Ukweli kuhusu kustaafu Askofu Pengo, Ashauriwa akaishi Mtoni Kijichi katika uzee wake

Heri ya sikukuu ya PASAKA!

wakati hali ya sintofahamu ikiendelea juu ya nyaraka mbili zilizotolewa na viongozi wakuu Wa makanisa ya katoliki na KKKT kutofautiana na maoni ya askofu Pengo.
Hatimaye jibu la ukomo Wa askofu pengo lapatikana!
Kwa mujibu Wa maelezo ya katibu Wa jimbo kuu katoliki la dar es salaam! Katika hitimisho la ibada takatifu ya ALHAMISI KUU iliyoongozwa na kardinali pengo mwenyewe.
Katibu Wa jimbo alitangaza rasmi maandalizi ya kustaafu Muadhama Kardinali Pengo kwamba tayali yameshafanyika!
Kwa mujibu Wa kanuni za kanisa katoliki, askofu Hustaafu akifikisha miaka 80.
Na ilivyo Kwa askofu Pengo kwasababu alikwisha kuandika Wosia, Kwamba endapo ikitokea amefariki aliomba Azikwe Pugu eneo ambalo wakatoliki huenda hija, na endapo akistaafu pia alipendelea kwenda kuishi hukohuko Pugu. Maandalizi ya nyumba yake huko Pugu tayari yamekamilika.
Lakini kutokana na Ushauri Wa wasaidizi wake kumuomba abadilishe mawazo yake, walipendekeza Akistaafu asiende Pugu, Bali wamjengee Nyumba hapahapa dar es salaam maeneo ya Mtoni kijichi katika eneo la Parokia ya EPIFANIA! ushauri ambao askofu pengo kaukubali na utatekelezwa kuanzia sasa.
Pamoja na kwamba Kwa sasa askofu Pengo bado hajatimiza umri Wa kustaafu! Ambapo Kwa hivi sasa ana umri Wa miaka 74. Basi Kwa mujibu Wa sheria bado ana miaka 6 za kuliongoza kanisa kama baba askofu mkuu.
Lakini kutokana na ushauri unaoendelea kutoka Kwa wasaidizi wake, ama pengine Kwa uzee wake ama Kwa sababu za kiafya ama kwasababu yeyote! Huenda askofu Pengo akaamua kustaafu mda wowote kadri anavyo penda yeye.

Askofu pengo ambaye amekuwa gumzo ndani na nje ya kanisa katoliki kutokana na maoni yake kuwa kinyume na baraza la maaskofu, kitendo kinachodhooofisha baadhi ya imani za wakatoliki. INGEPENDEZA ASTAAFU
Kutokana na maandiko matakatifu,
KIONGOZI WA KANISA LAZIMA
Maneno yako yathibitishwe na matendo yako.

Mathayo 5:36-37 '' Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.''

Hivi sasa Askofu mkuu Wa jimbo katoliki la dar es salaam, akiwa kama askofu, pia ni baba mlezi Wa parokia ya St. Mouris KURASINI, wakati huohuo ndiye Baba paroko wa kanisa kuu la St. JOSEPH huku makamu wake akiwa ni askofu NZIGIRWA.

Kutokana na historia nzuri ya askofu pengo, pamoja na usomi mkubwa, andaendelea kutumika kama mshauri akiwa mapumzikoni kijichi baada ya kustaafu.
HUENDA SASA KANISA LINAHITAJI AKILI MPYA, KIONGOZI MPYA ATAYEGUSWA NA MAISHA YA WATU.
=======================
* MHOGO UKIKAA MDA MREFU BILA KUVUNWA HUGEUKA MZIZI*
View attachment 731243
Mkwanja usio halali huondoa mazuri ya nyuma, hajatubu mpaka sasa.
 
1. Sheria ya Kanisa Katoliki linawataka Maaskofu wa majimbo kuomba kustaafu wanapofikisha miaka 75.
Baba Mtakatifu akisha pokea maombi ya askofu husika ni jukumu lake kukubali maombi hayo. Anakubali lini? Inategemea na utashi wake, anaweza akakubali mara moja au akakaa tu na maombi hayo bila kutoa jibu la kukubali.

2. Maaskofu wa Majimbo, kama hawakupeleka maombi ya kustaafu wanapofikisha miaka 75 ya kuzaliwa, huondolewa na mamlaka husika wanapofikisha miaka 80.

3. Kutokana na matatizo ya afya au shida nyingine Maaskofu wa majimbo uweza kuwasilisha maombi ya kustaafu hata kabla ya miaka 75.

