Ukweli juu ya nafsi(roho) kuendelea kuishi baada ya kufa kwa mujibu wa biblia

Mwanzo 2:7

BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Ukiangalia ;

Mwanzo 1:27

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Mungu alianza kuumba roho , baada ya roho tunaona Mungu akafanya mwili wa mavumbi sasa, baadae Mungu akapulizia pumzi ya uhai, tunaona mtu akawa nafsi hai . Nafsi ni matokea ya Mwili na Roho kuwa na puzmia ya uhai ndio ikaja nafsi kwa kugha nyepesi kuna ufufuno wa nafsi baada ya hiyo acts. Ila tunaona mtu akifa, mwili hurudi mavumbini, roho na nafsi hutoki, vinaenda palipo na ( roho iliyokuwa iki zi control ), kama Roho Mtakatifu basi vitaenda paradise na kama roho zidanganyazo basi itaenda kwa hizo roho zidanganyazo. Nafai ni muhimu sana, dunia itakufaidi nini kama ukapata kila kitu ila nafsi ikaenda motoni
Hakuna roho inayoendelea kuishi mtu akifa. Kwanza roho ya binadamu ni ile pumzi yake. Neno roho kwa kigiriki inaitwa pneuma ikimaanisha pumzi. Hilo ndilo limezaa neno pneumonia/nimonia.
 
Nafsi ni mtu mwenyewe. Siyo kitu kilicho ndani ya mtu. Na hata tunaposoma kiswahili utasikia nafsi ya kwanza umoja au nafsi ya pili wingi. Soma mwanzo sura ya 2 mstari wa 7 ujue kuwa binadamu mwenyewe ni nafsi.

Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Pia si sahihi kusema kuwa Nafsi ya mtu haifi. Biblia kwenye Ezekiel 18: 20 inasema kuwa nafsi inayotenda dhambi itakufa.

The soul who sins shall die. The son shall not suffer for the iniquity of the father, nor the father suffer for the iniquity of the son. The righteousness of the righteous shall be upon himself, and the wickedness of the wicked shall be upon himself.

Berean Study Bible
The soul who sins is the one who will die. A son will not bear the iniquity of his father, and a father will not bear the iniquity of his son. The righteousness of the righteous man will fall upon him, and the wickedness of the wicked man will fall upon him.

King James Bible
The soul that sinneth, it shall die. The son shall not bear the iniquity of the father, neither shall the father bear the iniquity of the son: the righteousness of the righteous shall be upon him, and the wickedness of the wicked shall be upon him.
 
So mchizi aliyekufa kabla ya yesu na yeye bado anangojea ufufua mpaka leo mika elf 2 na kedekede!!? Nikifika hapa nakua mzito kumini hizi ngano! Kuna akina daud nao wanangojea ufufua sijui ni mika elf ngapi mpaka sasa!! Acha nijipitie kushoto tu
yaani hapo Hata Mimi ndio huwa naona kuwa masimulizi ya dini Ni esopo
 
So mchizi aliyekufa kabla ya yesu na yeye bado anangojea ufufua mpaka leo mika elf 2 na kedekede!!? Nikifika hapa nakua mzito kumini hizi ngano! Kuna akina daud nao wanangojea ufufua sijui ni mika elf ngapi mpaka sasa!! Acha nijipitie kushoto tu
Nimecheka Sana
 
Nakubakiana na wewe kabisa. Lakini bado kuna "utata" katika hilo jambo la kifo.
Hebu niambie kuhusu maneno ya YESU kuhusu yule Lazaro maskini na yule tajiri, nini kiliwatokea au kuwakuta baada ya kufa?
Soma LUKA 16:19-30.
Nitazungumza kwa kadri ya hekima niliyojaaliwa kulielewa somo hili ambalo ni mfano wenye mafumbo ndani yake uliotolewa na Yesu ukitulenga sisi kama walengwa:

19. Akasema palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula siku zote kwa anasa.

Rejea: Mt 16:24-25 "Mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate, kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakaye poteza nafsi kwa ajili yangu ataiona.

* tafsiri yake; ukichagua ya dunia ina maana umechagua matamanio ya nafsi yako mwenyewe na kamwe uwezi pata kibali machoni mwa Bwana.

20. Na maskini mmoja, jina lake lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi.

*Nae analo hitaji lake au kiu aitakayo umtimizie uketi malangoni kwako kila siku akibisha hodi umkaribishe lakini nafsi yako imekuwa ikimtonesha mara kwa mara kwa ukaidi wako.

21.Naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri, hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.

Rejea: Mathayo 5:3-12 Heri walio masikini wa Roho maana ufalme wa mbinguni ni wao.
* tafsiri; heri walitafutao neno la Mungu au wenye kiu ya kujua na mwishowe ni kuishika iliyo hekima.

22.Ikiwa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika kifuani kwa ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa.

Rejea; Ufunuo 3:17-18 kwa kuwa wasema, mimi ni tajiri, nimejitajirisha wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge na mwenyewe mashaka,na masikini na kipofu na uchi.."

tafsiri; sawa na neno lake uza au acha vyote kisha nifuate mimi, jitunzie hazina yako mbinguni.

23. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake,alipokuwa katika mateso, akamwona ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kwa mbali,na Lazaro kifuani mwake.

Ibrahimu= Baba wa mataifa na imani, agano la mwanadamu na Mungu,kukubali kumtoa mwanae wa pekee kama dhabihu sawa na mfano wa Mwenyezi Mungu kwa mwanae Yesu.Yak.(KM)4:5 waaminifu pia hufanyika kwa uzao wa Ibrahimu (Gal.3:27-28)
-Bila shaka mfano huu umemtumia Ibrahimu kumwakilisha Mungu.

Lazaro- kielelezo cha mtiifu kwa Mungu/neno la Mungu/Yesu.

24. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

* Nafsi yenye dhambi (ikiwakilishwa na tajiri) itakapojuta nakutamani kutubu lakini haitowezekana.

25.Ibrahimu akasema, mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mema yako katika maisha yako, na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa na wewe unaumizwa.

*Kumbuka alikufa msalabani ili wewe ukombolewe lakini ukutambua wakati uliyo sahihi kwako.

26.Na zaidi ya hayo; kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutokana huku kwenda kwenu wasivuke kuja kwetu.

*Watendao uovu na machukizo hawana mahali pao kabisa katika ufalme wake Mwenyezi Mungu bali katika ziwa la moto na kamwe hawatokuwa sawa na wateule wa mwanakondoo.

27.Akasema, Basi, Baba,nakuomba, umtume nyumbani kwa Baba yangu,

28.kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali pa mateso.

*Mfano unamzungumzia roho mtakatifu toka kwa wamchao Mungu ukiwaombea wakosaji wapate wokovu hili wakiepuke kikombe cha ghadhabu yake Bwana.

29.Ibrahimu akasema, wanao musa na manabii, na wawasikilize wao,

*Naye Mungu akayajibu maombi yao kwa kuwajulisha kuwa tiyari wanalo neno langu nililowapa kupitia kwa manabii wangu wawasikilize na wapate kupona.

30. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.

*Sauti ya wenye haki ikaendelea kuwatetea wakosefu hili wapate nafasi ya kujisahihisha; wakiamini kuwa wakosefu wana mioyo migumu hivyo imempasa Mungu kumtuma mtu atakaye wahubiri na kufa kwa ajili yao na kufufuka wenda wataamini na kukombolewa.

31.Akamwambia, wasipowasikia musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.

*Hivyo hapa Yesu anadhihirisha juu ya uhakika wa neno la Mungu na unabii wake kuwa u hakika tupu toka kizazi hata kizazi na ya kwamba kama hamkuamini manabii wa Mungu toka kipindi cha mwanzo hata yeye pamoja na kufa kwake msalabani na kufufuka bado hamtomwamini nakufata mafundisho yake.
 
Ume

Umeandika gazeti, lakini, bado hujajibu swali langu.
 
Nimelijibu kwa ufasaha kabisa, mfano huu hauna mahusiano yeyote na kitendo cha mtu kufa na kuendelea kuishi; Lazaro ni kiwakilishi cha Neno au Yesu, Kifo kimetumika kuwakilisha kufa na kufufuka kwake na kutoka hapo ataenda mahali pa babaye yaani kifuani kwa Ibrahimu. Na akaendelea kumzungumzia tajiri(wakosefu) katika nyakati za hukumu ambapo roho zilizoshindwa kumkana shetani zitachomwa moto ndipo watajuta nakutamani wokovu nyakati hizo pasina mafanikio.

Hivyo anaenda mbali zaidi nakuchomekea kisa cha yeye kuja duniani kama mbadala wa manabii waliotumwa mwanzo lakini atukuwasikiliza kwahiyo anaonesha jinsi alivyotupigania kwa Baba yake wakati anaomba ruhusa ya kuja kutukomboa, akawa anaulizwa kama walishindwa kuwasikiliza akina musa na manabii waliokutangulia unadhani hata ukifa na kufufuka watakuamini, watakusikia na kupokea toba?

Hivyo ikiwa hadithi hii inagusia stori nzima juu ya ujio wa Yesu, lengo na hitimisho lake(yaani siku ya hukumu) hili uitumie kama mfano wa kuthibitisha hoja yako ya kutokufa kwa roho basi fatisha hadithi nzima ya maisha yake duniani mpaka kifo chake na utokuwa na swali tena.

(kumbuka yesu aliwajulisha wanafunzi wake mara kadhaa juu ya kifo chake lakini hawakuelewa kama alijizungumzia mpaka nyakati za mwisho ndipo alianza kuwafasiria)
 
Mungu alipuliza pumzi ya uhai mana ke oxygen. Pamoja na Hydrogen =H,0 Maji.

Mwili wa mtu asilimia 90 ni maji. Na roho wa Mungu alitulia juu ya vilindi vya maji.

Na maji huenda juu by means of evaporation then yana kuja km mvua. Kwa hiyo mtu ni maji na upepo.

Ukikosa maji au hewa ya oxygen una kufa.

Mtu ni upepo tu yaani hewa hii ukifa tunakuvuta ili tuishi. Ukivutiwa ulaya unakuwa mzungu.africa magharibi unakuwa m cameroon.tena una zaliwa huko.

Mungu ni upepo yuko kila mahali
 
"Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula mpaka ushibe. Lakini kuhusu matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula,utakufa hakika" (mwanzo 2:16,17)

Lakini je kuna sehemu fulani ya mwanadamu inayoendelea kuishi baada ya mtu kufa?

Biblia inasema "Mungu hawezi kamwe kusema uongo" (waebrania 6:18) ukweli ni kwamba shetani ndiye alisema uongo alipomwambia Hawa hivi "Hakika hamtakufa" mwanzo 3:4.

Hivyo basi swali ni; ikiwa fundisho la kutokufa kwa nafsi ni uongo ni nini hutokea mtu anapokufa?

"Yehova Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi ya nchi na kupuliza katika mianzi ya pua yake pumzi ya uhai,naye mtu akawa nafsi hai" usemi "nafsi hai" unatokana na neno la kiebrania ne'phesh, likimaanisha kiumbe anayepumua.Mwanzo2:7

Hivyo biblia haielezei kuwa mwanadamu hakuumbwa akiwa na "nafsi isiyoweza kufa" badala yake ni "nafsi hai"

Ni kina nani basi walioleta fundisho la nafsi kutokufa kama siyo Mungu mwenyewe?

Wamisri walikuwa kikundi cha kwanza,wakifuatiwa na wababiloni na wagiriki walioeneza mafundisho hayo kuenea katika himaya nzima ya ugiriki katika mwaka wa utawala wa Aleksanda Mkuu 332W.K,

Baadae madhehebu ya kiyahudi ya waesene na mafarisayo, yalianza kufundisha kutokufa kwa nafsi kwa kupokea mawazo ya Plato" ilikuwa rahisi kuunganisha falsafa ya Plato na ukristo sababu ya nadharia ya Plato kwamba mwanzoni nafsi zetu zilikuwa mahali pazuri na sasa zinaishi ulimwengu uliopotoka"

Mtume Paulo analiongeleaje,"...vipindi vya nyakati za mwisho wengine wataanguka kutoka kwenye imani, wakisikiliza maneno yaliyoongozwa kwa roho yenye kupotosha na mafundisho ya roho waovu"(1Timotheo 4:1) Hivyo basi biblia haiungi mkono fundisho hilo na chanzo chake ni falsafa na dini za kale za kipagani.

