Ukuta wa Mirerani upo lakini bado Tanzanite inaibwa...

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Waziri awaagiza TAKUKURU kutinga Mererani kuchunguza wizi unaofanyika.

Tuliambiwa kuwa kujenga ukuta ndiyo ingekuwa ni muaraobaini wa kuibiwa kwa madini hasa Tanzanite.

=====

Kachunguzeni wizi wa Tanzanite"-Mchengerwa
-
"Niliwaombe ndugu zangu wa TAKUKURU kumekuwepo na wizi mkubwa sana kwenye eneo letu la Madini Manyara na taarifa hizi sio siri tena ukifika Arusha unapata taarifa ni namna gani wizi unaendelea na rushwa imekuwa ikitamaraki katika eneo hili.

"Sasa niwaagize TAKUKURU nawapa wiki mbili ili muende mkafanye uchunguzi kile kinachoendelea kule Mererani katika mgodi ambao unamilikiwa na serikali na wizi mkubwa unaoendelea kutokana na taarifa ambazo zimeenea katika Mikoa ya Arusha na Manyara ili tuweze kubaini ni kitu gani kinaendelea katika mgodi wetu," amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohammed Mchengerwa, wakati akizindua program tumishi ya Ajira App uliofanyika leo Novemba 19, 2021 jijini Dodoma.

#MtanzaniaDigital
 
Waziri awaagiza Takukuru kutinga mererani kuchunguza wizi unaofanyika.

Tuliambiwa kuwa kujenga ukuta ndiyo ingekuwa ni muaraobaini wa kuibiwa kwa madini hasa Tanzanite...
Kwani walinzi wa tanzanite hawana ndugu na jamaa wanaohitaji misaada? Hawataki kuwa na nyumba, hawataki kusomesha watoto wao shule nzuri? Wizi hautazuiiwa na ukuta bali hali Bora ya wananchi wote.
 
Kwa kujenga ukuta na kupeleka Jeshi kwa kiasi kikubwa sana imepunguza wizi. Ni dhahiri wadau waliokuwa wananufaika na uholela na wizi uliokuwepo hawakufurahi kuona Ukuta na Jeshi kwasababu wenzetu hawa katika uadilifu na Uzalendo wana Uafadhali kidogo kuliko wadau wengine tunaowafahamu.

Sasabasi. Hizi taarifa za wizi Serikali inatakiwa kuwa makini sana katika maamuzi . Nina shaka huenda ikawa ni Propaganda za wadau hasa wafanyabiashara wa Arusha, Manyara na Kenya kutaka Mfumo unaofanya kazi Mererani ubadilishwe ili iwe rahisi kwao kufanya yao.
 
Waziri awaagiza Takukuru kutinga mererani kuchunguza wizi unaofanyika.

Tuliambiwa kuwa kujenga ukuta ndiyo ingekuwa ni muaraobaini wa kuibiwa kwa madini hasa Tanzanite...
Madini yanaibiwa halafu yanapita wapi?huyo waziri anasema akiwa kalewa kiwingu
 
Huyo Waziri si ndo yule mkwe wa Samia,yupo kwenye project ya kuonyesha alichofanya Magufuli hakifai,alianza kutangaza waliofoji vyeti watarudishwa kazini,mimi nimempuuza ni mpuuzi
Kwa kujenga ukuta na kupeleka Jeshi kwa kiasi kikubwa sana imepunguza wizi. Ni dhahiri wadau waliokuwa wananufaika na uholela na wizi uliokuwepo hawakufurahi kuona Ukuta na Jeshi kwasababu wenzetu hawa katika uadilifu na Uzalendo wana Uafadhali kidogo kuliko wadau wengine tunaowafahamu.

Sasabasi. Hizi taarifa za wizi Serikali inatakiwa kuwa makini sana katika maamuzi . Nina shaka huenda ikawa ni Propaganda za wadau hasa wafanyabiashara wa Arusha, Manyara na Kenya kutaka Mfumo unaofanya kazi Mererani ubadilishwe ili iwe rahisi kwao kufanya yao.
Ukuta, Sabaya na gambo ni mkakati wa kuidhiofisha kama sio kuiua Chadema.
 
Kama huelewi umuhimu wa mifumo imara na katiba bora rejea Marekani Trump alipojaribu kung'ang'ania madaraka baada ya kushindwa uchaguzi na akafurushwa kama mbwa koko na kila taasisi. Ingekuwa Africa wangetumwa wazee wenzake kwenda kumbembeleza aondoke.
Muarobaini ni uadilifu na uzalendo tu sababu hata mifumo inaendeshwa na watu wakiamua kuihujumu hamna kitu mtafanya!

Same as to katiba mtu akiamua kuipuuza hata ingekuwa nzuri kiasi gani hamna jema litatukia!
 
Waziri awaagiza Takukuru kutinga mererani kuchunguza wizi unaofanyika.

Tuliambiwa kuwa kujenga ukuta ndiyo ingekuwa ni muaraobaini wa kuibiwa kwa madini hasa Tanzanite...
CCM na Serikali yenu dhalim msipoacha ushetani wa kuwabambikia watu kesi za ugaidi mtapata pigo lingine kuuuubwa sana,pigo moja tu pigo lililonyooka pigo takatifu mpaka mtie akili.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom