Ukweli kuhusu 50 cent kupiga picha na Jakaya Kikwete

NEW NOEL

JF-Expert Member
May 21, 2011
863
407
Ukweli ni kuwa JK alikutana na 50 cent katika mkutano wa UN wa ''every woman,every child milenium Development Goals'' na kama ambavyo 50 cent ameanzisha taasisi ya kusaidia tatizo la njaa kwa watoto Afrika. Kwa hiyo nadhani ilikuwa ni kukutana kwao tu,ndio kulipelekea kupiga kwao picha ya pamoja. Na 50 cent alipost picha hiyo katika account yake ya twitter.
Zaidi tembelea www.raprid.com
 
Sasa Mpwa sijakuelewa au labda kwasababu natumia simu; title unasema "UKWELI" halafu katikati ya thread yako unasema "UNADHANI" sasa sijui kipi ni kipi! Naomba ujaribu kuweka mambo sawa ili na wewe usilitet maswali mengi kuliko majibu, asante kwa kunielewa Mpwa, vipi wamekupa bei gani
 
Kudhani na ukweli ni maneno mawili yenye maana tofauti kabisa huwezi kuwa unadhani na muda huo huo uka-claim kuwa unachodhani ndio ukweli! karibu thupu
 
Umetumwa na nani? 50%, Silva Rweyemamu? Philemon Luhanjo? Waziri wa Chakula? Wziri wa Sera? Ww ni Premi?
 
Mwaka huu mbona kama vile umekua mrefu kwa CCM? SIJUI hapo tarehe tisa desemba itakuaje? Uhuru wa "Tanzania" utasherehekewa na Wageni kama 50 Cent na wengine kama 20 %
 
Sasa Mpwa sijakuelewa au labda kwasababu natumia simu; title unasema "UKWELI" halafu katikati ya thread yako unasema "UNADHANI" sasa sijui kipi ni kipi! Naomba ujaribu kuweka mambo sawa ili na wewe usilitet maswali mengi kuliko majibu, asante kwa kunielewa Mpwa, vipi wamekupa bei gani

mbona mnakaba mpaka penalti? Unajuwa kikwete ndio raisi wa mwisho kutokea ccm, cha msingi mtu kama huyu mleta mada tumshauri ajiandae kisaikolojia kushuhudia watanzania tukibadilisha chama tawala kwa amani. Na kama yeye ni mtumishi wa serikali basi hasiofi ajila yake itaendelea kama kawaida na zaidi ajila zitaongezwa zaidi serikalini.
 
Kwenye Huo mkutano walikuwa wawili tu?
50 Cent ndo pekee ana hiyo foundation ya kusaidia Barani africa?
Na ile aliyopiga na Boyz II men, nayo walikutana kwenye mkutano?
Lete utetezi mwingine mkuu!
 
Ukweli ni kuwa JK alikutana na 50 cent katika mkutano wa UN wa ''every woman,every child milenium Development Goals'' na kama ambavyo 50 cent ameanzisha taasisi ya kusaidia tatizo la njaa kwa watoto Afrika. Kwa hiyo nadhani ilikuwa ni kukutana kwao tu,ndio kulipelekea kupiga kwao picha ya pamoja. Na 50 cent alipost picha hiyo katika account yake ya twitter.
Zaidi tembelea www.raprid.com

ni rais gani mwingine wa Africa kapiga picha na 50?
Na alipopiga picha na Boyz ll Men unamteteaje? Na vp kuhusu mabembea ya Jamaika? Jakaya ja :bange:
 
Sasa Mpwa sijakuelewa au labda kwasababu natumia simu; title unasema "UKWELI" halafu katikati ya thread yako unasema "UNADHANI" sasa sijui kipi ni kipi! Naomba ujaribu kuweka mambo sawa ili na wewe usilitet maswali mengi kuliko majibu, asante kwa kunielewa Mpwa, vipi wamekupa bei gani

hawa ndio wametumwa na magambaz na wametengewa 600 mil. Kuiharibu JF
 
teh teh teh, Chama Cha Mafisadi mwaka huu hata muwanunulie watanzania wopte nyumba ya ghorofa tatu na kila mtu mumpe nissan murano ili kuwanyamazisha kwa uovu wenu, wala hatunyamazi,

m.kwere amechemka toka mwanzo kachemka tu hana cha kujitetea, karibu atapiga picha akiwa beach na watoto warembo anaogelea, ngoja tuone uozo wake
 
Back
Top Bottom