Ukweli: Kama Lowassa angekuwa rais, MCC wasingeweka pembeni faili la Tanzania

Mashine ya MRI sio kwamba nimbovu, model ya ile mashine ni ya Phillips ambayo hazitumiki tena duniani kwa techologia iliyopo kwa sasa. Ile mashine ni famba kwani inatumia Helium gas nyingi sana na ambayo ni shida sana kuisafirisha.

Hii gas huwezi kuisafirisha kwa ndege ni mpaka meli tu na ikifika hapa itakuwa nusu kwani ina react na humidity kubwa ya bahari.

Mama Nyoni alishauriwa wanunue mashine ya Siemen akakataa kwa kwasababu wahindi ambao ni maagent wa Phillips walikuwa wamemkatia dau kubwa sana ikabidi alazimishe mpaka muhimbili wakaipokea.

Kimsingi ile mashine haiwezi kutengamaa hata siku moja, suluhu nikununua nyingine mpya tu. Mpya ya Siemen ni $400,000 ambayo ni cheap kuliko kufanyia matengenezo hiyo iliyopo.

Kwanini mashine itengenezwe kwa Tzs 3 billion wakati tunaweza kununua nyingine 4 kwa hizo hela za matengenezo.

Naamini Kigwangala yuko huku, naomba ufuatili hii issue kiundani.
 
Msitishike na hiyo misaada ya kijinga. tujikite kukusanya kodi, hao akina OBAMA watatusikia tu kwenye bomba.

Kumbuka hata mtoto hazaliwi akatembea. tupunguze maneno ya wakosaji japo kidogo wakatu tukipewa kesho kwa vigezo vingine visivyotufunga tunapokea kwa mikono mnne
 
Ni kweli mkuu ila kumbuka ndo tunaanza na sehem ya huo msaada ungetuasidia sana kusogelea tunapokusudia.

LEO mnaona msaada ni mzuri, si mlisema JK ni ombaomba? Magufuli hataki ujinga huo na ndiyo maana haoni sababu ya kwenda kupiga magoti na kuamua kubaki na kuendelea kutumbua majipu. Akiyatumbua vizuri tutaisahau hiyo misaada ambayo leo mnaiona mizuri wakati ndiyo mliotumia kumtukania MKWERE.
 
Walikuwa wanamuunga mkono ili akishinda atengue mikataba ya gesi badala yake awape watu wa MCC ...alafu wao wanajiona wana demokrasia wakati wanataka favouritism kutoka kwa viongozi fulani, na Lowassa naye baadae angegeukwa na kufanywa kama akina C. Tayrol
 
Dawa za UKIMWI, DAWA ZA TB, DAWA ZA MALARIA, CHANJO ZOTE tunawategemea wazungu hivi wakisitisha hii misaada na wewe utapona?

Kweli una mawazo ya mbali sana na unaona mengi sana mkuu. hongera kwa michango yako. Nahisi kuna watanzania sasa wanaelekea kumfanya JPM nabii ama mtume.
 
LEO mnaona msaada ni mzuri, si mlisema JK ni ombaomba? Magufuli hataki ujinga huo na ndiyo maana haoni sababu ya kwenda kupiga magoti na kuamua kubaki na kuendelea kutumbua majipu. Akiyatumbua vizuri tutaisahau hiyo misaada ambayo leo mnaiona mizuri wakati ndiyo mliotumia kumtukania MKWERE.

Fwatilia habari achana na michapo ya vijiweni..hukumsikia Magufuli alivyoongea kwa bashsha wakati ule aliposikia marekani wana mpango wa kusaidia umeme vijijini?
 
ukishanyimwa unasonga mbele siyo mambo ya angekuwa fulani, ujinga huo. unajikombakomba nini?

Ndahani wewe hutaki kabisa ukweli na kikubwa kwako ni ushabiki wa kitoto, Tumenyimwa kwa sababu ambazo zingeweza kumalizika kidemokrsaia ila kwa sababu wewe na wenzako mmeibana , haya sasa haya ndo madhara yake. Nasisitiza tuache maneno ya wakosaji.
 
Kwasababu ni mwizi mwenzao na madini makubwa makubwa atawapa hao wageni.

hebu soma tena ulichoandika ina maana hata haya malalamiko ya wachimbaji wadogo kufukuzwa na maeneo kupewa wazungu huyajui?
Mbaya zaidi wazungu wamesamehewa kodi kwenye migidi yao
Almas..mwadui dhahabu..tanzanite aaaaaa acha hizo
 
kwa SABABU Marekani wangejua iko siku zitawarudia kwa mlango wa Nyuma? Sasa wataisoma namba. Msukuma siyo mjinga kama akina LOWASSA.

Asante kwa kutaja hilo jina kubwa. Ni kweli lina ring most of the bells, lingekua dawa lingeshakutibu siku nyingi. Na ngekua raisi tungeshapiga hii bingo toka jana. If you know the truth, speak out.
 
hebu soma tena ulichoandika ina maana hata haya malalamiko ya wachimbaji wadogo kufukuzwa na maeneo kupewa wazungu huyajui?
Mbaya zaidi wazungu wamesamehewa kodi kwenye migidi yao
Almas..mwadui dhahabu..tanzanite aaaaaa acha hizo

Kumbe tanzanzania kuna watu wanafwatilia habari za nchi yao..hongera sana mkuu
 
Tanzania yangu democrasia bado safari ndefu sana.

Ishu ya Zenji??? demokrasia sifuri, mama yangu, haya hii ya wale mashujaa wa IT wa UKAWA??? demokrasia sifuri pia. Na hizi ishu mbili tu, yaani mbili tu kwa mwenye kuelawa, ndo zimetunyima huo msaada, sasa tunabaki na maneno kibaaao ya wakosaji. Kweli mkuki kwa nguruwe mtamu sana ila kwa mtanzania ............................
 
Kwa sababu alisema madini makubwa makubwa atawapa wakubwa?

Haya mambo ya kusoma Uzi mstari wa kwanza na wa mwisho haya!

Hapana mkuu, hiyo si sababu ya msingi, jaribu ingine

kWELI KABISA. ila jambo jema ni kwamba tunkoelekea na kasi hii, hata hizo pesa za MCC hatutakuwa na haja nazo. Tumuunge mkono rais ili hawa Wazungu washike adabu. Wanatushia NYAU ili iweje.

Kweli mkuu, Hii ishu ya Zenji ni moja ya sababu ya Tz kukosa huo msaada mnono

kwa SABABU Marekani wangejua iko siku zitawarudia kwa mlango wa Nyuma? Sasa wataisoma namba. Msukuma siyo mjinga kama akina LOWASSA.

Kwasababu ni mwizi mwenzao na madini makubwa makubwa atawapa hao wageni.

Tatizo la huyu anayejipambanua kwa jina la mzee wetu Mandela "Tatamadiba" hana hekima wala Busara hata kidogo ndiyo maana kila kitu anakijadili zaidi ki-CCM.
Tatizo ni Ulevi wa CCM ndicho kinacho wachanganya hawa akina Simiyu yetu na Lizaboni pamoja na Tatamadiba.

Hapa hoja ni kwamba MCC imezuwia pesa kwa kushindwa kutimiza masharti ya Democracy ikiwa ni pamoja na kitendo cha kunyang'anya Ushindi wa CUF bila sababu yeyote.
Pili kitendo cha kukamatwa kwa vijana wa Chadema na kituo cha Sheria cha Haki za binadamu LHRC na kuharibu Computer zao.

Tanzania inahitaji sana Nchi za Magharibi kuendelea. Sisi hatuzalishi kitu chochote hapa sasa tukijifanya kichwa ngumu tutakuwa kwenye wakati mgumu sana.
 
Ishu ya Zenji??? demokrasia sifuri, mama yangu, haya hii ya wale mashujaa wa IT wa UKAWA??? demokrasia sifuri pia. Na hizi ishu mbili tu, yaani mbili tu kwa mwenye kuelawa, ndo zimetunyima huo msaada, sasa tunabaki na maneno kibaaao ya wakosaji. Kweli mkuki kwa nguruwe mtamu sana ila kwa mtanzania ............................

Na sasa hivi kinachoendelea ni ubabeubabe tu.
 
...bila jitihada hizi za kamata mwizi na mguu pande, hata huo msaada wa MCC tusingeona faida yake maana ungeishia kubakwa na wachache...so it is a win win situation if you ask me
 
Labda niulize maana kulikuwa na hujuma nyingi sana za teamLowasa.

Lowasa angeshika tungepewa kwa kuwa mkurugenzi MKUU wa huo mfuko wa MCC kwa Tanzania ni Bernard MCHOMVU toka KILIMANJARO labda naye alikuwa team Lowasa? au unataka kusema nini? Sijakuelewa

Sasa kwa kuwa Lowasa hajapata kwa hiyo mnamtumia Mchomvu kuchonga tusipate au nini?

Mnalipa kisasi cha kushindwa au ni nini?
 
tutashabikia weee, tutajifanya wajuaji weee, tutatoa mapovu weee, tutajufariji weee, tutatofautiana weee, lakini ifike mahala nyeusi tuiite nyeusi na nyeupe tuiite nyeipe.

Ukweli kabisa tanzania tunahitaji kujitegemea nak tunahitaji kabisa kuwa among the doner countries lakini bado tuna safari ndefu, bado inayohitaji hekima, mikakati na elimu ya kutosha ya uchumi wa kujitegemea.

Kuota ndoto usiku na kukurupuka asubuhi kusema we are going to be the doner country itatusaidia tu kujaza kurasa humu za kusifiana na kujazana vichwa, lakini itabaki nadharia bila kuwa kabisa na clear vision na objectives hatutaamka tu asubuhi tukajikuta tunajitegemea.

Hebu jiulize machine mbili tu za mri na ct scan zimeihenyesha serikali imeshindwa kulipa billion saba zinazodaiwa tatizo likafumbuliwa au kununua nyingine mpya kila siku ni kurepea repea viraka alafu unataka ufukuze watendaji!

Turudi kwenye mada sasa! Kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa ni kweli kwamba swala la zanzbar limechelewa sana na inahitajika mtu ambaye kweli amejaa hekima na busara kuweza kulimaliza mi simuoni mwingine kwa sasa zaidi ya mh lowasa... Na hapa tutamkumbuka sana pamoja na ushabiki wetu. Hivi niwaulize swali?

Juzi si tulimuona mwigulu kule morogoro na vyombo vya habari kwenye mgogogoro wa wakulima na wafugaji? Alipoondoka tu kesho yake watu ishirini na mbili walifyekwa mapanga na mikuki je alirudi tena? Na je tatizo limeisha?

Hii nchi bado haiwezi kujitegemea kwa sasa iko kwenye kujenga misingi ya kujitegemea misaada ikikatwa moja kwa moja hakuna rangi mtaacha kuona.. "maisha ni hatua huwezi kusimama kabla huja kaa" kufanya mambo kibabe tukidhani tayari tunaweza, itawaumiza hasa wale ambao mvua isiponyesha serikali inatakiwa iwe na chakula cha kutosha kwenye ghala cha kuwasaidia sio kuwapa kopo tano unaita media tumetoa misaada ya njaa.

Mtu ambaye mshahara wake ni zaidi ya million 36 na anazipewa baada ya miaka mitano ya kazi hata akiharibu hatoathirika sana.

Tanzania ni yetu sote twende mbele turudi nyuma, wa ccm kaolewa na wa ukawa, wa bara kaolewa na wa visiwani lolote likitokea wote ni wahanga.

Sijui kwanini nawaza sana juu ya hatma ya tanzania..kila ukidhani mnapiga hatua kumbe indirect mnarudi nyingine kumi lakini mtanzania aliyeitwa kichwa cha mwendawazimu hataki kushirikisha ubongo amebaki kucheka tu na kushabikia kila kitu.
lowasa nilimsapoti bt nmekuja kugundua kuwa nilikua wrong kiukweli asingeweza kuwadhibiti wafanyabiashara wakubwa ambao wana interest kwenye migodi ambao wana interest kwenye migodi yote mikubwa ambao ndio wakwepa kodi wakuu ..nanukuu maneno ya mheshimiwa rais magufuli siku alipoongea na wafanyabiashara akimweeleza deo mwanyika ambaye ni mwakilishi wa migodi ya barick iliyobadili jina na kujiita accacia ili kukwepa kuanza kulipa kodi nanukuu'' mwanyika kuna zile ndege zinazorukaruka kule kwenu bila kulipa kodi yetu kuwa makini naskia nyie wahehe mambo yakiharibika huwa mnajinyonga" mwisho wa kumnukuu mheshimiwa rais ukweli ni kwamba migodi mikubwa madini yanatoroshwa sana na hayalipiwi kodi ata mtoto mchanga wa geita..mara..shinyanga ...arusha anajua...hivyo ili eneo limulikwe kwa macho kumi mheshimiwa rais ...bandari na migodi pameoza bila kusahau mikataba ya gesi...tuna imani na mheshimiwa rais magufuli
 
Labda niulize maana kulikuwa na hujuma nyingi sana za teamLowasa.

Lowasa angeshika tungepewa kwa kuwa mkurugenzi MKUU wa huo mfuko wa MCC kwa Tanzania ni Bernard MCHOMVU toka KILIMANJARO labda naye alikuwa team Lowasa? au unataka kusema nini? Sijakuelewa

Sasa kwa kuwa Lowasa hajapata kwa hiyo mnamtumia Mchomvu kuchonga tusipate au nini?

Mnalipa kisasi cha kushindwa au ni nini?

Sijui kama unauelewa kiasi gani wa neno tuhuma
 
Back
Top Bottom