Ukweli kuhusu Azimio la Arusha

sinajinasasa

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
2,989
4,129
Nilikuwa naangalia TBC habari jioni hii.
Sam Mahela akawa anasoma habari ya Mzee mmoja ambaye anaomba arudishiwe nyumba zake zilizotaifishwa na serikali mwaka 1971.

Tukio la habari hiyo halikuweza kusomwa karibu mara mbili baada ya mtangazaji kusema taarifa hii haipo tayari, nina wasi wasi walioandaa taarifa hiyo walizuiwa kuirusha hewani ili kuficha maovu yaliyofanywa na chama na serikali kipindi hicho.

Kipindi hicho xha Azimio la Arusha, ambapo mali za wananchi matajiri au waliokuwa na uwezo walifilisiwa mali zao, sera hizo hazikuwafurahisha wengi na wengine kama Wakina Kambona walitorokea Uingereza.

Lengo la kuwafukarisha wananchi ni kufanya chama kiweze kuwatawala wananchi kinavyotaka bila kupata upinzani wa aina yoyote, kwa vile inaeleweka mtu akisha kuwa wealthier ni vigumu kumtawala.

Kipindi hicho waziri mkuu Kawawa alitekeleza vyema sera hizo za kuwatia watu umasikini kwa kuunda vijiji vya ujamaa, kwa kauli za wanasiasa walisema kwamba tunaunda vijiji ili iwe rahisi kwa serikali kuwahudumia, lakini kumbe nyuma ya pazia lengo lake ni kuweza ku control umma, kujua nani anatupinga.

Zoezi hilo lilileta njaa kubwa nchini, maana watu waliacha mashamba na mifugo, mashamba ya miti na majumba, magari ya kijeshi yalikusanya watu kwa nguvu kuwapeleka kwenye vijiji vya ujamaa, mashamba mengi yaliachwa na mazao yake na kuwa mapori
Wajamaa au wasoshalisti hawapendi kupingwa, naangalia jinsi nchi za kijamaa zilivyo na shida, nchi ambazo viongozi wake wanajitamba kuleta maendeleo, wanajidai wana pesa, lakini kumbe wanategemea misaada ya nje kuendesha serikali zao, wajamaa kama wakina Maduro, Mugabe marehemu, nchi za Ethiopia, Zambia, Eritrea nchi kama Kyjgistan, Venezuela na baadhi ya nchi za Ulaya kama Hungary, Poland nk ni mateso matupu watu wana shida, serikali ni njaa tupu.

Hayo ndo mambo ambayo CCM ni sera zake, kwamba umasikini wa wananchi ndo uhakika wa Viongozi wake ku survive, wana lugha nzuri hadharani lakini wakijifungia chumbani ni fisi wala nyama.
Hawataki kabisa uwakosoe, watu wamejaa uwoga wa kutawaliwa, na watawala wana enjoy sana hali kama hii kwa kuwa hakuna anaye wa challenge.
Sam Mahela ajiangalie, anaweza kufukuzwa TBC akidhani yupo huru kama ITV, habari za TBC lazima waziri au serikalini wazichekeche kabla hazijaenda hewani.

Alamsiki, naenda kulala.
Nna wasiwasi pia kama uzi huu uta trend kwa kuwa wajamaa wapo na mikono mirefu kila kona.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata sisi kwetu Kyela, shamba letu.lilichukuliwa na kulifanya la Kijiji baada ya ujamaa kuisha limebadirishwa na kuitwa la ccm. Yaani kila nikikumbuka, naumia Sana.

Basi tu ipo siku ccm itatoka.

Tutakuwa huru, na kufanya maendeleo yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ndio maana hua namshangaa zitto, kijana mdogo anamlengo wa siasa wa ajabuajabu, ujamaa ni ujinga na umasikini.
 
Back
Top Bottom