Yesu anasema" Nanyi mtaijua kweli, nayo kweli itawaweka ninyi huru" (Yohana 8:32)
Yesu kristo alisali hivi kwa Mungu; "uzima wa milele ndio huu, waendelee kupata ujuzi juu yako wewe, Mungu wa pekee wa kweli na juu ya yule uliyemtuma,yesu kristo"

Je wafu wako wapi? Wafu wako kaburini wakingojea ufufuo (Yohana) hawateseki au kuhisi maumivu yoyote, kwa sababu "wafu hawajui lolote kamwe" (mhubiri 9:5)-(mhubiri 9:10) hata hivyo, kupitia ufufuo, Mungu atakishinda kifo milele. 1 Wakorintho 15:24,55;ufunuo 21:4
Kauli tata; ijapokuwa mwili hurudi udongoni, roho humrudia Mungu.(Mh.12:7)

Utatuzi wake; kufuatana na sulemani, katika kifo, hakuna tofauti ya roho za wanyama na za wanadamu, wote huenda pamoja (mh.3:19-21). Anachomaanisha kuwa kinamrudia Mungu ni ile cheche ya uhai (mwa.2:7)

Imani ya kuongea na wafu(spiritualism) ikiwa wafu hawana ufahamu, je wanaongea huwa na akina nani?

Imani ya kuongea na wafu imeanzia kwenye uongo wa awali wa shetani kwa Hawa."Hakika hamtakufa"(mwa.3:4) Maneno hayo yalikuwa hubiri la kwanza (linaloendelea hivi sasa) juu ya kutokufa kwa roho(nafsi)

Roho itendayo dhambi itakufa(Eze.18:20)imebadilishwa kimtizamo kuwa "roho hata ikitenda dhambi itaendelea kuishi milele"

Hivyo utamaduni wa mafundisho haya umejenga imani yenye dhana yakubatilisha ukweli nakutimiliza matakwa ya shetani. Na kila haaminiye nakutimiliza matendo yakiimani katika njia hii ujinasibu mwishoni kuwa yu mungu au mwenye nguvu juu yake mwenyewe zakuumba nakuponya kujua kabla na baada ya,kutoa na kutwaa nakujitukuza mwenyewe sawa na ahadi ya babaye shetani "mtakuwa kama miungu"(Mwa.3:5)
Huu ni Upotoshaji ambaoni mwepesi sana kudeal nao.Umetumia Scripture reference nyingi ambazo lengo lako ni kufanya andiko lako lionekane ligit lakini unfortunately haziendani article yenyewe.

Mungu wakati anamuumba mwanadamu mpango wake ulikuwa mwanadamu aishi milele katika mwili usioharibika.Baada ya mwanadamu kutenda dhambi ndipo kifo cha mwili kikaingia duniani.Hiki kifo tunachokizungumzia hapa ni roho kuacha mwili sio roho(spirit) kufa.

Kwa sababu Mungu anampenda sana mwanadamu tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu alishaweka mpango wa kumpatia tena mwanadamu ule uzima wa milele alioudhamiria hapo awali.Hapo ndipo Yesu Kristu anapoingia sasa.Na ufufuko wa Yesu umekuja na tumaini la ufufuko wa wafu (miili) ambao tutapewa miili mipya isiyoharibika.(lengo likiwa ni kutupatia ukamilifu tuliokuwa nao awali ambao Mungu alikuwa ameudhamiria.

My point hapa ni kwamba Roho kamwe haifi kwa maana ya kuacha kuexist.Roho ni Eternal.Mwili ndio unaoharibika na baada ya ufufuko tutapata mwili mpya usioharibika.
Kwenye biblia mahala popote walipozungumzia roho kufa walikuwa wanazungumzia hali ya kutengana na Mungu sio kuacha kuexist.

Note;Though Roho(Spirit) na Nafsi(Soul) ni vitu viwili tofauti most of the time haya maneno yanatumika interchengably kwa sbabu huwa vina kwenda pamoja,hazitengani.
 
Mwanadamu mpaka lini utaendelea kuwa na moyo mgumu kwa kupingana na neno la Mungu?

Kinachotusumbua siku zote wanadamu ni ile tamaa yetu yakutaka kuiforce akili yetu iamini kuwa atutokufa kamwe ili tujipe moyo na matumaini kabla yakuonja mauti.

Ukweli mchungu ni kuwa ukifa na biashara yako imeisha, hivyo vifungu vyote nimevitoa kwenye biblia nasijajitungia au kuvigushi kujustify madai yangu.

Kwa mara ya kwanza ulipewa uhai ukaukataa nakuchagua kifo ukiaidiwa na shetani aliyekudanganya kuwa utajua kila kitu nakuishi milele (uongo anaozidi kukuaminisha mpaka waleo), kwa kuwa Mungu akiahidi jambo uwa atendi tofauti kweli ahadi yake ya kifo ikawa implemented kama alivyoahidi tukienda kinyume na sheria yake.

Ni kweli ulivyoeleza kuwa hayakuwa makusudio ya Mungu kwa mwanadamu kufa bali kuishi milele hivyo kurejesha agano hili mwanadamu alipewa second chance kujirekebisha kwa kufuata sheria

ya Mungu kwa ukamilifu hili baada ya adhabu ya kifo mwanadamu arejeshewe pumzi ya uhai tena kupitia ufufuo (ambayo kwa mujibu wa maandiko roho hii urejea punde kwa Muumba mara tu unapokufa na wewe habari yako inakuwa imeishia hapo mavumbini)

Kwa mara ya kwanza wafu('watu wasiotambua chochote kile kinachoendelea wala awana sehemu yao katika wale walio hai' kwa mujibu wa biblia) watafufuliwa(watarejeshewa pumzi na kuzinduka mfano wa waliotoka usingizini walipokuwa wamelala

hawajitambui) atakapo rudi Yesu Kristo kuchukua walio wake, hakuna narudia tena hakuna mahali bible imezungumzia reincarnation kama kuna hicho kifungu basi kilete tubishane kwa vifungu nipo tiyari.
 
Mungu alipuliza pumzi ya uhai mana ke oxygen. Pamoja na Hydrogen =H,0 Maji.

Mwili wa mtu asilimia 90 ni maji. Na roho wa Mungu alitulia juu ya vilindi vya maji.

Na maji huenda juu by means of evaporation then yana kuja km mvua. Kwa hiyo mtu ni maji na upepo.

Ukikosa maji au hewa ya oxygen una kufa.

Mtu ni upepo tu yaani hewa hii ukifa tunakuvuta ili tuishi. Ukivutiwa ulaya unakuwa mzungu.africa magharibi unakuwa m cameroon.tena una zaliwa huko.

Mungu ni upepo yuko kila mahali
Hizi ni mambo za mafundisho ya siri na ya wale wanaojinasibisha na universe laws ni mambo yaku-assume nakujitungua kulingana na fahamu zetu tu ambayo pia ni kinyume kabisa na mafundisho ya biblia.
 
Mimi ni mkristo tena kindaki ndaki,lakini hua nina kigugumizi kikubwa sana ya story za maisha badala ya kifo, binafsi ninahisi na kuona wazi kwamba:-

1. Hakuna maisha baada ya kifo zaidi ya kutishana ili tustaarabiane hapa Duniani

2. Hakuna moto wa milele hata kidogo,nao ni uongo ili watu tustaarabiane tusilipe visasi na kutenda mabaya

3. Kwa mbaaaali nakua naamini yamkini baada ya kifo uhai huhamia kwenye kasha jingine lenye limezaliwa punde

4. Hakuna mwisho wa dunia isipokua pale tu mtu anapokufa
Ni vyema ukaamini kuwa Mola yupo uende umkose kuliko kutokuamini hayupo alafu uende umkute, itakuwa ni kilio na kusaga meno
 
Nafsi ni mtu mwenyewe. Siyo kitu kilicho ndani ya mtu. Na hata tunaposoma kiswahili utasikia nafsi ya kwanza umoja au nafsi ya pili wingi. Soma mwanzo sura ya 2 mstari wa 7 ujue kuwa binadamu mwenyewe ni nafsi.

Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

Pia si sahihi kusema kuwa Nafsi ya mtu haifi. Biblia kwenye Ezekiel 18: 20 inasema kuwa nafsi inayotenda dhambi itakufa.

The soul who sins shall die. The son shall not suffer for the iniquity of the father, nor the father suffer for the iniquity of the son. The righteousness of the righteous shall be upon himself, and the wickedness of the wicked shall be upon himself.
Mwanadamu mpaka lini utaendelea kuwa na moyo mgumu kwa kupingana na neno la Mungu?

Kinachotusumbua siku zote wanadamu ni ile tamaa yetu yakutaka kuiforce akili yetu iamini kuwa atutokufa kamwe ili tujipe moyo na matumaini kabla yakuonja mauti.

Ukweli mchungu ni kuwa ukifa na biashara yako imeisha, hivyo vifungu vyote nimevitoa kwenye biblia nasijajitungia au kuvigushi kujustify madai yangu.

Kwa mara ya kwanza ulipewa uhai ukaukataa nakuchagua kifo ukiaidiwa na shetani aliyekudanganya kuwa utajua kila kitu nakuishi milele (uongo anaozidi kukuaminisha mpaka waleo), kwa kuwa Mungu akiahidi jambo uwa atendi tofauti kweli ahadi yake ya kifo ikawa implemented kama alivyoahidi tukienda kinyume na sheria yake.

Ni kweli ulivyoeleza kuwa hayakuwa makusudio ya Mungu kwa mwanadamu kufa bali kuishi milele hivyo kurejesha agano hili mwanadamu alipewa second chance kujirekebisha kwa kufuata sheria

ya Mungu kwa ukamilifu hili baada ya adhabu ya kifo mwanadamu arejeshewe pumzi ya uhai tena kupitia ufufuo (ambayo kwa mujibu wa maandiko roho hii urejea punde kwa Muumba mara tu unapokufa na wewe habari yako inakuwa imeishia hapo mavumbini)

Kwa mara ya kwanza wafu('watu wasiotambua chochote kile kinachoendelea wala awana sehemu yao katika wale walio hai' kwa mujibu wa biblia) watafufuliwa(watarejeshewa pumzi na kuzinduka mfano wa waliotoka usingizini walipokuwa wamelala

hawajitambui) atakapo rudi Yesu Kristo kuchukua walio wake, hakuna narudia tena hakuna mahali bible imezungumzia reincarnation kama kuna hicho kifungu basi kilete tubishane kwa vifungu nipo tiyari.
Kaka mi nadhani we mwenyewe hujui unaandika kitu gani,mi natambua kufa kupo na wala sijabisha kuhusu hilo.

Kifo kipo cha namna mbili
Aina ya kwanza ni kifo cha mwili ambacho kila mtu atapitia na aina ya pili ni kifo cha kiroho ambacho ni kutengana na Mungu.

Believers wanapokufa mara moja roho zao zinakwenda mbinguni wakati wakisubiri hukumu ya mwisho(hukumu hii sio ya kuamua uende mbinguni au motoni ni ile ya kukupimia kiwango cha malipo unayostahili kupewa). Kibiblia hawa wanatambulika wamekufa kimwili lakini roho zao bado zinaishi kwa kuwa hawajatenganisha na Mungu.

Unbelievers once wanapokufa roho zao zinakwenda hell right away. Zikisubiri siku ya hukumu ambapo haitakuwa kwa ajili ya kuamua nani aende mbinguni au lah bali itakuwa ni ya kupimiwa ni kiwango gani cha msoto wanastahili.Kibiblia hawa wanatambulika kuwa wamekufa kwa sababu wametengenishwa na Mungu milele au tunaweza sema roho zao zimetenganishwa na Mungu milele.

Kwa hiyo kaka sihitaji kuweka reference nyingi sana kukuonyesha haya.Roho inaishi milele.Baada ya mwanadamu kuondoka duniani ikiishi pamoja na Mungu tunasema iko hai ila ikitenganishwa na Mungu kwa maana ya waliokwenda hell tunasema imekufa.Na ndipo palipo na mateso ya milele.

