SubiriJibu
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 1,803
- 1,863
- Thread starter
- #21
Ndugu Subirijibu.... Nimesikitishwa sana na ujasiri wa kutetea uwoga wako na utraitor wako... mimi ni miongoni mwa G211 na ni mmoja wa viongozi tuliongoza kundi la G211 NA KUSHINDA KESI DHIDI YA CHUO... Naikumbuka sana historia hii na haitakuja kutoka kichwani pangu.... sina haja ya kurudia historia nzima hila napenda kukufahamisha haya machache kwa faida ya wana Jf na kuweka kumbukumbu sahihi..
Tuna kila sababu ya kuwaita nyinyi matraitor kwa sababu .... sheria za chuo zilieleza wazi kwamba mtihani ukichelewa au mwanachuo akichelewa kufika kwenye chumba cha mtihani kwa zaidi ya dk 30 hataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha mtihani na vilevile mtihani ukichelewa kwa dk 30 ... wanafunzi wanaweza kutoka kwenye chumba cha mtihani unless kuna taarifa za kuchelewa kwa mtihani... Tukio lilivyotokea ni kwamba mtihani ulichelewa zaidi ya masaa 2 na bila taarifa YOYOTE.
Muonamambo,
Hapa ndipo hata anayesoma thread hii anapoona mlikosea. Ukiichukulia kama unavyoileta unaweza kudhani ni kweli mtihani ulichelewa na hakukuwa na taarifa yoyote.
Ni kweli mtihani ulichelewa. Lakini je ni kweli hukuwa na taarifa yoyote? Kama hukuwa na taarifa yoyote ulikuwa unafanya nini eneo la FOE tena mmekaa kundi kubwa mnaongelea tukio hilo?
Usidanganye watu hapa. Nimesema na haujakanusha ni kwamba mzozo huo ulianza mwezi April na mliujua. Taarifa mlishaambiwa kwamba Mathematics Department haita-liaise na Engineering first year hadi wa-apology. Hukupata taarifa hii?
OK, siku ya mtihani, tulikusanyika pale nje na tukakubaliana tusiondoke hadi tujue Class Reps wamekubaliana nini na Lecturers. Ulitaka taarifa gani wakati viongozi wako wako mazungumzoni na hujapata feedback.
Halafu unasema kuwa ni u-traitor nione aibu. Nitaonaje aibu kutetea history ambayo mmeipotosha kwa miaka mingi.
Tatizo lenu ni kwamba hata kwenye mikutano hamkutaka wenzenu tutoe hoja mkawa mnatumia ubabe na kuzomea mkipewa vipande.
Unakumbuka bwana mmoja alieleza walimu walivyowakuta darasani mkamzomea na kumuita "WA NDANI WA NDANI WA NJE WA NJE".
Lete hoja tusahishe history.
SOTE tulikubaliana ya kwamba tusiendelee na mtihani hule na kwa vile wengine walikuwa na mitihani inayofuata muda wa mchana... sasa matraitor wachache kama wewe mliendelea kufanya mtihani hata baada ya kuletwa masaa ma 3 baadaye..
Uongo ambao unapimwa kwa kitu kidogo tu. Kama wote tulikubaliana, iweje wale Class reps wakae kule ofisini waki-discuss jambo lile. Unataka kutuambia wakati Sweke, Karungubare na Kitilinga mlishawapindua mkaweka resolution yenu nyingine kabisa.
Na kama mlishakubaliana si mngeondoka mlikuwa mnasubiri nini maeneo yale huku mitihani mingine ikiwasubiri jioni. Uongo mtupu.
Hata baada ya kuendelea na mtihani, tuliokuwa nje tuliwasihi mtoke ili tuwe na msimamo wa pamoja nanyi mliweka masilahi yenu mbele kama mafisadi na kusahau masilahi ya wengi..
Ona unavyojichanganya katika jambo hili. Sasa kama sisi tulikuwa ndani ya exam room na nyinyi mlikuwa nje, mlitusihi kwa mawasiliano gani. Kwamba mlikuwa mnakuja darasani mnatutangazia halafu sisi tunakataa?
Huu ni uongo ambao kila anayejua logistics za mtihani ataung'amua. Ukiingia kwenye exam room mtu wa kwanza kukutana naye ni msimamizi au invigilator. Sasa mliwezaje kumvuka invigilator aache kusimamia exam awape muda mtangaze azama yenu kututaka tuache mtihani kisha akawaruhusu mtoke ili sisi ama tukubali ama tuache.
Ni uogo ambao hauwezekani. Kilichotokea inawezekana kweli mlikuwa mnatuma watu kuja kututoa. Lakin badala yake watu hao wakifika mlangoni wanaona kila mtu amejipinda kwenye pen wanaajiunga pia kuwa na sisi. Na bahati yenu sheria ilikuwa ni nusu saa lakini ingekuwa zaidi basi wengi tu wangechomoka huko kwenu wakaja kufanya paper maana tatizo la wengi walidhani kutokana na mzozo basi Mathematics wametukomoa ili tufeli lakini mtihani ule kumbe ulikuwa rahisi na kila mtu angefaulu.
Napenda kuwapongeza tena wana G211 kwa moyo wa kizalendo na wa kijasiri wa kuungana pamoja dhidi ya udhalimu wa chuo/serikali na kushinda ... nawatakia kila la heri kwenye shughuli zenu na mungu akipenda aweze kutuunganisha tena ili tushinde vita dhidi ya ufisadi kwani naamini bado mnaendeleza mapambano huko mliko
Hapa ndipo mlipopotoka. Nimeeleza kirefu hadi inachosha lakini lengo langu ieleweka kuwa mzozo haukuwa na sura yoyote ya kisiasa au hata kiutawala.
Mbona hata siku moja hamkutaka tuujulishe umma kwamba chanzo cha mzozo ni ile test ngumu ya vector calculus yenye curl na divergence. It was a pure academical matter and never administrative or political.