Ukweli kuhusu Mafao ya PSSSF sheria mpya ya kustaafu

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Ni upi ukweli kuhusu sheria mpya ya mafao ya pensheni? Wengi hawaelewi haswa kinachojiri, na wengine hupata taarifa zinazozua taharuki miongoni mwa walio karibu kustaafu, hasa zile zinazowaambia watapata robo tu ya kile ambacho wenzao walipata kabla ya kutumika sheria mpya.

NARUKA!: Haya ni maoni binafsi, na mimi si mwanasheria msomi. Aidha, nilishiriki kutoa maoni kwenye Kamati ya Bunge iliyokuwa ikisikiliza maoni ya wadau kuhusu sheria ya PSSSF; nikiwemo kwenye timu iliyoundwa na THTU kuuchanganua muswada na kuwasilisha maoni.

Gazeti la Novemba 13 2018 la Nipashe limeipa uzito mkubwa habari ya pensheni. Nikinukuu:
Hivi ndivyo mafao yatakavyokuwa
Kwa mujibu wa kikokotoo cha zamani, malipo ya mkupuo kwa mtu mwenye mshahara wa aina hiyo, yangekuwa Sh. milioni 71.6, lakini kwa kikokotoo kipya atalipwa Sh. milioni 35.8, huku pensheni ya mwezi kwa zamani ikiwa Sh. 371,800 na ya sasa ni Sh. 557,800, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.

Tatizo kwenye nukuu hiyo neno "Zamani" halikufafanuliwa ipasavyo. Kwa mfano, tukichukulia Novemba 2014 kuwa ni "Zamani" basi maelezo hayo siyo sahihi (kwa wanachama wa GEPF, NSSF, PPF na kwa wanachama wa LAPF na PSPF wa baada ya Julai 2014).

Kikokotoo cha mafao ya pensheni kilirekebishwa Julai 2014, na ndicho kinachotumika hadi sasa, japo jina la kanuni limebadilishwa.

Pension_Formula_2014.png

Kikotoo cha pensheni cha mwaka 2014 (hapo juu) kilinganishe na kile cha mwaka 2018 (hapa chini)
Pension_Formula_2018.png
Kikokotoo cha pensheni cha mwaka 2018.

Hakuna tofauti.

Watu wanazungumzia 25% distribution factor kana kwamba ni kitu kipya. Kipo toka 2014. Kama unamfahamu mtu yeyote mliyekuwa naye mfuko mmoja, na mlijiunga takriban wakati mmoja, mafao yenu yatafanana tu ikiwa uchangiaji ulifanana.

Kwa wepesi, pensheni ziko hivi:

A. Unachangia michango ya kila mwezi, ukiungwa mkono na mwajiri.
B. Ukifikia umri wa kustaafu, na umechangia vya kutosha, unasitisha kuchangia.
C. Mfuko wa Pensheni unadumbukiza kwenye kikokotoo taarifa mbalimbali na kupata linamba fulani likubwa kuliko jumla ya michango uliyochanga.
D. Hiyo jumla kubwa inagawanywa mafungu mawili:
(1) Mafao ya Mkupuo ("Kiinua Mgongo") -- Haya ndiyo wengi huyangojea kwa hamu :) ambacho toka mwaka 2014 ni robo ya lile lijumula kubwa lao la (C) hapo juu. Ukisikia, "jamaa kastaafu, kavuta 89m" ni hicho kiinua mgongo. Watu hawanaga stori na kile anacholipwa kila mwezi.
(2) Pensheni ya kila mwezi inayotolewa kwa mstaafu mpaka pale atakapofariki. Hii hukokotolewa toka kwenye albaki ya lijumla kubwa baada ya kutoa kiinua mgongo [(Jumla kubwa - Kiinua Mgongo) ÷ 150].

Shida kubwa ni pale watu wanaposema (au ku-insinuate) kwamba:

(a). Watapata robo tu ya Kiinua Mgongo ambacho wenzao walikuwa wanapata, jambo ambalo si kweli.
(b) Kikokotoo hiki ni tofauti na kilichokuwa kikitumika miaka michache tu iliyopita, jambo ambalo pia si kweli.

Vyanzo vyenye kuonyesha kanuni hizo vimeambatishwa kwa rejea.

Ukiwa na swali, usisite kuuliza.

Maelezo haya yametolewa kama Public Service :D

EDIT 1: Kiambatisho cha faili la Excel linalokokotoa mafao. (Wajuzi tusaidieni kujua iwapo ina makosa).
Kikokotoo.xlsx.zip
Daunilodi na uanzip ulipate faili la Excel.

EDIT 2: Angalia nini kinatokea ukilinganisha mafao ya sasa na michango ya mwanachama.
Nataka Pesa Zangu Zote wakati wa kustaafu - JamiiForums

EDIT 3: Pana mabadiliko kwa waliokuwa wanachama wa PSPF na LAPF toka kabla ya Julai 2014. Kwao hao, mafao ya mkupuo yamepungua kwa nusu (toka 50% mpaka 25%), lakini mafao ya kila mwezi yameongezeka. Hakuna mabadiliko kwa wengine wote.

EDIT 4: Pongezi kwa Mheshimiwa Rais kwa maamuzi ya kuhusu kikokotoo. Maamuzi ya Mheshimiwa Rais ni kwamba kikokotoo kilichokuwa kinatumika punde kabla ya kuanza kwa sheria ya kuunganisha mifuko, ndicho kitumike kwa muda wa mpito mpaka 2023 kitakapopatikana kikokotoo kingine kitakachopatikana baada ya maoni ya wadau na tathmini (actuarial valuation.)
 

Attachments

  • Pension_Harmonization_rules_2014.pdf
    1.6 MB · Views: 58
  • Social_Security_Schemes_Benefits_Regulations_2018.pdf
    452.4 KB · Views: 53
  • Kikokotoo.xlsx.zip
    5.1 KB · Views: 36
Maelezo mahsusi kwa wa PSPF na LAPF wa kabla ya Julai 2014 yameongezwa kama Edit 3.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom