Ukweli kuhusu kuwa na mwandiko mdogo na uchoyo

Wanawake wengi ndio wanamiandiko midogo,

Miandiko Kwa sehemu kubwa inachangiwa na mambo Yafuatayo;
1. Ushikaji wa Kalamu,
2. Size ya kiganja na vidole.
3. Kalamu
4. Umri uliojifunzia kuandika.
5. Akili
6. Msawazo wa macho.
Msawazo wa macho ni vile macho yaonavyo karatasi na muandiko wakati mtu anaandika.
Ndio maana kuna ambao hawezi kuandika wakati karatasi imenyooka, wanaipindisha karatasi upande au shingo zao.

Muandiko unaosomeka unaashiria akili iliyotulia ingawaje haimaanishi kiwango cha akili.
Muandiko mcharazo unaashiria akili ambayo haijatulia, yaani inayoenda Kasi na kufikiria Kwa upesi, Sana.

Muandiko unamahusiani na tabia,
Wenye muandiko midogo kitabia huwa Wabinafsi na endapo ubinafsi ukizidi hugeuka wachoyo.
Wanawake wengi huandika miandiko midogo na hii huelezea tabia zao za ubinafsi.

Hata wanaume wenye miandiko midogo huwa Wabinafsi.
Tofauti na watu wenye miandiko mikubwa ambao hawabanii mistari kwenye karatasi.

Niishie hapa.

Taikon wa Fasihi
Asante mkuu.. naandikia mkono wa kulia japokuwa am left handed.. huwa nalazia shingo na karatasi au daftari upande wa kushoto ..
Mwandiko wangu ni mcharazo kuelekea kulia na mdogo.

Asante nmejifunza kitu hapo .. mimi sio mchoyo ila nna kaubinafsi tu
 
Ohoo! Nionavyo watu wenye miandiko midogo wanakuwa na hulka ya upole kitabia,watu wataratibu kiujumla zile hulka za upole Kama mimi..😜

Swala la uchoyo nafikiri si lakiuandishi bali hulka au mazingira aliyokulia mtu, isipokuwa watu wa hulka ya upole huchukulia wachoyo maana hujikuta muda mwingi wana spend peke yao,so mambo yao yanakuwa yanaonekana Kama ya kibinafsi wengine hutafsiri Kama uchoyo.! Hawa watu wa aina hi mpk uzoeane nao ndo utawaelewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom