Ukuzaji wa lugha ya Kiswahili nilazima uende sambamba na ukuzaji wa nyanja nyingine

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,476
2,147
Katika wakati huu tunapokipigia kiswahili debe ili kiweze kukua na kuenea Afrika na duniani kwa ujumla nilazima tukumbuke kuwa mashiko ya lugha yeyote nilazima yaendane na hali ya kiuchumi na maendeleo mengine miongoni mwa wazalishaji wa lugha hiyo.

Nikiwa na maana kuwa lugha sio maneno tu Bali kile kinachobebwa na kuibeba na lugha hiyo. Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri utakubaliana nami kuwa lugha ya kilatini ni miongoni mwa lugha za mwanzo kutawala dunia kutokana na uwezo waliokuwa nao dola la kirumi kiuchumi n.k Leo hii lugha hii imekosa mashiko kutokana na kuzorota kwa dola hii na kuacha misamiati kadhaa ya kitaaluma kama, geografia, kemia n.k ikitumika katika lugha nyingine za ulaya na marekani.

Pwenti ya msingi ninayoilenga kiswahili hakiwezi kupata mashiko yakutosha Afrika na duniani kama tutaendelea kusalia nyuma kiuchumi nk.

Lazima kuwepo na sababu za msingi zinazowasukuma watu kujifunza lugha hii na sababu hizo ziwe nizalazima.

Aidha sababu hizo zinaweza kuwa zifuatazo,
Moja kuwepo kwa uchumi imara unaoweza kuwavutia wawekezaji na wafanya biashara kutoka nje ya mipaka yetu kutawalazimisha hao wageni kujifunza kiswahili ili waweze kufanya biashara nasisi

Pili, Elimu bora au maendeleo katika sekta ya elimu yenye uwezo wakuwavutia wageni kuja kusoma hapa nchini na ujuzi wa lugha ya kiswahili kiwe miongoni mwavigezo vya udahili

Tatu, vyombo vya habari vya kiswahili kutoka Tanzania vyenye uwezo wa kuvuka mipaka ya kimataifa

NNE, Utoaji wa bidhaa/ export than import.
Uzalishaji na ukuaji wa viwanda vitakavyozalisha bidhaa zenye ubora kushindana katika masoko ya kimataifa kutoka Tanzania na bidhaa hizo ziwe ma majina na lebo za kiswahili kunaweza kuchangia katika hili.
Mwisho fursa za lugha ya kiswahili zitaongezeka pale ambapo lugha hii itapata mashiko yakutosha lazima tuanze na hili kwanza.
 
Back
Top Bottom