Wakati Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akihutubia wakazi wa Mkoa Kagera, alionyesha kuhusisha janga la ukimwi na tabia ya uasherati na kuonyesha kama lilikuwa janga la kujitakia.
Alionyesha maneno "mto ngono" na neno "Katerelo" kuyahusisha na tabia ya uasherati. Leo hii kwa faida ya kila mtu aliyesikia anayahusisha neno mto ngono na uasherati kufuatia neno la kishwahili la ngono kama tendo la kujamiana, aelewe maana halisi na aachane na upotoshaji.
Nimeshawika kuelezea maneno haya na yalivyotokea katika lugha ya kihaya na maana yake. Nianze na neno mto ngono; Mto ngonon unaanzia eneo linaloitwa Lwamilinga, eneo lililopo wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera.
Mto ngono humwaga maji yake katika mto Kagera, ambao nao humwaga maji yake ndani ya Ziwa Victoria. Ziwa nalo humwaga maji kwenye mto Nile kabla ya kuinufaisha bahari ya Mediterranean.
Katika mto ngono kuna aina fulani ya mimea inayotambaa, nayo inaitwa "omugono". Mimea hiyo hutumika kutengenezea aina fulani ya mitego ya samaki. Wingi wa "omugono" ni "engono". Hivyo ndivyo unavyoitwa mto ngono na watu wa eneo letu. Kwa maana hiyo neno ngono halina uhusiano na tendo la kujamiiana kama rais anavyotaka ifahamike. Hakika akutukanae
hakuchagulii tusi.
Katerelo ni eneo lililopo katika wilaya ya Bukoba Vijijini karibu na bandari ya Kemondo. Hapo palikuwa makao makuu ya tarafa. Tarafa ya Katerrlo wakati wa utawala wa kikoloni ilikuwa ndio makao makuu wa chifu wa eneo linaloitwa Kianja. Utawala wa machifu ulikuwa unaendeshea shughuli za kiutawala hapo na hadi leo hii jengo lililokuwa likitumiwa na chifu bado lipo.
Hukumu zilitoleewa hapo na adhabu halikadhalika. Moja ya adhabu hizo zilikuwa ni kuwachapa wahalifu viboko. Kwa maana hiyo kila aliyeshitakiwa na kuitwa, alijua eneo hilo ndipo wanapochapiwa. Kwa kihaya neno kupiga ni "kutela" na eneo wanapotolea adhabu ya kuchapa viboko ni "Katerelo". Kwa
maana halisi neno hilo halina uhusiano na mtindo wa kufanya mapenzi kama ambavyo rais wa nchi anataka watu waamini.
Nihitimishe kwa kusema lugha ya kiswahili imeundwa na maneno ya kibantu na lugha ya kihaya ni lugha ya wabantu. Isishangaze maneno kuingiliana na hata kama yana maana tofauti. Kwa mfano; wanyakyusa wanatumia neno "mwagona" likiwa na maana ya salamu, wakati katika lugha ya kihaya neno wagona lina maana ya "kukoroma"
Cc: Lameck Mwijage
....Abhahaya bona omu nimwo mwatu
.......Facebook group......