Ukweli kuhusu hali ya uchumi nchini Tanzania

Super Don

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,978
1,779
Ipo dhana inayotembea vichwani mwa watanzania waliowengi kwamba hali ya maisha na hali ya nchi ilivyo sasa, imesababishwa na serikali ya Rais Magufuli ili ijenge nchi vizuri...

Hii imetumiwa hata na rais kufuatia kauli zake za kwamba anainyoosha nchi... Watu wameaminishwa kuwa serikali imeamua taifa lipitie humu ili kunyoosha nchi..

Huu ni uongo wa mchana, lakini ni uongo wa kisomi, ni uongo unaopangiliwa na ili uujue inabidi uwe muongo uliyeusomea kama hawa waongo magwiji wanaotudanganya ambao wengi wamesomea hasaa.... tena kwa kodi zetu wenyewe ii watudanganye...

Serikali takatifu ya Rais John Pombe Magufuli haihusiki na hali ngumu ya maisha inayowakumba Watanzania hivi sasa, bali nayo ipo kwenye hali ngumu kama tulivyo sisi, haielewe nini kilicholikumba taifa kwa hali hii... Ili iende sambamba na korasa ya kiutawala imeamua kununua ugumu wa maisha kuwa ni sera ya serikali hii katika kujenga taifa.

Ndio serikali zote duniani zinazokumbana na majanga ya aina hiyo hujichubua ngozi yake na kujifanya zenyewe zimezalisha janga hilo ili kufanya jambo kwa manufaa ya umma...

Hali ya mambo katika taifa ilianza bada ya ccm kuleta sheria ya mitandao kimkakati kwa ajili iwabebe katika uchaguzi, kisha tukanyimwa sehemu ya bajeti ya nchi kupitia wahisani wetu wa MCC kuelekea uchaguzi mkuu, ambao kimsingi walikuwa wakichangia zaidi ya 3trioni kwa mwaka, wakati tukishangaashaanga hilo, baada ya uchaguzi serikali ikabaka demokrasia kule Zanzibar kisha wahisani wetu katika bajeti wale wanaochangia zaidi 40% wakajitoa na kutwambia tukome kwenda kuomba kwao EU, nasi kupitia rais wetu mpendwa tukajibu mapigo kwamba hatutaki misaada yenu, serikali yetu haihitaji misaada, tutajitegemea kwa 100%.. Laaah haulaa...

Tukajifanya oooho wavimba macho wapo watatusaidia, lakini sera ya mvimba macho ni tofauti na sera ya mwenye pua ndefu katika misaada ya hisani.. Mvimbambacho umeomba kujengewa reli anakukopesha lakini sharti yeye ndie atakuwa mkandarasi na kibarua yeye... Kwamaana hiyo reli utapata, pesa nchini haitakanyaga itaishia huko huko mashariki ya mbali, na zaidi utalipa deni na pesa kwenda tena huko huko mashariki ya mbali... Watu wako wataendelea kubet mikeka na kupiga soga za kubebeana wake bila kusahau soga za simba na yanga na chadema na ccm katika vijiwe vya gahawa...

Ni taifa lipi litakaloweza kujiendesha bila kuyumba ikiwa litakosa bajeti yake zaidi ya 60%? Ni wazi kuyumba kwetu ni matokeo ya kibri cha kikundi kidogo tu cha makada wa ccm wanaoamini wao wanahati milki ya Tanzania na sisi wanatufanya kama mifugo ya kuku au bata tu.

Ugumu wa maisha waliyonayo watanzania leo ni kosa la kiserikali, sio sera za uchumi za serikali ya Rais Magufuli, wala sio katika harakati za serikali kulijenga taifa bali katika harakati za serikali kulibomoa taifa kwa uzembe na siasa za kikundi cha watu wa chache. Na sasa wanaliliza taifa na kilio wanakifanya ni ingizo la harakati za kulijenga taifa...

Serikali haikuwa na sera hii, wala haikutegemea hali hii itokee... Rejeeni ilani ya chama cha Mapinduzi.... Mkopo ya elimu ya juu ilisemaje ilani na leo nini kinatokea? Afya, usalama wa raia, kisiasa na mengineyo, leo kinachotokea kipo ndani ya ilani hiyo? Leo ccm wamembebesha mzigo mzito Rais Magufuli ilihali asingeuzimiza kichwa wala kuumiza taifa kama angepata bajeti inayostahili kama ilivyokuwa huko nyuma.

Kama kinachotokea hakipo katika Ilani ya ccm elewa hayo niliyokwambia....
 
Uongo tu hapa umeandika ili kutetea serikali
 
Kah bravo brother hii NONDO haswa..nakubaliana na hoja yako 100%
 
Uongo tu hapa umeandika ili kutetea serikali
Kweli tumetofautiana katika kuelewa duh. So hapa kumbe serikali imetetewa eti?
Mi naona kama imejikwaa alafu haina cha kufanya.
Ni kama uambiwe usisimame wala usichuchumae..
Jibu la pekee ililobakiza may be ni kuwashawishi pua ndefu kwa angalau tume huru.
Jeuri kama hii wanayofanya hivi sasa ilitaka maandalizi, sio tu kumuiga mugabe kichwa kichwa.
 
Mleta uzi nashukuru umekiri kuwa hali ngumu imetokana na kukosa misaada ambayo serikali ilikuwa ikapata huko nyuma. Iwapo kweli serikali imeweza kujiendesha bila misaada iliyokuwa ikipata basi kuna haja kubwa ya kumpongeza Magufuli kwamba kwa mwaka mmoja tumeweza kutembea wenyewe hiyo ni hatua kubwa sana kama tumeweza kwa mwaka mmoja basi inawezekana kwa miaka yote.
Ni wakati watanzania tunapaswa kufanya kazi kwa juhudi ili tulifanye taifa letu lisimame bila kujitegemea. Taifa linalotegemea misaada haliwezi kupanga mambo yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom