Ukweli kuhusu asilimia 80% ya mapato ya Serikali inatoka Dar es salaam

PUNKY

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
560
250
Imekuwa ikinipa tabu kuamini kauli za viongozi mbalimbali wakisema asilimia 80% ya mapato ya serikali inatoka Dar es salaam. Kauli hii inatia shaka kwa kuzingatia kuwa Dar ni sehemu ndogo tu katika nchi hivyo si sahihi kuwa inatoa asilimia zote hizo pekee, ukizingatia raslimali nyingi zipo sehemu nyingine ya nchi.
Naomba wenye uelewa wa hili watupe ufafanuzi, ni vigezo gani vinavyotumiwa kuthibitisha 80% ya mapato ya serikali yanatoka Dar.
Ufafanuzi huu ni muhimu kwani inaleta unyonge kwa mikoa mingine kuonekana si chochote katika uchumi wa taifa ili.
 
Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,700
2,000
Ni kutokana na Malipo mengi kufanyika Dar , unakuta Barrick Malipo yao yote wanaifanyia Dar wakati hawazalishi Dar, nk nk ni kutokana na mfumo mbovu .....uliopo
 
PUNKY

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
560
250
Mimi ni mtumishi wa serikari nipo Mwanza, PAYE ninakatwa moja kwa moja hazina Dar, kwa hiyo iyo pesa inahesabika kuwa ni mapato ya dar na si mwanza ninapozalisha?
Hii sio sawa inabidi warekebishe.
 
TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,306
2,000
Imekuwa ikinipa tabu kuamini kauli za viongozi mbalimbali wakisema asilimia 80% ya mapato ya serikali inatoka Dar es salaam. Kauli hii inatia shaka kwa kuzingatia kuwa Dar ni sehemu ndogo tu katika nchi hivyo si sahihi kuwa inatoa asilimia zote hizo pekee, ukizingatia raslimali nyingi zipo sehemu nyingine ya nchi.
Naomba wenye uelewa wa hili watupe ufafanuzi, ni vigezo gani vinavyotumiwa kuthibitisha 80% ya mapato ya serikali yanatoka Dar.
Ufafanuzi huu ni muhimu kwani inaleta unyonge kwa mikoa mingine kuonekana si chochote katika uchumi wa taifa ili.

Wanaweza wawe sahihi na pia wasiwe sahihi.On paper Dar inaonekana kuwa mji ulio busy sana kibiashara kuliko miji mingine hapa nchini,In reality miji kama ya Arusha,Shinyanga,Mwanza,nk ndiyo iliyopaswa kuwa wachangiaji wakubwa wa kodi na shughuli nyingine nyingi za maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania isipokuwa mfumo wa centralized government umeigeuza hii Miji yenye rasilimali nyingi kuwa sehemu ya mavuno ya hizi rasilimali na kisha kupelekwa Dar wanakoamini kwamba ndiyo kila kitu.Angalia nchi kama USA ambayo inafuata mfumo wa decentralized government Jimbo lenye rasilimali nyingi kama California ndilo linaloongoza kwa kuchangia sana katika shughuli za maendele za nchi hiyo badala ya jimbo la New York ambao ndilo jiji maarufu la kibiashara kule USA.
 
Nimekuelewa vizuri mkuu, sasa kwa hali hii viongozi hawakupaswa kutumia kauli hii kama kigezo cha Dar kupewa kipaumbele kwenye maendeleo ya miundombinu kama wanavyodai sasa.
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,699
2,000
Viongozi Wanakosea wanavyosema hivyo si kweli kwamba mapato 80% yanatoka dar,kwanza Dar hawazalishi mazao yoyote,pili ofisi nyingi za serikali zipo dsm kwahyo transactions hata za watu wa mkoa sometime wanafanyia dsm hiki kitu nyerere alikuwa akitaki katika azimio la arusha alikuwa anapigania maendeleo yawe sawa sehemu zote sio fursa zote ziwe dar mfano barabara za juu wanataka kujenga dar,treni za juu dsm!! Dar ishakuwa jiji la hovyo waendeleze kibaha/chalinze/mdaula/ubena zomozi kabla hazijaelemewa.
 
Endeleaaa

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,391
2,000
Hapo ndo unaona umuhimu wa mfumo wa serikali za Majimbo. Inakuwa rahisi kupima kiuhalisia mapato na matumizi ya kila eneo la nchi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom