Ukweli kuhusu fedha za Kagera

Kibstec

JF-Expert Member
May 21, 2016
1,205
2,339
Jamani watanzania wenzangu ebu wakati mwingne tunatakiwa kufahamu msimamo wetu ni nini kama nchi linakuja suala la kumchagua raisi wa kuongoza taifa hili........

Sababu kuu ya msingi ya mimi kusema nilichosema hapo juu ni kwamba..
Tunakiwa kulalamika pale tunapoona jambo fulani limefanyika nje ya kusudio la msingi naseema haya nikiwa na maana ya kauli ya jana ya mhe..Raisi juu ya matumizi ya fedha za janga lilitokea mkoani kagera...

Mzee wa watu kasema ukweli kabsa unaotoka moyoni kwake juu ya hali halisi ya wahanga wa tetemeko katika mkoa husika.....Sasa baada ya kauli hiyo wametokwea wapuuzi wachache ambao siku hizi wamekuwa ni watetezi wa mafisadi kupitia baadhi ya vijana maalumu kwenye mitandao walioandaliwa na chama fulani kuchafua kila jema analosema raisi....Mimi kwenye hili la wahanga wa kagera nilikuwa nategemea watu waje na ajenda ya matumizi ya hizi pesa hapa na maana ya kwamba..

Mfano tuseme zimepatikana billion kumi 16 jumla lakini hizo elah hazijatumika zote ndani ya mkoa husika baadhi zimemegwa na serikali kuu...Hapa kweli tungepazaa sauti zetu.....Lakini hilo halijatokea mpaka sasa hizo fedha zote zilizotumika zimeelekezwa kenye mkoa husika kuboresha miundo mbinu na huduma muhimu,,.....Na siku zote tunasema mtu unaweza kukosa makazi lakini ukawa na uhakika wa kupata huduma zote muhimu kwa binadamu amabazo zinatakiwa zime provided na serikali na ndio maana serikali imeona umuhimu katika hili.......

Ukweli lazima usemwe hili siku nyingine akirudi hapo asiwe na deni na wananchi......
 
Ukijenga shule umejengea wananchi wengi nyumba. Na niliona kinajengwa kituo cha afya kizuri kwa ajili ya wana kagera waliopata maafa. JPM yuko sahihi. Sasa ukimjengea nyumba mtu binafsi halafu mtoto wake hana pa kusoma utakuwa umeisaidiaje jamii ya wanyonge? Acheni watoto wasome tena bure sijui watz tunataka nini?
 
Issue siyo kujenga au kutojenga miundo mbinu. Issue ni jinsi serikali ilivyojipatia pesa kwa kutumia maafa ya tetemeko hili. Kilio cha kuchangisha pesa ilikuwa ni kusaidia waathirika wa tetemeko. Nia ya wachangiaji ilikuwa ni kuwasaidia waathirika kwa kuwanunulia chakula na tents (sio kujenga nyumba). Kuna watu mpaka sasa hawana pa kulala wananyeshewa mvua na chakula ni shida sana.

Kana kwamba hiyo haitoshi Serikali ilipiga marufuku watu binafsi kuwapelekea misaada moja kwa moja waathirika na kuamuru kila kitu kipitie kwenye kamati ya maafa. Hata hivyo kamati ya maafa haikutoa misaada hiyo ndio maana jana Rais ametoa agizo kwamba watu binafsi sasa ni ruksa kutoa misaada yao moja kwa moja bila kupitia kamati maalum.

Iweje Rais Uhuru Kenyatta atoe msaada wa chakula na tents na serikali yetu isiweze na kujikita kwenye miundo mbinu tu? Waamini kupitia makanisa walichanga fedha tukiamini zinaenda kusaidia wahanga moja kwa moja kumbe sivyo.

Hivi kama janga lingine (Mungu apishe mbali) kama hili likitokea kuna mtu atachangia tena? Kiukweli swala la tetemeko Kagera limevurundwa na serikali haiwezi kukwepa lawama.

Watu kwanza miundo mbinu baadaye.
 
Halafu ameagiza wote waliotoa ahadi kutimiza ahadi zao mara moja.
 
Jamani WATANZANIA wenzangu EBU wakati mwingne tunatakiwa kufahamu MSIMAMO WETU ni nini kama NCHI linakuja suala la kumchagua RAISI wa kuongoza TAIFA hili........

