Ukweli kuhusu fedha za wanufaika wa chuo kikuu cha Tumaini university Makumira

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
TAARIFA KWA UMMA

Kufuatia TAARIFA zinazosambaa kwenye Mitandao ya kijamii kama jamiiforum na mengineyo. Wizara Ya MIKOPO TuMaSo inapenda kuutangazia UMMA wa WanaTuMa na jamii kwa ujumla UKWELI wa hoja ZILIZOPOTOSHWA MTANDAONI, aidha ni kwa MAKUSUDI au kwa uchache wa TAARIFA.

UKWELI ni huu, kuna vitivo vimesaini toka ijumaa..lakini SI KWELI kwamba kuna vitivo(faculties)za BEDPE 2&3,BEDMATH 2&3 na BEDECE 2&3 havijaona majina yao,UKWELI NI kwamba: BEDECE 2,BEDPE 2 na BEDMATH 2 HAWANA TATIZO na kusema hawajaona majina ni UONGO wa kuupuzwa na fedha walishawekewa kwenye ACCOUNTS ZAO.

BEDPE 3,BEDECE 3, BEDMATH 3 suala lao limeshafanyiwa utaratibu stahiki kwa kufuata ngazi husika na majina yao yameshapokelewa chuoni kwa ajili ya taratibu nyingne...
AIDHA wizara ya mikopo inakanusha kukaa kimya kwani wanawasiliana na kuwafikia walengwa kwa njia mbalimbali kupita madarasani,kwenye mitandao rasmi ya kijamii Facebook, watsapp pamoja na Instagram.

Pia, Wizara Ya MIKOPO TuMaSo inapenda kukanusha kwamba chuo kikuu cha Tumaini Makumira kufanya figisu, wizi au namna yeyote ya udanganyifu & biashara pesa za Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Wizara Ya MIKOPO TuMaSo inafanya juhudi zote zilizo ndani ya uwezo wao kuhakikisha pesa zinafika kwa walengwa ndani ya muda mfupi pasipo kuwaathiri wanachuo kisaikolojia.

Mwisho, Wizara Ya MIKOPO TuMaSo inapenda kuwasihi WanaTuMa na Jamii kwa ujumla kutafuta TAARIFA kwenye vyombo rasmi vya chuo kwa ajili ya kupata TAARIFA za KUAMINIKA.

Facebook :Wizara Ya Habari TuMaSo.
Instagram :makumirauniversity_tumaso.
Tafadhali epuka TAARIFA zisizo RASMI TOKA MTANDAONI.

Imetolewa na :
DAWATI LA MIKOPO_TUMA.
C. C
Harry_moya_Waziri wa Habari na Mawasiliano.
Alphoncina Shio_Naibu Waziri wa Habari.


14/11/2017
12:45pm
 
Hongera Dawati la Mikopo kwa umakini na uwajibikaji wenu.

TUMA Alumni.
 
Back
Top Bottom