Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,197
- 128,127
Eneo la stend ndogo(Vifodi) lipo katika Mtaa wa Levolosi,Kata ya Levolosi Halmashauri ya Jiji la Arusha.Eneo hili lina jumla ya vibanda (Maduka) 394 yaliyojengwa kwa nyakati tofauti.Mwaka 1994 Halmashauri iliingia mkataba wa ujenzi(Build Operate Transfer) na wananchi kwa lengo la kuendeleza eneo hilo,mkataba huo ulimruhusu Mjenzi kujenga kwa gharama zake ambazo ziliidhinishwa na Mhandisi wa Halmashauri na yeye Mjenzi kufanya biashara kwa miaka kumi(10) bila kulipa ili ajifidie gharama za ujenzi.Hivyo kuanzia mwaka 1994 hadi 2004 Wajenzi walikaa BURE bila kulipa.Kuanzia mwaka 2005 walianza kulipa kodi ya Upangaji chini ya Mkataba wa Upangaji baada ya ule mkataba wa kwanza kuisha (hakukuwa na malalamiko ya wajenzi kuhusu mkataba mpya)
Kwenye mkataba wa Upangishaji Halmasahuri ya Manispaa ilijulikana kama MMILIKI NA MPANGISHAJI wakati Mjenzi alijulikana kama MPANGAJI.Moja masharti ya mkataba huu wa upangishaji ni kuwa Mpangaji hatoruhusiwa kumpangishia mtu mwingine kibanda bila idhini ya mmiliki ambaye ni halmashauri ya Manispaa.Pia ilikubaliwa kulipa kodi ya PANGO ya Tshs 10,000/=(elfu kumi tu) kwa mwezi .Kodi ya elfu kumi ililipwa hadi mwaka 2008 ilipopanda hadi 20,000na baadae mwaka 2009 ilipanda tena hadi 40,000 kisha kufika 60,000,mwaka 2012 kodi ilipandishwa hadi 125,000tshs kwa mwezi hadi sasa.Katika kipindi chote hiki hoja ya Umiliki haijawahi kuwepo kwa kuwa wajenzi wanaelewa fika kuwa sio wamiliki bali ni Wapangaji
Mwaka 2012 kulifanyika Special Audit katika Halmashauri ya Jiji,miongoni mwa mapendekezo ya CAG ilikuwa kuwa Halmashauri iweke bei ya soko ili kwenda sambamba na viwango vya IPSAS sambamba na kuanisha mali zake rasmi.Mwaka 2013 Halmashauri ilitangaza zabuni hata hivyo hiyo Zabuni haikufanyika licha ya wananchi kununua tender documents,hadi leo hakuna majibu
Kuanzia mwaka 2016 Halmashauri ilifanya uchambuzi wa maeneo hayo,na kugundua kuwa kwa zaidi ya miaka kumi hawa Wajenzi wamekuwa wakipangisha vyumba hivi kwa bei kati ya 350,000 hadi 700,000 kwa mwezi,kinyume cha masharti ya mkataba wao wa Upangaji.Wale wanaofanya biashara ndani wanalipa kwa Mjenzi na yeye mjenzi halipi hizo fedha Halmasahuri,wakati wa opresheni mfanyabiashara ambaye yupo ndani ndie anayeumia pale halmasahuri inapoamua kufunga duka ili kodi ilipwe.Kufuatia changamoto hiyo Halmashauri iliwaandikia wafanyabiashara waliopo ndani na kuwaelekeza kuwa walipe madeni yote na kwamba Halmasahuri ingewapa mikataba kwa kutumia vigezo vya leseni ya biashara,Tin,na kulipa kodi.Wafanyabiashara hawa walilipa kodi ya PANGO na mikataba ikaandaliwa kabla ya Mkurugenzi aliyepo sasa kukataa kusaini kwa shinikizo la aliyekuwa mkuu wa wilaya ambaye sasa ni mkuu wa mkoa
Mkuu wa Wilaya aliunda kamati ya uchunguzi ili kupendekeza njia mwafaka ya kumaliza changamoto hii,kamati ya uchunguzi ilipendekeza njia mwafaka ni ZABUNI.Na ili kufikia kutangazwa kwa ZABUNI iliamuliwa kwenye vikao rasmi kuwa waliojenga wafutwe kwenye mfumo wa malipo,pia wapewe NOTISI ya siku 30 kwa mujibu wa sheria.Notisi ilitolewa na Zabuni ikatangazwa kwa utarataibu wa ushindani wa Kitaifa.Zabuni ilifunguliwa mwishoni mwa January 2017.Siku moja kabla ya ufunguzi wa Zabuni Mkuu wa mkoa aliitisha kikao na anaoita Wajenzi na kuwahakikishia kuwa wao watarudishiwa maduka
Mkuu wa mkoa wa Arusha ameingilia mchakato wa zabuni ndio mahali penye mkwamo hadi sasa!wafanyabiashara wanaolipa kodi zote za serikali wamefungia maduka kwa amri ya mkuu wa mkoa,ambaye ameagiza polisi kutowapa ushirikiano wapangaji halali wa Halmashauri.Ni wazi kuwa kuna rushwa hapa
Msimamo wa baraza la madiwani ni kuwa Tenda ifike mwisho apate yeyote kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma ili Halmashauri ipate kodi stahiki pamoja na sheria kufuatwa.