Sababu kuu ya msingi ya mimi kusema nilichosema hapo juu ni kwamba..
Tunakiwa kulalamika pale tunapoona jambo fulani limefanyika nje ya kusudio la msingi naseema haya nikiwa na maana ya KAULI YA JANA ya MHE..RAISI juu ya matumizi ya fedha za JANGA lilitokea mkoani KAGERA...Mzee wa watu kasema ukweli kabsa unaotoka moyoni kwake juu ya hali halisi ya WAHANGA wa tetemeko katika mkoa husika.....Sasa baada ya kauli hiyo wametokwea wapuuzi wachache AMBAO SIKU HIZI wamekuwa ni WATETEZI wa mafisadi kupitia baadhi ya VIJANA maalumu kwenye mitandao WALIOANDALIWA NA CHAMA FULANI kuchafua kila jema analosema RAISI....mimi kwenye hili LA wahanga wa KAGERA NILIKUWA NATEGEMEA watu waje na AJENDA YA MATUMIZI YA HIZI PESA hapa na maana ya kwamba..MFano tuseme zimepatikana billion kumi 16 jumla lakini hizo elah HAZIJATUMIKA ZOTE NDANI YA MKOA HUSIKA baadhi zimemegwa na SERIKALI KUU...hapa kweli TUNGEPAZAA SAUTI ZETU.....lakini hilo HALIJATOKEA mpaka sasa hizo fedha zote zilizotumika ZIMEELEKEZWA KENYE MKOA HUSIKA KUBORESHA MIUNDO MBINU NA HUDUMA MUHIMU,,.....na siku zote tunasema MTU UNAWEZA KUKOSA MAKAZI lakini ukawa na uhakika wa kupata HUDUMA ZOTE MUHIMU KWA BINADAMU amabazo zinatakiwa zime PROVIDED NA SERIKALI na ndio maana serikali IMEONA UMUHIMU KATIKA HILI.......UKWELI LAZIMA USEMWE HILI SIKU NYINGINE AKIRUDI HAPO ASIWE NA DENI NA WANANCHI......
Acha kutetea udhaifu ndugu, ni ahibu kubwa serekali kutamka maneno kama hayo. Hii inaonesha kua mfuko wa dharura haupo na serekali haina fedha.
Kujenga kituo cha afya ni wajibu wa serekali kufanya hivyo lakini watu wanapotoa fedha zao ni kwa ajili ya waanga, ndiyo maana mliweka picha zao ili watu waone huruma na waamasike kuchangia. sasa leo hii unasema kila mtu abebe mzigo wake, si dharau hiyo? mbon wakati wakuchangisha hamkusema maneno hayo? Kama ni matumizi ya fedha sisi wananchi wa Kagera tutajuaje kama fedha zote zimetumika wakati hatujaona mapato na matumizi.

Kwa kua kisu kipo mikononi mwenu ni haki yenu kufanya lolote, ila mjue Mungu anawaona, na kila jambo na wakati wake. ni wakati wenu wakatamba na kufanya jambo lolote. ila mkumbuke waliomtetea raisi Bagbo wa Ivory Cost hao hao ndio waliomkwida na kumpeleka ICC. Kwa sasa hongereni saana kwa maamuzi yenu.
 
Mkuu hiyo michango ni ya dharura kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko na wakati tunachanga tuliambiwa hivyo, serikali ina mfuko wa majanga kwanini isitoe huko fedha kujenga hizo miundo mbinu ya serikali achilia mbali kodi tunalipa.

Miaka kadhaa tuliona tetemeko lilitokea HAITI na michango iliyotolewa ilielekezwa kusaidia wahanga na sio kuzijengea barabara wala shule
Ukijenga shule umejengea wananchi wengi nyumba. Na niliona kinajengwa kituo cha afya kizuri kwa ajili ya wana kagera waliopata maafa. JPM yuko sahihi. Sasa ukimjengea nyumba mtu binafsi halafu mtoto wake hana pa kusoma utakuwa umeisaidiaje jamii ya wanyonge? Acheni watoto wasome tena bure sijui watz tunataka nini?
 
Hizo pesa si za serikali nipesa za wahanga Kama serikali ingependa kuboresha miundombinu yake ingetoa kwenye vyanzo vyake vya mapato si dhuruma ..... Hii nikumaanisha kuwa tetemeko la ardhi bukoba kilikuwa chanzo kikubwa cha mapato kuboresha miundombinu yake ....... Hata nifungwe mkuu kakosea ......
 
Serikali ilishatimiza wajibu wake wa kujenga miundo mbinu, mfano shule ya sekondari Ihungo. Sasa tujiulize hii sekondari imeenda wapi? kulikoni kuijenga tena? Miundo mbinu hii kama Ihungo si wahanga wa tetemeko? Kama miundo mbinu nayo imekumbwa na tetemeko kuna ubaya gani serikali kutumia michango ya tetemeko kuondoa baadhi ya madhara ya tetemeko?

Na washawasha!
 
Huu uzi nao ni wa kipuuzi sitatoa maoni
Maana huyu mtoa uzi ameifikirisha akili yake kwa utetezi pasipo kifikiria nini jamii inahitaji..
 
Jamani watanzania wenzangu ebu wakati mwingne tunatakiwa kufahamu msimamo wetu ni nini kama nchi linakuja suala la kumchagua raisi wa kuongoza taifa hili........

Sababu kuu ya msingi ya mimi kusema nilichosema hapo juu ni kwamba..
Tunakiwa kulalamika pale tunapoona jambo fulani limefanyika nje ya kusudio la msingi naseema haya nikiwa na maana ya kauli ya jana ya mhe..Raisi juu ya matumizi ya fedha za janga lilitokea mkoani kagera...

Mzee wa watu kasema ukweli kabsa unaotoka moyoni kwake juu ya hali halisi ya wahanga wa tetemeko katika mkoa husika.....Sasa baada ya kauli hiyo wametokwea wapuuzi wachache ambao siku hizi wamekuwa ni watetezi wa mafisadi kupitia baadhi ya vijana maalumu kwenye mitandao walioandaliwa na chama fulani kuchafua kila jema analosema raisi....Mimi kwenye hili la wahanga wa kagera nilikuwa nategemea watu waje na ajenda ya matumizi ya hizi pesa hapa na maana ya kwamba..

Mfano tuseme zimepatikana billion kumi 16 jumla lakini hizo elah hazijatumika zote ndani ya mkoa husika baadhi zimemegwa na serikali kuu...Hapa kweli tungepazaa sauti zetu.....Lakini hilo halijatokea mpaka sasa hizo fedha zote zilizotumika zimeelekezwa kenye mkoa husika kuboresha miundo mbinu na huduma muhimu,,.....Na siku zote tunasema mtu unaweza kukosa makazi lakini ukawa na uhakika wa kupata huduma zote muhimu kwa binadamu amabazo zinatakiwa zime provided na serikali na ndio maana serikali imeona umuhimu katika hili.......

Ukweli lazima usemwe hili siku nyingine akirudi hapo asiwe na deni na wananchi......

siku yakikukuta uje uandike
 
Issue siyo kujenga au kutojenga miundo mbinu. Issue ni jinsi serikali ilivyojipatia pesa kwa kutumia maafa ya tetemeko hili. Kilio cha kuchangisha pesa ilikuwa ni kusaidia waathirika wa tetemeko. Nia ya wachangiaji ilikuwa ni kuwasaidia waathirika kwa kuwanunulia chakula na tents (sio kujenga nyumba). Kuna watu mpaka sasa hawana pa kulala wananyeshewa mvua na chakula ni shida sana.

Kana kwamba hiyo haitoshi Serikali ilipiga marufuku watu binafsi kuwapelekea misaada moja kwa moja waathirika na kuamuru kila kitu kipitie kwenye kamati ya maafa. Hata hivyo kamati ya maafa haikutoa misaada hiyo ndio maana jana Rais ametoa agizo kwamba watu binafsi sasa ni ruksa kutoa misaada yao moja kwa moja bila kupitia kamati maalum.

Iweje Rais Uhuru Kenyatta atoe msaada wa chakula na tents na serikali yetu isiweze na kujikita kwenye miundo mbinu tu? Waamini kupitia makanisa walichanga fedha tukiamini zinaenda kusaidia wahanga moja kwa moja kumbe sivyo.

Hivi kama janga lingine (Mungu apishe mbali) kama hili likitokea kuna mtu atachangia tena? Kiukweli swala la tetemeko Kagera limevurundwa na serikali haiwezi kukwepa lawama.

Watu kwanza miundo mbinu baadaye.
Upo sawa mkuu
 
Ukijenga shule umejengea wananchi wengi nyumba. Na niliona kinajengwa kituo cha afya kizuri kwa ajili ya wana kagera waliopata maafa. JPM yuko sahihi. Sasa ukimjengea nyumba mtu binafsi halafu mtoto wake hana pa kusoma utakuwa umeisaidiaje jamii ya wanyonge? Acheni watoto wasome tena bure sijui watz tunataka nini?
Tafadhali futa Id yako haiendani na hadhi ya Kadhi Mkuu. Wananchi wanasubiri fedha za rambi rambi ili wajengewe kituo cha Afya. Kwa wa Tandahimba nao kwa vile kuna vijiji hawana kituo cha Afya waombe yatokee maafa ili serikali yao tukufu ikusanye rambirambi iwajengee kituo cha Afya!? Kama haya ni mawazo ya Kadhi Mkuu sijui waumini wako wana hali gani. Kwanza Mods msikubali watu wajipe Id takatifu wakati wanatetea ufirauni.
 
Halafu ameagiza wote waliotoa ahadi kutimiza ahadi zao mara moja.
Watimize ahadi wakati za awali zimelambwa, nani mwehu anaona wenzake wametoa kwa ajili ya watu lakini zinapelekwa kwenye vitu?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom