzi, lakini ajabu ni kwamba watu wa kabila moja (waarabu) wanalundikwa na kuua kwa pamoja.

Kulikuwa na haja gani ya kuua watu waliokwisha surrender kama siyo kutaka kufuta jamii hiyo (ethinic cleansing)

Kuna maandishi mengine yanasema waliuuwa wengi wao ni masheik wenye elimu kubwa ya dini ya kiislamu ili kisiwa hicho chenye sifa kemkem kuhus uislamu kibaki tupu..kisiwe na wanazuuoni ..hapo ndipo tunapo connect dots vipi mtakatifu nyerere alivyo husika kwasababu za kidini (chuki zake kwa uislamu)
 
Anayetaka kuyajua haya akasome historia ya Sheikh Hassan Bin Ameir atayaona kwanini walionekana hawa masheikh walikuwa na nguvu ya ushawishi zanzibar kwasababu jamii iliwakubali kama viongozi (nikifika hapa hutamani hata kulia kwani it is a disgrace kwakweli!!!)

Pateni reference hiyo msome zaidi;

http://victorian.fortunecity.com/portfolio/543/nyerere_and_islam.htm
 
Tumaini,

..je walikuwa wanauawa Masheikh indiscriminately, au walikuwa wanachaguliwa Masheikh wa Kiarabu tu?

..je, Zenj kulikuwa na Masheikh wowote wale wa Kiafrika?

NB:

..kama Mapinduzi yaliongozwa na Nyerere na wa-Tanganyika, kwanini Sultani alikimbilia Dar baada ya kukataliwa kuingia Kenya?

..kwanini huyu Sultani hajirudii tu kwao Oman. vitabu vyote vya historia vinasema huko ndiko ukoo wao ulikotokea.
 
..je walikuwa wanauawa Masheikh indiscriminately, au walikuwa wanachaguliwa Masheikh wa Kiarabu tu?
JIBU Waliua wengi waarabu lakini pia waafrika kwakuwa vita hii ilikuwa na mkono wa kidini nia ilikuwa ni kuondoa wanazuoni wengi as possible!

..je, Zenj kulikuwa na Masheikh wowote wale wa Kiafrika?

JUBU: Walikuwepo wengi na waliuawa wengi pia

..kama Mapinduzi yaliongozwa na Nyerere na wa-Tanganyika, kwanini Sultani alikimbilia Dar baada ya kukataliwa kuingia Kenya?

JIBU: Maandishi mengi yaliyoonyeshwa alitekwa na jeshi la Tanganyika" kwa hiyo kurudishwa Tanganyika ni maombi ya nyerere kwa serikali ya kenya
 
Anayetaka kuyajua haya akasome historia ya Sheikh Hassan Bin Ameir atayaona kwanini walionekana hawa masheikh walikuwa na nguvu ya ushawishi zanzibar kwasababu jamii iliwakubali kama viongozi (nikifika hapa hutamani hata kulia kwani it is a disgrace kwakweli!!!)

Pateni reference hiyo msome zaidi;

http://victorian.fortunecity.com/portfolio/543/nyerere_and_islam.htm

Mzee
Hii link yako inasema CCM siyo Chama Cha Mapinduzi bali ni ''Christian Church Movement'':

Quote :''This is a clear testimony that the union of Zanzibar and Tanganyika was the creation of Karume, a racist dictator nominal Muslim from Nyasaland (Malawi) and Nyerere, an autocratic devout Christian from Tanganyika. And consequently, Zanzibar has lost her strong Islamicity and sovereignty to Tanganyika since April 26, 1964 when the dictator Karume, signed the Articles of the Union, drafted by British expatriates, Attorney General Roland Brown and Chief Parliamentary Draftsman, P.R.N. Fifoot, to form Tanzania under the clique of the Christian Church Movement (CCM) of Tanganyika''.

Hivi wakereketwa wa CCM mnaikubali hii ? au ni Freemasons na Da Vinci Code?
 
Back
Top Bottom