Itakumbukwa Mwadhama Rugambwa, Askofu Mkuu wa zamani wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam aliondoka madarakani akiwa na miaka 80 mwaka 1992. Kabla yake 1990 aliletwa Polycarp Pengo kama Askofu Mkuu Mwandamizi, maana yake Askofu Mkuu mwenye hadhi ya kurithi.

Askofu Msaidizi Nzigilwa hana hadhi ya moja kwa moja ya kumrithi Mwadhama Pengo. Kwa uzoefu, Kanisa litamtangaza mtu mwingine kuja kuwa Askofu Mkuu wa Dar es Salaam wkati Asksofu Nzigilwa akibaki na wadhifa wake huo huo wa Askofu Msaidizi - sio tafsiri sahihi ila ndio tunavyofahamu, ni Auxilliary Bishop. Ebu fananisha na Auxilliary Police kama unaweza kupata maana pana ya neno auxilliary!
Mkuu ina maana yeye yupo tu kama auxiliary verb is, be, are ambazo hazina maana mpaka ziwekwe na main verb milele?
 
Kwa mujibu Wa Canon law sheria namba arobaini Maaskofu wakuu na maaskofu wanatakiwa kwa mujibu wa sheria hiyo kuwasilisha kwa Papa barua ya kustaafu wanapotimiza miaka 75 na sio 80 kama ulivosema
Sahihisho la pili Polycarp kadinali Pengo sio paroko wa wa parokia ya mtakatifu Yosef ile parokia ina paroko wake askofu mkuu hawezi kuwa paroko
Kama ni kweli ana miaka 74 basi ana mwaka mmoja tu kuhudumu kama askofu mkuu
Ataendelea kuwa kardinali na akitimiza miaka 80 atapoteza haki ya kupiga kura ya kumchagua papa
 
Kwa mujibu Wa Canon law sheria namba arobaini Maaskofu wakuu na maaskofu wanatakiwa kwa mujibu wa sheria hiyo kuwasilisha kwa Papa barua ya kustaafu wanapotimiza miaka 75 na sio 80 kama ulivosema
Sahihisho la pili Polycarp kadinali Pengo sio paroko wa wa parokia ya mtakatifu Yosef ile parokia ina paroko wake askofu mkuu hawezi kuwa paroko
Kama ni kweli ana miaka 74 basi ana mwaka mmoja tu kuhudumu kama askofu mkuu
Ataendelea kuwa kardinali na akitimiza miaka 80 atapoteza haki ya kupiga kura ya kumchagua papa
Wewe ni mweupe sana kichwani kuhusu haya, sema unalazimisha kujua;
Sasa kama sheria inasema miaka 80 ni umri Wa kustaafu, ....unaposema wakifika miaka 75 maaskofu wanatakiwa kuandika barua ya kustaafu; sijaelewa unaposema wanatakiwa maana yake ni lazima, sasa hiyo miaka 80 yanini kama 75 unatakiwa kuandika barua?
SHERIA IPO HIVI
Mda Wa kustaafu askofu ni miaka 80, lakini endapo Kwa hiari yake akapenda kustaafu mapema basi, askofu husika huandika barua kuaomba hilo akiwa na umri kuanzia 75, na ombi hilo hukubaliwa au hukataliwà!
NOTE; Sheria hiyohiyo inasema askofu anaweza kuomba kustaafu mda wowote paspo kujali umri ikiwa kuna sababu nyingine zikiwemo ugonjwa, au makosa ya kuwajibika!
Kwahiyo hata akiwa na 70 askofu anaweza omba kustaafu
 
Kwani Pugu ni jimbo la Morogoro? Au iko nje ya Dar es salaam
Sina hakika na hii habari, ila Kwa ramani mpya inayokuja, pugu inaangukia jimbo la bagamoyo kumbuka bagamoyo ilikuwa ndani ya jimbo la morogoro

Hawa washuuri walikuwa wapi kumshuri kabla ya nyumba ya pugu kuanza, sasa wakianza kumjengea nyumba nyingine kijichi tutaanza kutoa michango tena, ikiisha ya kijichi watakuja wengine watamshauri aende akapumzike tegeta. NENDA PUGU BABA
 
Kiukweli tu Pengo ameshachoka Kimwili, Kiakili na Kiroho. Maaskofu, Mapadri na waumini nao wameshamchoka sana. Hana kitu kipya tena. Angepumzika mapema ingekuwa ni busara zaidi. Kwa sasa analichosha tu Kanisa Katoliki.
Magonjwa yanayomuandama sana yameharibu uwezo wake wa kufikiri....akapumzike tu hakuna namna.
 
Back
Top Bottom