UKWELI: Hali ya Muhimbili Hospital na Ocean Road ni ya HATARI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UKWELI: Hali ya Muhimbili Hospital na Ocean Road ni ya HATARI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Jul 3, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,219
  Likes Received: 3,780
  Trophy Points: 280
  Imenilazimu leo kutembelea hospitali hizi kubwa nchini na kujionea hali ya mambo ilivyo,

  Nasikitika na kustaajabu ya Musa (serikali) kuona inaendesha propagana kuwa mgomo umekwisha ilihali hali ya mambo bado ni mbaya:

  HAKUNA huduma zinazoendelea zaidi ya wauguzi tu ndio wapo tena nao wachache!

  Nimefika Muhimbili Hospital saa tisa alasiri nikakaa mpaka saa kumi na moja jioni, nikaenda Hospitali ya Ocean Road, ambako nako nimekuta hali ni mbaya!

  Anaedanganya umma kuwa huduma zimrejea halitakii mema taifa hili,

  Nasema tena mgomo bado upo, labda madaktari warejee usiku huu au kesho!

  Seikali ielewe kuwa kanuni ni ile ile watumiayo wa amini wa kiroho:

  (waislamu) Huwezi kupata thawa za mwenyezi Mungu bila kuenenda na ktk utakatifu wake!

  (Wakristo) Huwezi kwenda mbinguni bila kupita kwa Yesu kristu.

  Njia pekee ya kumaliza mgogoro huu ni meza pana yenye kuratibiwa na ulimi wa busara tu!

  Ubabe na vitisho havitafanikiwa kwa hili, kitakachoumia ni nyasi tu (wananchi)

  Kama huamini nenda Muhimbili au UGUA kisha njoo jukwani hapa useme ulichoshuhudia au kilichokupata!

  Mungu lisaidi Taifa na Waja wako!
   
 2. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,279
  Likes Received: 10,463
  Trophy Points: 280
  matatizo ya vibahasha ndio haya.najua wagonjwa watasema ukweli hiyo kesho!

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  JK ni comedian...period.JK aliambiwa nchi haitatawalika akadhani utani..sasa ndo anaona mboga moto ugali moto ...mchana NZI usiku MBU...kudadadeki
   
 4. l

  lugano5 JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 4,342
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 5
  kweli nimeamini hii nchi inaendeshwa kwa propaganda na si vitendo
   
 5. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Afisa mahusiano wa Mhimbili kama kweli hiyo taarifa aliyotoa kaandika yeye Mungu hata msamehe kabisa, ni bora kukaa kimya kuliko kudanganya tena Uma. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabaliki Madakitari na Mungu mubariki Ulimboka
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  dhaifu tupu, propaganda za enzi za ukomunisti
   
 7. PAMBA1

  PAMBA1 Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Watanzania hatuna umoja,laiti tungekuwa wamoja mpaka sasa serikari ingekuwa imeondoka madarakani. Hat a maandiko matakatifu yanasema uoga ni dhambi tena mtu mwoga hataishi milele kwani atakufa kwa uoga wake. NA neno usiogope limeandikwa Mara 360 ndani ya biblia NA ni kila Kurasa imeandikwa usiogope. Ukiwa unasoma kila Kurasa kwa siku moja utasoma neno usiogope mwaka mmoja kasoro siku 6
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa walioangalia taarifa ya habari TBC wamesema chochote kuhusu hali ya huduma Muhimbili?
   
 9. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Madaktari, mna habari kwamba tunalipa bima ya afya kila mwezi? Sasa kwa nini mnatutelekeza hivi? Hivi mmeigomea serikali ama walipa kodi? Je, mliwahi kumwona kiongozi yeyote wa kisiasa akija kwenu kutibiwa? Au hamjui kwamba politicians wanatibiwa Bara Hindi?
   
 10. F

  FUSO JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  Taarifa ya Habari ITV saa mbili inasema mgomo umeisha na madaktari Bingwa wote wanaendelea na kazi kama kawaida hata yule aliyetoa press release jana kwenye vyombo vya habari kuwa madaktari bingwa wametangaza mgomo basi hata yeye yupo kazini.

  Pia wale wanafunzi wa udaktari wameambiwa wakariport wizarani haraka sana kujua hatma yao.

  Sasa sijui huyu msemaji wa muhimbili akawa sawa na yule Waziri wa Ulinzi wa IRAQ wakati wa vita ambaye alipata Tuzo ya propaganda ya kusema urongo? Kama hamjui basi hii ndiyo TZ yetu.
   
 11. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo Biblia Takatifu ina kurasa 360 na kila ukurasa umeandikwa USIOGOPE, siyo?!
   
 12. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kuna watu wakisikia madaktari wamejea kazini wataugua. Sijui wananufaika nini na mgomo huu!
   
 13. Sisomeki

  Sisomeki Senior Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nimengalia TBC habari wanaonyesha picha ambazo jana pia niliziona hizo hizo,sasa najiuliza ni propaganda au? maana jipya ni kamati sijui ya mkoa wa Dar es Salaam na kauli ya Kova
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,856
  Likes Received: 2,333
  Trophy Points: 280
  bila kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi unafikiri madaktari wanaweza kuwatibu hata hao walala hoi kwa ufanisi?

  Imagine hata CT-Scan machine moja katika hosp za serikali nchini hamna, mpaka uende Aghakhan au Regency --- kweli wakuu? hivi unategemea TZ hii bila kudai haki yako utaipata?

  Tujilaumu wenyewe kuiweka madarakani serikali isiyojali ubora wa huduma za jamii -- hasa Afya na Elimu. haya ndiyo madhara yake. ngoja tujifunze ili next time tuwe makini.
   
 15. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Watangaze nini tena maana mgomo ulishaisha kwa hiyo hakuna habari tena
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Kuna watu wengine bado wako enzi za mwalimu. Wanafikiria ubabe unafanya kazi in this sophiscated world.
   
 17. Mpangamji

  Mpangamji JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 536
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa mujibu wa TBC, hali imeendelea kuimarika, wagonjwa wanapata huduma kama kawaida, kisha wakaonyesha picha ya daktari waliyoonyesha jana akipita wodini kuangalia wagonjwa, kisha wakamhoji mheshimiwa Dr. Mwinyi akiwa Arusha, akasema wapo madaktari wengi waliorudi kazini na wachache bado wameshikiria msimamo wao. Mwisho wakamuonyesha Kamanda wa kanda maalum akitoa wito kwa wale wanaotoa vitisho kwa madaktari wanaoendelea na kazi na kutoa namba ya simu ambayo wakipata meseji ya kitisho chochote wawasiliane nae mara moja nae atachukua hatua mara moja.

  Jf watch out, unaweza kukamatwa kwa kisingizio kuwa umetoa kitisho kwa daktari anayeendelea na kazi.
   
 18. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  "Mtu yeyote, ambaye hatafanya kitu chochote, ataishi, hatimaye atakufa, bila kufanya kitu chochote"
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red: mtindo wa ccm, polisi watatengeneza 'message' inayoonekana kama vitisho toka kwa madaktari walio goma ili ionekane 'wale wanaoendelea na kazi' wanatishiwa na madaktari wenziwe.

  CCM kwa propaganda hawana tofauti na Jim Jong-il , the late 'dear leader' of North Korea.
   
 20. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kama ni kweli madaktari wamerudi kazini jee huduma ya afya itarejea kama mwanzo.vyombo vya habari vinataka kutusahaulisha mgomo huu.
   
Loading...