Yesu aliposhuka kuzimu baada ya kifo chake alikwenda kuwapa nafasi wale wote waliokufa kabla ya kifo chake wakiwa na tumaini la ufufuko.Watu hawa walimwamini Mungu na kuzishika amri zake lakini hawakuwa wamehesabiwa haki mpaka damu ya Yesu ilipoenda kuwafanya wawe righteous machoni pa Mungu.Kundi hili ni pamoja na akina Abrahamu na wengine. Lakini watu waaminio waliokufa baada ya Yesu kufufuka wote wanakwenda mbinguni moja kwa moja hawasubiri katika upweke wala mateso tena kwa sababu wamehesabiwa haki kwa damu ya Yesu tayari.

Kama ni msomaji mzuri nadhani unakumbuka Saul alipojaribu kutumia nguvu za kiroho zisizompendeza Mungu kujaribu kuzumgumza na Samweli aliyekuwa amekwisha kufa.Samweli hakuwa mbinguni na wala hakuwa hell kwa sababu alikuwa amekufa akiwa na tumaini la ufufuko lakini hakuwa amehesabiwa haki na Mungu bado kwa sababu damu ya Yesu peke yake ndo yenye uwezo wa kutufanya tuhesabjwe haki na mpaka wakati huo Yesu alikuwa hajafa bado.

I believe kifo kipo.Bali roho inaishi milele.Pumzi inayozungumziwa ndo hiyo Spirit (Roho).
 
Kuna kifo cha aina mbili...blaa!..blaa!..blaa! Nadhani unatumia hisia na ufahamu wako binafsi ila siyo biblia.

Watu wema na waovu hufa mara moja na hakika(Kifo hakina matabaka kwani wafu wote huwa sawa pindi wakishakufikwa na mauti), ROHO au PUMZI YA UHAI ni Mali ya MUNGU

(Uhai aliokupa umetoka ndani yake yeye aliyekuumba hivyo hawezi kujiua yeye mwenyewe bali ukupa ukomo wa matumizi ya uhai huo ndani ya mwili alokupatia,

Hivyo baada ya kuufinyanga udongo ule siku ile alikupulizia pumzi yake ukawa NAFSI hai(yaani ukawa na ufahamu kuwa u hai na ni kiumbe)) na pindi unapokufa roho ile umrudia mmiliki wake, mwili hurudi mavumbini na aliyekufa kwa mujibu wa maandiko hajui chochote kile wala kuhisi chochote.

Muda wa mtu kuamua maisha ya after life duniani ni kile kipindi hakiwa NAFSI(kipindi akiwa hai na mwenye ufahamu) lakini pindi ROHO ikishamrudia MUNGU na mwili ukapumzishwa basi MFU hawezi hamua lolote, haisi chochote na wala hawi kokote pale.

Ufufuo ni ahadi ya Mungu kwa watu wake wote (wabaya na wema) baada ya hapo waliokufa wakiwa wametenda mema katika maisha yao yalopita duniani na wale wema walokutwa hai mpaka siku ya tukio

watapalizwa mbinguni kwenda kutawala na Yesu Kristo huko mahali pa juu(mbinguni) huku wale waovu wataachiwa miaka kadhaa ya utawala wa shetani hili watakapojutia mshahara wa dhambi zao na kwanini walirubuniwa na shetani,

waweze kupata nafasi nyingine ya wokovu kutokea hapa watapitia kipindi kigumu cha mateso na shuruba kali mpaka kufanikiwa kukombolewa(ndiyo maana Yesu anaonya na kutukumbusha kutumia nafasi hii tuliyonayo sasa) na kwa wale walokula sahani moja na shetani mpaka mwisho wakawa loyal kwake hata baada ya awamu ya pili ya matazamio kuisha watateketezwa nae kwenye moto wa milele.

Hivyo kwa mara ya kwanza baada ya kufa wafu watarudishiwa Nafsi zao na pumzi ya uhai(Roho) ile siku tu atakaporudi Yesu na kuwafufua wanadamu wote waliokufa na ndiyo maana ya msemo KILA jicho litamwona Bwana akishuka mawinguni akija kuwachukua walio wazima na wafu.
 
If thats what your Bible says i cant argue with you.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom