Ukwaju unalimwa wapi Kwa wingi?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,233
12,508
Ukwaju umeajili watu wengi Sana Tanzania na hasa dar salaam ambako kuna tani nyingi za juice na icream za ukwaju unaopatikana kila kona ya jiji zikiwa zimeandikwa Ukwaju.

Huwa ninajiuliza ni wapi matunda ya ukwaju yanatoka Kwa wingi maana Tanzania hakuna kilimo cha ukwaju, mikwaju iliyoko ni miti ya asili iliyojiotea yenyewe porini, tena wananchi huwa wanaikata na kutengeneza mkaa, inazidi kupungua kwakuwa hakuna wakulima wanaoipanda miti ya mikwaju. Hivyo huwa ninajiuliza ni nchi gani duniani inalima na kuexport ukwaju Kwa wingi kiasi hiki?

Au hizi ice creams sio za ukwaju halisi?
 
ukwaju unapatikana maeneo mengi sana
Dodoma
Singida
Tabora
Shinyanga
Simiyu
Rukwa
Mwanza
 
Mkuu zile icecream usidhani ktk kutengeneza zinamaliza hata gramu5 za ukwaju,ni kiasi kidogo sana huwekwa kwaajili ya ladha.
 
Umenijaza mate mdomoni
Mimi pia.

Ukweli ni kuwa demand ya ukwaju ni ndogo kuliko supply. Ni asilimia ndogo sana inaingia sokoni. Mengi yanaishia kudondoka tu mitini na kuona. Ma miti yao mazuri sana kwa mkaa.
 
Mkuu zile icecream usidhani ktk kutengeneza zinamaliza hata gramu5 za ukwaju,ni kiasi kidogo sana huwekwa kwaajili ya ladha.
Kwahiyo ile rangi ya ukwaji (brownish) tunayoiona ni vitu vingine sio ya ukwaju? Kama ni kweli unachosema haiwezekani gram 5 za ukwaji zibadilishe rangi ya maji ya mapipa 1,000,000 ya sim tank zenye ujazo wa lita 10,000 kila moja kwa siku ya kutengenezea Ice creams. hebu wacha utani wako aloo.
 
Mm natengeneza Sabuni za kuogea ladha ya Ukwaju na Kahawa. Ukwaju nanunua Saadani. Kahawa nachukua Moshi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom