Kwa uchunguzi wangu ushindi wa CCM unafanikiwa kutokana na idadi ndogo ya wapiga kura wanaojitokeza kuchagua viongozi wa Taifa letu la Tanzania. Ukiangalia vizuri idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ni ndogo sana ukilinganisha na waliojiandikisha. Pia kwa uchunguzi wangu wanachama wa CCM hupiga kura haswa. Kwa mfano mwaka huu iwapo tungejitokeza wengi kupiga kura hakuna namna kura zingechakachuliwa. Mimi nachukulia idadi iliyobaki(ambayo haikupiga kura) asilimia kubwa wangepiga kura zingeenda upinzani. Hivyo sasa ni jukumu letu sisi tunaopenda mabadiliko na maendeleo ya kweli kuanza kuuelimisha uma umuhimu wa kura. Na hivyo naamini mafanikio yatakuwa makubwa katika uchaguzi ujao.
Naomba kuwasilisha hoja.....
Naomba kuwasilisha hoja.....