Ukweli Kuhusu Electronic Fiscal Devices ( EFDs)

Hii issue kweli wafanyabiashara wameamua kuipotosha...issue sio bei za machine coz hizo bei ni TRA wenyewe ndio wanaolipia kupitia makato ya kodi...hakuna mfanyabiashara anae nunua ile mashine kwa hela yake mkononi....ni TRA ndio itakayofanya setoff kwenye kodi....wakubwa msirukie mada kabla ya kuielewa vzr na kuanza kulaumu...huu ukwepaji kodi hauvumiliki....its time kila mtu alipe kodi sasa.
 
Tatizo kuu linatusumbua Watanzania ni kufanya mambo bila malengo na mpangilio maalum. Akili za kuzima moto haziwezi kutufikisha popote pale. Kunahitajika akili ya kuzuia moto katika kupambana na mazingira na maswala mbali mbali.

Kama kungekuwa na umoja wa wafanyabiashara kusingekuwepo na mazingira ya TRA kujiamulia mambo kama haya bila kuwahusisha kwanza wadau ili kuepuka migongano na sintofahamu kama hizi.

Where is the role of The Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) with their slogan said "alone you are weak, together we are strong". Wamefanya kazi gani katika kuwaunganisha wafanyabiashara na TRA kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara katika majukumu yao ili wawe pia linkage na Wizara ya fedha.

Where is the role of PAC, Economic Affairs, Industries and Trade Committee and also Budget Commettee katika kuwaunganisha wafanyabiashara na hazina kupitia Wizara ya Fedha.

Wafanyabiashara wamefanya juhudi gani katika kuhakikisha wanakuwa wamoja katika majukumu yao ili kuwepo na sauti nzito na kali ambayo haiwezi kupuuzwa pindi inapopigwa na wafanyabiashara.

Kama kungekuwa na umoja katika jamii ya wafanyabiashara, ninaamini hata TRA wasingefanya mambo kienyeji na kwa kificho kwa kiasi hiki bila kuwashirikisha wadau kiasi kwamba kwa sasa hakuna anayefahamu vigezo vilivyotumiwa na TRA katika mchakato huu wa kutumia machine.

Lazima tubadilike na kuwajibika katika maeneo yetu ya kazi kitu ambacho kitafanya hata serikali na taasisi zake kuwajibika hata bila kupenda.
 
punguzo umekuja na wazo zuri. Mimi najiuliza swali moja. Je nisababu zipi za msingi zinaziwafanya wafanya biashara wagome kutumia hizo mchine. Je ni kwasababu ya bei zake (initial cost) au kwavile wanajua kuwa utaratibu huu utawafanya wajulikane kipato chao basi hawataki kuzitumia. Je ni kwavile hawaoni faida ya wao kulipa kodi na hivyo kutafuta mwanya wa kuendelea kukwepa kulipa kodi?

Kuna vitu viko wazi ambavyo mimi naviona. Ukusanyaji wa kodi kwa TRA bado upo kwa kiwango cha chini, cha kusikitisha hata hicho kidogo kinachokusanya ni kiwango kidogo kinachofanya kazi za maana/kinachotumiwa kwa maendeleo. Kiasi kikubwa kinaishia mikononi mwa wachache kwa njia za deal deal. Na hiyo inawafanya watu wasione umuhimu wa kulipa kodi.
Pili hata wale wenye EFD tayari bado hawazitumii inavyotakiwa. Utakuta bado wanatumia risti zao za zamani au hatoi risti kabisa. Na mara nyingi sana na hii imenitokea mara kibao wafanya biashara anakwambia bei ya kifaa hiki ni mfano laki 7 ukitaka risti au laki 5.5 bila risti. Mteja yoyote atakimbilia kuchukua bidhaa bila risti na mwisho wa siku mfanya biashara ananufaika kwa kukwepa kodi. Lakini ki u-halisia huwa wanaongeza bei kumtisha mteja na hivyo kusababisha mteja akubali kutochukua risti. TRA needs to workout that, vinginevyo mtakuwa na hizo EFD lakini bado efficiency yenu ya kukusanya kodi itakuwa ndogo. Usahauri wangu kama zipo machine zinazoweza kupatikana kwa bei ndogo kama ulivyo pendekeza itakuwa ni jambo zuri. Lakini pia wanaweza kuwakopesha wafanya biashara na wakawa wanawakata hela yao kidogo kidogo hadi itakapo isha. Tusilazimishe kununua machine hizo kwa hela ndefu hivyo. Si kila mfanya biashara anahela ya kutoa kwa haraka na hasa anapogundua kuwa hicho kifaa hakimsaidi kama wanavyoelezwa eti kutunza kumbukumbu. Ingekuwa kweli wao wanaona kitawasaidia basi wangekimbilia, kumbukumbu zao wanazo ila huwa wanajaribu kuzificha na kwasababu TRA hawanauwezo wa kuzipata hujikuta wakiwakadilia malipo kidogo ya kodi licha ya kwamba utaona wengi wanalalamika kama vile wamekadiliwa kwa kiwango cha juu.

Wito wangu: Serikali ijitahidi kutumia vizuri kodi za wananchi, hii itawafanya wananchi ambao ndo walipa kodi waone kwamba kodi yao inatumika vizuri. Binafsi huwa nasikitika naposikia watu wamepiga hela za miradi flani, au wanafanya ubadhilifu, au wanatumia vibaya magari ya serikali. Wanafanya uchakachuzi katika sekta mbalimbali huwa nasikitika sana. Najua mwisho wa siku sisi ndo tunaumia maana hizo ni kodi zetu. Ukweli ni kwamba kama wafanyakazi wa nchi hii nao wangekuwa na option ya kukwepa kulipa kodi ya mapato (pay as you earn) watu wasingelipa. Hakuna mtu anayegoma kulipia huduma na hasa anapoona huduma zinzotolewa ananufaika nazo.
Watu hawana hospitali, viongozi wanakimbizwa nje wanapougua, shule zetu zinakwisha watoto wa viongozi wanasomeshwa nje au shule private nzuri. Barabara mbovu, tembelea maeneo wanapokaa wao. Huduma za maji na umeme mbovu kwao wanapata masaa yote. Sasa mtu anajiuliza kwanini nilipe kodi. Kwanini nami nisifanye saving itakayo nisaidia baadaye nitakapo ihitaji.

Swadakta. Mkuu umenena. Kama raia mwema unalipa kodi imlipe mbunge, itolewe ruzuku kwa vyama vya siasa au imlipe askari polisi mshahara. Halafu eti, mbunge atumie kodi yangu kubamba na kubaka binti zangu! Polisi niliyempa mshahara asifanye kazi yake barabara. Kiongozi wa chama auchune na mwingine wa chama kupitia wazazi amtetee 'mbakaji'?
 
Last edited by a moderator:
Mwanaume think on your own,,usisaidiwe kufikiri,,tatizo lako umeshalishwa sumu kuhusu hizi machine na wakwepa kodi and you come here talking cheap.....hayamkini huna hata uelewa wa mambo ya kodi.poor you,,,unafatafata mkumbo tu??!!!!idiot.
Hivi wewe ni mwanaume au mwanamke!!!!!
Hebu weka wazi ujulikane nia yako maana kila unapokuja mjadala wa EFD lazima ulete mada ya ku divert attention kuwa kuna ajenda ya siri,au wafanya biashara hawataki kulipa au kuwa wafanyakazi wanakatwa na mambo kama hayo!!!!!!

Jua kitu kimoja kuwa hawaTRA ndio wanajukumu la kuondoa ambiguities zote hizo unakurupuka nazo kwa kuwekeza wao katika muundombinu huu ili tumalize hili suala tufuate ajenda nyingine za manufaa ya nchi!!!!!!

Umeagizwa na nani na.unalipwa shilingi ngapi,if I may buy you out madam!!!!!!
So that we(without you) can pave the way for a more brighter and sustainable means to build this Nation!!!!!
 
issue sio tulia kodi mkuu, issue ni bei ya efds kuwa juu. umeelewa?
Mkuu issue sio bei coz bei TRA inakuja kufanya setoff kwenye kodi,,so hakuna mfanyabiashara hata mmoja atakayelipa kutoka hela yako mfukoni,,tusifuate mkumbi wakubwa na wala kulishwa sumu na hawa wakwepa kodi,,,issue hapa ni kuthibiti wakwepa kodi,,,they are damn rich kwa sababu ya kukwepa kodi na gap la masikini na tajiri linazidi kuongeza kwa sababu hiyo.
 
Kwa hizo mashine zimefungwa kamera ili kujua ni kitugani kimetok na kipi kimeingia? Kama jibu ni hapana wizi utakuwa palepale watauza na hawatatoa risti.

Wizi utakuwepo kwa kiasi kidogo na utapungua kwa kiasi kikubwa kama TRA wamedhamilia kufanya Mapinduzi ya kweli katika ukusanyaji wa kodi, kama wamejipanga, wanajua ni divice ipi inafaa kwa mazingira ya technology ya tanzania na wakatueleza ni jinsi gani watamonitor, watamanage na ku-control kuepuka mianya ya ukwepaji kodi, kutakuwa hakuna tatizo kabisa. Pia watafanikiwa zaidi kama wakiwa wawazi na wakweli, wakielimisha wananchi, na wakifanya kwa malengo ya kuinua uchumi kwa kupunguza mianya ya ukwepaji kodi na sio kufanya kama kwamba ni fursa ya biasasha kwa TRA.

The use of fiscal devices in the world can be divided into three main categories:

  1. Offline operating electronic fiscal devices with built-in fiscal memory (so called first generation fiscal devices);
  2. Electronic fiscal devices with Internet connection capabilities to the revenue authority central server (so called second generation fiscal devices);
  3. Electronic fiscal devices with Internet connection capabilities and latest use of various encryption methods for digital signing of each issued receipt (third generation fiscal devices).
Due to the main disadvantages which the first generation fiscal devices are having i.e. easy manipulation, lack of control from the tax office, no printing of fiscal receipts etc., the second generation fiscal devices are becoming more and more popular and many countries are changing their fiscal requirements and moving to Internet enabled fiscal devices (mostly using GPRS network) and implementing the so-called online Information and Tax Collection System.[SUP][

[/SUP]

Such kind of second generation fiscal devices are eliminating most of the problems which their predecessors were having. All fiscal cash registers and fiscal printers are connected online through the Internet to the central server and sending their reports and/or fiscal receipts in predefined time intervals. However these devices still have some black holes which are used by the majority of tax payers who are cheating and not paying their taxes. Such are: printing of fake fiscal receipts, manipulation of daily reports before they are sent to the tax office etc.
This is why the third generation fiscal devices were introduced and running successfully currently in several countries in the world. These kind of devices are very similar to the second generation devices but an additional software security is used for digital signing of every fiscal receipt. The third generation fiscal devices are eliminating all previously known issues and giving additional security to all tax agencies which are using such systems. Each fiscal receipt is digitally signed using unique signature printed either in the form of a 2D Bar Code or various characters depending on encryption rules in place. The tax administration can easily and quickly check if the issued receipt is authentic and correct.
 
Wangezigawa bure, kwanini vifaa vya kuwasaidia kwenye kazi yao wanunue wengine?
Basi askari nao waanze kununua bunduki wao wenyewe wanapoajiriwa.
 
Hii issue kweli wafanyabiashara wameamua kuipotosha...issue sio bei za machine coz hizo bei ni TRA wenyewe ndio wanaolipia kupitia makato ya kodi...hakuna mfanyabiashara anae nunua ile mashine kwa hela yake mkononi....ni TRA ndio itakayofanya setoff kwenye kodi....wakubwa msirukie mada kabla ya kuielewa vzr na kuanza kulaumu...huu ukwepaji kodi hauvumiliki....its time kila mtu alipe kodi sasa.

Kwahiyo wanapewa Bure?
 
Mod, kama inawezekana nakuomba ufute posts za hasira na zisizo na lugha nzuri. Huu uzi sio wa ugomvi au wa kisiasa ni moja ya swala muhimu na la msingi katika taifa letu. Huu mradi pia utasaidia kujenga maadili katika biashara, hata mambo ya nipunguzie nipunguzie yatapungua au mambo la kulanguliwa !
Tatizo ni mchakato, ukweli na uwazi katika utekelezaji wa huu mradi.
 
Jamani ndio maana mijadala mingi inakosa lengo kuu.Hapa tuache kujadili tatizo la wafanyabiashara kutolipa kodi maana ni mjadala mpana sana.Mada kuu ni gharama za EFD na sijasikia popote wafanyabiashara wakigoma kulipa kodi zaidi ya uzembe wa TRA tu na mfano mimi nayafahamu makampuni tena makubwa ambayo hata assessment ya kodi haijawahi kufanyika yaani kampuni inajilipia tu kodi itakavyo!

Mjadala ni bei za machine za EFD na sio ukwepaji kulipa kodi. Tusipoteze uelekeo wa mjadala huu.

Well stated!! Tatizo sio kodi ni hicho kidude chao.
 
Pamoja kuwa kulipoa kodi ni mada tofauti ukweli nikwamba wafanya biashara waliogoma wanachozungumzia ni kwamba hawataki machine.
Nawelewa kwamba machine zitawalazimu kulipa kodi ambazo wafanyabiashara hawa wamekuwa wakikwepa.

Ni wakati wafanyabiashara hasa wa kariakoo nao waanze kulipa kodi.
 
Pamoja kuwa kulipa kodi ni mada tofauti ukweli nikwamba wafanya biashara waliogoma wanachozungumzia ni kwamba hawataki machine.
Nawelewa kwamba machine zitawalazimu kulipa kodi ambazo wafanyabiashara hawa wamekuwa wakikwepa.

Ni wakati wafanyabiashara hasa wa kariakoo nao waanze kulipa kodi.
 
Something is behind this mgomo...but the bottom line is TRA ikicheka na wafanyabiashara hakuna kodi itakayokusanywa....hawa sio watu wa kuwachekea kabsa...pamoja na vipato vyetu vya chini wafanyakazi tumelipa kodi sana....tuanze kugawana maumivu sasa na kuongezwa tax base kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii.

Ndugu, unajadaili NJE ya mada.
Hapa mjadala ni mashine zenyewe, yaani EFD. Kwamba, bei hali ya mashine hizo ni mara 15 chini ya bei wanazouza kwenye maduka yaliyopendekezwa na TRA. Kwa nini hali iko hivyo? Kwa nini TRA wasiache biashara ya EFD iwe huru kama zilivyo calculators na laptop?
 
Wabongo tumezoea sana wizi na kukwepa, wafanya biashara wamezoea super profit, kwa vile sasa mashine zitaonyesha kila kitu, nanataka kuzigomea!. Mbona wahindi wanazitumia na hawagomi?!.

Anayelipa kodi ni end user, hivyo anayepaswa kugoma ni mteja baada ya kupandishiwa bei kufuatia wafanya biashara kulipa kodi!, na sio wafanya biashara wagome kuuza, kisa kodi iko juu!. Huu sasa ni mwanzo mzuri wa hivi vibiashara mchoro mchoro vifungwe zibaki biashara halali tuu!.

Kwa upande wa EFD, nako ni wizi mtupu!, mashine inauzwa dola 100, hapa unauziwa dola 1000!.
Ukiamua kununua mwenywe, wale maajent wa TRA hawakubali ku install!.
Mijimashine yenyewe approved kwa Tanzania yote inatumia windows only kwa sisi tunaotumia mac, tunalazomika kununua computer ya window kwa ajili ya EFD tuu!.
Huu pia ni nyanyasaji!.
Pasco.
Pasco.

naomba kuuliza swali ambalo liliulizwa na mtu huko nyuma

Je nchi za Ulaya, usa, south africa wanatumia mashine zipi?

Kenya na Rwanda wanatumia mashine zipi?
 
punguzo umekuja na wazo zuri. Mimi najiuliza swali moja. Je nisababu zipi za msingi zinaziwafanya wafanya biashara wagome kutumia hizo mchine. Je ni kwasababu ya bei zake (initial cost) au kwavile wanajua kuwa utaratibu huu utawafanya wajulikane kipato chao basi hawataki kuzitumia. Je ni kwavile hawaoni faida ya wao kulipa kodi na hivyo kutafuta mwanya wa kuendelea kukwepa kulipa kodi?

Kuna vitu viko wazi ambavyo mimi naviona. Ukusanyaji wa kodi kwa TRA bado upo kwa kiwango cha chini, cha kusikitisha hata hicho kidogo kinachokusanya ni kiwango kidogo kinachofanya kazi za maana/kinachotumiwa kwa maendeleo. Kiasi kikubwa kinaishia mikononi mwa wachache kwa njia za deal deal. Na hiyo inawafanya watu wasione umuhimu wa kulipa kodi.
Pili hata wale wenye EFD tayari bado hawazitumii inavyotakiwa. Utakuta bado wanatumia risti zao za zamani au hatoi risti kabisa. Na mara nyingi sana na hii imenitokea mara kibao wafanya biashara anakwambia bei ya kifaa hiki ni mfano laki 7 ukitaka risti au laki 5.5 bila risti. Mteja yoyote atakimbilia kuchukua bidhaa bila risti na mwisho wa siku mfanya biashara ananufaika kwa kukwepa kodi. Lakini ki u-halisia huwa wanaongeza bei kumtisha mteja na hivyo kusababisha mteja akubali kutochukua risti. TRA needs to workout that, vinginevyo mtakuwa na hizo EFD lakini bado efficiency yenu ya kukusanya kodi itakuwa ndogo. Usahauri wangu kama zipo machine zinazoweza kupatikana kwa bei ndogo kama ulivyo pendekeza itakuwa ni jambo zuri. Lakini pia wanaweza kuwakopesha wafanya biashara na wakawa wanawakata hela yao kidogo kidogo hadi itakapo isha. Tusilazimishe kununua machine hizo kwa hela ndefu hivyo. Si kila mfanya biashara anahela ya kutoa kwa haraka na hasa anapogundua kuwa hicho kifaa hakimsaidi kama wanavyoelezwa eti kutunza kumbukumbu. Ingekuwa kweli wao wanaona kitawasaidia basi wangekimbilia, kumbukumbu zao wanazo ila huwa wanajaribu kuzificha na kwasababu TRA hawanauwezo wa kuzipata hujikuta wakiwakadilia malipo kidogo ya kodi licha ya kwamba utaona wengi wanalalamika kama vile wamekadiliwa kwa kiwango cha juu.

Wito wangu: Serikali ijitahidi kutumia vizuri kodi za wananchi, hii itawafanya wananchi ambao ndo walipa kodi waone kwamba kodi yao inatumika vizuri. Binafsi huwa nasikitika naposikia watu wamepiga hela za miradi flani, au wanafanya ubadhilifu, au wanatumia vibaya magari ya serikali. Wanafanya uchakachuzi katika sekta mbalimbali huwa nasikitika sana. Najua mwisho wa siku sisi ndo tunaumia maana hizo ni kodi zetu. Ukweli ni kwamba kama wafanyakazi wa nchi hii nao wangekuwa na option ya kukwepa kulipa kodi ya mapato (pay as you earn) watu wasingelipa. Hakuna mtu anayegoma kulipia huduma na hasa anapoona huduma zinzotolewa ananufaika nazo.
Watu hawana hospitali, viongozi wanakimbizwa nje wanapougua, shule zetu zinakwisha watoto wa viongozi wanasomeshwa nje au shule private nzuri. Barabara mbovu, tembelea maeneo wanapokaa wao. Huduma za maji na umeme mbovu kwao wanapata masaa yote. Sasa mtu anajiuliza kwanini nilipe kodi. Kwanini nami nisifanye saving itakayo nisaidia baadaye nitakapo ihitaji.

umenigusa sana mkuu.Watanzania hawa hawa wanaoona ugumu kulipa kodi kwa serikali,ndio hawa hawa wanaopanga foleni kuingia viwanja vya michezo,disko,kumbi za starehe tena kwa gharama kubwa,iweje hawapendi kulipa kodi?something must be wrong somewhere!watu hawaoni faida ya kodi ndio maana anaona bora hela yake anywe pombe ambayo hata kama ina negative impact lakini anaiona impact kuliko kupeleka pesa mahala pasipo na return au ndogo sana!
 
Last edited by a moderator:
Something is behind this mgomo...but the bottom line is TRA ikicheka na wafanyabiashara hakuna kodi itakayokusanywa....hawa sio watu wa kuwachekea kabsa...pamoja na vipato vyetu vya chini wafanyakazi tumelipa kodi sana....tuanze kugawana maumivu sasa na kuongezwa tax base kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii.

Ndugu yangu, mimi ninafanya kazi Advatech Office Supplies hii ni kampuni imeanzia Kenya na ipo TZ, Zimbabwe, Rwanda, Uganda, Malawi, na sasa itafunguliwa ofisi Juba, South Sudan. Mimi ninafanya kazi ya ku Train operators (customers), ku install/program, ku repair, ku consult clients or new buyers, na ku sell hizi efd (E-Sign, Fiscal Printers, na ETR). Ninafanya kazi katika maeneo ya Dar, Moro, Dom, Singida, Tabora, Lindi na Mtwara. Najua mambo mengi sana kwenye hii industry.

Phase I ilianza 2012 na ni wale ambao revenue ni above TZS 40m kwa mwaka. Ukiachia domestic large tax payers, hawa domestic wadogo katika ile phase I walikuwa moto wa kuotea mbali kukubali kutumia EFD kipindi hicho 2010, ila leo hawana shida, wanakutafuta wenyewe uwauzie.

Kipindi cha phase I mashine ya bei rahisi mwanzoni ilikuwa ETR DP50 (mobile device) TZS 1.593m, ingawa kulikuwa na ETR zingine zilikuwa bei ya juu kidogo, kuhusu E-Sign na Fiscal Printer ilikuwa bei moto 3.5m na 2.7m respectively.

Warrant ilikuwa mwaka mmoja.

Hawa wa sasa phase II (siyo VAT registered, only TIN ila revenue zao kwa mwaka ni TZS 25m and above) ambao wanatumia EFD, ETR peke yake na hasa kwa ofisi yetu wanauziwa DP25 kwa 800,000/= na anaweza kulipa kidogo kidogo ila kwa kuanzia si chini ya 400,000/=. Hela ya kununua EFD atarudishiwa TRA kwenye return zake mpaka hela yote iishe, the same to phase I.
Warranty ni miaka mitatu (3).

Sometimes huwa tunailalamikia sana serikali, ila kiasili hawa walipa kodi wadogo hawapendi EFD kwa kuwa zinaweka mambo wazi sana hivyo kuwafanya wasiweze ku-dodge tax kirahisi. Wafanyakazi ndiyo walipa kodi wazuri sana nchi hii.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom