DOKEZO Ukweli kuhusu changamoto zinazosababisha Shirika la Bima ya Afya Tanzania (NHIF) kuanguka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Mengi yamejadiliwa kuhusu jinsi ya kutatua tatizo la shirika la bima ya afya Tanzania NHIF kufilisika lakini je tuna taarifa za kutosha zinazoweza kutuwezesha kufanya maamuzi sahihi?. Bima ya afya kwa wote ni sera nzuri itakayo wawezesha watanzania kupata huduma bora kila wanapo ugua lakini tusifikirie kwamba kipato hiki cha ziada kita tatua tatizo la fedha lililopo kwenye shirika au kuliwezesha shirika kuwa hudumia watanzania kwa ufanisi zaidi.

Ni muhimu kufahamu sababu zinazofanya shirika kuanguka ili kuhakikisha kwamba haya yote hayajirudii. Nitaeleza kwa ufupi kuhusu changamoto zilizopo NHIF na jinsi ya kuzitatua

Nianze kwa kusema kwamba mali bila daftari hupotea bila habari. Hadi sasa, hospitali zinazo wahudumia wagonjwa kupitia mfuko wa NHIF hazina mfumo wa kompyuta wakuliwezesha shirika kupata uhakika kuhusu huduma zinazotolewa kwa wahusika au kufahamu idadi ya dawa zilizopo hospitalini kwa ajili ya wanufaika wa mfumo huu. Mbadala kwa mfumo huo, hospitali zetu hutumia mfumo wa kompyuta unaoitwa "JEEVA". Mfumo huu umetengenezwa India na hutumika na hospitali zetu kupata nakala hizo.

Shirika la NHIF hutegemea fomu za bima zilizojazwa kwa mkono kulipa hospitali na vituo vya afya mbalimbali kwa kutoa huduma kwa wagonjwa.

Pili, mfumo wa JEEVA hautoi mchanganuo wa vifurushi vilivyopo NHIF bali huonyesha tu kama mgonjwa ana "Brown card" au "Green card". Shirika la bima ya afya lina vifurushi 66 vyenye malipo tofauti na benefits tofauti kwenye matibabu husika. Kwa mfano, familia ya baba, mama na watoto wanne inaweza kuchangia 816000, 900000, 1452000, 1584000 au 2028000 kila mwezi na kwasababu hiyo, vifurushi vyote vitano vina benefits tofauti.

Mfumo wa JEEVA kushindwa kutoa mchanganuo wa vifurushi vyote vya bima na limit ya bima kwa kila mgonjwa kunaweza kusababisha hospitali kutoa huduma ambazo haziko covered kwenye kifurushi husika haswa kwa wanufaika ambao wanaweza kuugua zaidi ya mara moja kwa mwezi au kwa wanufaika ambao lazima wapate huduma zenye gharama kubwa mara kwa mara kama dialysis.

Imesemekana kwamba magonjwa ambayo haya ambukizi kama presha na kisukari yame changia kwa kiasi kikubwa kuanguka kwa shirika hili lakini tufahamu kwamba kimo cha chini kabisa cha NHIF kina changiwa 192,000 kwa mwezi. Ili suala hili lisababishe kufilisika kwa NHIF lazima wagonjwa wengi wapate matibabu mara nyingi kwa mwezi na kwa muda mrefu. Katika haya yote, tuelewa kwamba hamna bima ambayo haina kikomo.

NHIF wana utaratibu wa wagonjwa kupata dawa kwenye famasi ambazo zipo nje ya hospitali endapo dawa hizi hazipatikani hospitalini. Katika hili, wanufaika huandikiwa fomu 2c ambayo hutumika kwa sababu hii. Famasi ambazo zipo nje ya hospitali hutumia "portal" ya NHIF kuweza kuwa hudumia wagonjwa hawa.

Changamoto iliyo hapa ni kwamba portal hii haitoi mchanganuo wowote wa vifurushi tofauti tofauti vinavyo changiwa na wanufaika. Sambamba na hilo wagonjwa hawa nufaiki vya kutosha na huduma hii kwasababu fedha inayolipwa na bima kwa ajili ya dawa haiendani na uhalisia wa gharama za dawa sokoni kwa muda huu.

Suala lingine ni kwamba precribing kwa wagonjwa wa NHIF hufanyika kwa kutumia disease codes. Yaani bima wana mwongozo unaotumia tarakimu kufafanua ugonjwa ambao mnufaika anaumwa. Kama ufasaha ulitumika katika kujaza nyaraka hizi basi disease code yoyote lazima iendane na vipimo ambavyo mgonjwa alifanyiwa na dawa ambazo mgonjwa alipata.

Makosa katika kitengo hiki husababisha matumizi mabaya ya vipimo na dawa zinazo tolewa kwa wagonjwa. Vilevile, hospitali na famasi zilizo nje ya hospitali hushindwa kupata malipo kikamilifu kutoka NHIF kwasababu ya nyaraka hizi kukosewa kwenye claims form.

Katika mfumo huu ambao makaratasi huwezesha NHIF na hospitali kufahamu kuhusu matibabu ya wagonjwa, kupotea kwa kumbukumbu hizi hufanya shirika lisifahamu ukweli kuhusu matibabu ya wahusika na hospitali zisinufaike kikamilifu kwa mpango huu wa bima. Naamini tuna kubaliana kwamba lazima wahusika wote hospitalini na NHIF wafanye kazi kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu bila usimamizi kuhakikisha kwamba masuala yote yanafanywa sawa.

Haya yote yanatupa picha fulani kuhusu hali iliyopo NHIF lakini naamini kwamba kuna mambo mengine ambayo sijaweza kujadili. Tunaweza kufahamu umuhimu wa kuwa na takwimu za muda mrefu ili kupata mwanga zaidi lakini hilo haliwezekani kwasababu shirika la bima ya afya halina taarifa zozote kuhusu idadi ya wagonjwa wanao tibiwa katika hospitali zetu na matibabu wanayoyapata.

Ninakubali kwamba serikali haiwezi kumudu kuwapa wananchi wote huduma bure za aya lakini kabla ya kupitisha sera mpya ya bima ya afya kwa wote, kuna umuhimu wa kufanya tathmini ya kina ili kufahamu jinsi ya kufanya shirika la NHIF liwe profitable. Sambamba na hilo, sio sahihi kwa hospitali zetu kuendelea kutegemea mafungu kutoka serikalini kila mwaka. Huduma nzuri za afya zinatakiwa kuwa nufaisha watanzania kwa vizazi vijavyo na kwasababu hiyo hospitali zetu zote zinatakiwa ziweze kujiendesha.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania
 
Hizi ni operational problems. Sasa kazi ya MANAGEMENT ni nini kama hawawezi kutatua matatizo madogo kiasi hicho?

Mtoa nada umechambua vizuri sana, sasa weka uzoefu wa wa management team. Tusiwalaumu Bure yawezekana uwezo wait ni mdogo kuliko kazi waliyopewa
 
Back
Top Bottom