Ukuu wa mikoa waleta mpasuko ccm

AMARIDONG

JF-Expert Member
Jun 24, 2010
2,502
177
BAADHI ya vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), hasa wenye maslahi na nafasi kadhaa za uteuzi, wanadai kwamba Rais Jakaya Kikwete anakosa uamuzi katika kuteua wakuu wa mikoa, baadhi yao wanadai kwamba upo uwezekano wa mkuu huyo wa nchi kumrejesha kwenye nafasi hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba.
Hadi anateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Makamba alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na kwa kiasi kikubwa alisifiwa kwa utendaji hodari.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, Makamba anaweza kurejeshewa ukuu wa mkoa kwa sababu amepwaya mno katika nafasi ya Katibu Mkuu.
Wanasema ingawa mwenyekiti wake, Rais Kikwete, amekuwa akimtetea kila mara ambapo wana CCM wametaka kumng’oa Makamba kwenye ukatibu mkuu, sasa wanayo hoja ya msingi, kwani CCM imeshindwa katika nafasi nyingi, kinyume cha matarajio yao.
Katika nafasi za ubunge, Tanzania Bara, CCM imeshinda kiti kimoja tu kilichokuwa kinashikiliwa na CHADEMA katika Jimbo la Tarime, mkoani Mara.
CHADEMA imeongeza idadi ya wabunge kutoka watano wa kuchaguliwa hadi 22 kutoka majimbo yaliyokuwa chini ya CCM.
Vilevile ni katika kipindi cha ukatibu mkuu wa Makamba ambapo migogoro imekuwa mingi ndani ya CCM na kuongeza makundi yanayohasimiana, huku upinzani nje ya CCM ukikua zaidi.
Baadhi ya vigogo wamefikia mahali pa kusema, “rais ameshindwa kuteua” wakuu wa mikoa, wakitaja baadhi ya majina ya rafiki zake wanaofikiriwa, na kwamba amekuwa na majina ya wateule wake kwa zaidi ya wiki sasa, lakini anashindwa kufanya maamuzi.
Baadhi yao wanasema kigugumizi hiki cha rais kinatokana na deni linalomkabili la kulipa fadhila kwa baadhi ya watu, ama waliomsaidia au rafiki zake wa karibu.
Baadhi ya vyanzo vyetu vya habari vina wasiwasi kwamba iwapo Rais atashindwa kuteua watu sasa, anaweza kujikuta anabadilisha majina kabisa kwa shinikizo la watu wengine, ikiwa ni pamoja na ushawishi wa baadhi ya wana familia.
Majimbo kadhaa katika baadhi ya miji mingi yenye biashara na guvu kisiasa yamechukuliwa na wapinzani. Miji hiyo ni pamoja na Dar es Salaam ambapo Kawe na Ubungo yamechukuliwa na CHADEMA; Mbeya Mjini imechukuliwa na CHADEMA; Iringa Mjini imechukuliwa na CHADEMA; Nyamagana na Ilemela Mwanza Mjini yamechukuliwa na CHADEMA; Musoma Mjini imechukuliwa na CHADEMA.
Habari zinaeleza kuwa baadhi ya wakuu wa mikoa wanaopewa nafasi kubwa ya kurudi ni wale waliokuwa wabunge na ambao wameshindwa kutetea nafasi zao majimboni, ambao ni Mohamed Abdulaziz, James Msekela na Monica Mbega.
Aidha, wakuu wengine wanaotajwa kuendelea kuwepo ni wale waliokuwepo tangu awali ingawa wapo watakaoondolewa kwa sababu za umri na kukosa rekodi nzuri ya utendaji.
Miongoni mwa vigezo vinavyoweza kutumika kuwapunguza baadhi ya wakuu wa mikoa ni kwenye maeneo ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefanya vibaya au kimeshindwa kwenye matokeo ya uchaguzi mkuu.
Kwa Dar es Salaam, mkoa ulio wazi baada ya aliyekuwa mkuu wake, William Lukuvi, kuteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, unadaiwa kuwa mgumu kiutendaji kutokana na aina ya watu wanaoishi na wingi wa shughuli zake.
Hata hivyo waliowahi kuwa wakuu wa jiji la Dar es Salaam wanapewa nafasi ya kurudi tena kwa madai mbalimbali ikiwemo ya kumpata mtendaji mwenye uwezo wa kukabiliana na vurugu za jiji hili.
Abbas Kandoro, aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa huu ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mwanza, naye anapewa nafasi pia ya kurejea jijini hapa.
Alipozungumza na gazeti hili, mmoja wa watendaji wa Ikulu, aling’aka akidai kwamba Rais Kikwete hafanyi kazi kwa shinikizo la vyombo vya habari.
“Mwacheni rais afanye kazi yake, ninyi watu wa vyombo vya habari ndio mnaoleta shinikizo, rais hafanyi kazi kutokana na vyombo vya habari… nakuomba muwaache watu wafanye kazi kwani hata asipotangaza sasa hivi nani anadhurika?
“Huu sio utawala mpya, rais anaendelea kwani lazima atangaze? Anaweza kuwaacha walewale… kwani hakuna wakuu wa mikoa hivi sasa?” alihoji ofisa huyo na kusisitiza akilitaka gazeti hili kuachana na habari hiyo.
Hata hivyo, zipo taarfa kuwa wakati wowote sasa Rais Kikwete anatarajia kuteua wakuu wa mikoa 29 huku kukiwa na sura kadhaa mpya.
 
another pumba if nt habari ya kufikirika.lets focus on other mo productuve things people.
 
What extra-ordinary thing do you expect from teuzi hizo? search for another foci! :whoo:
 
NAPENDA MAKAMBA AENDELEE kUWA KATIBU MKUU WA CCM , ILI AKIMALIZE KABISA. MPAKA 2012 UCHAGUZI WA CCM UKIWADIA, CCM chini ya MAKAMBA KAMBA PWAA, tena KWA KUJIFUNGA MABAO YENYEWE. SI UNAJUA TENA JK HURUSU TAKUKURU KUWAANDAMA BAADHI YAO.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom