Ukuta Open space iliyovamiwa Ocean Road Wavunjwa

Vipi kuhusu lile eneo zuri sana la wazi katikati ya central police station, trl au station ya reli na nyumba za police mkabala na traffic makao makuu??? Nana limezungushiwa wigo kama vile linataka kujengwa. Ni aibu. Dar hewa itatoka wapi. Mbona maeneo ni mengi?? kuna anayejua kinachoendelea pale atupatie habari za kweli ili tupinge kwa huja. Sura ya jiji kwaheri. Miundo mbinu haiongezeki wakati maghorofa yanazidisha giza mjini.
 
ni kwali jamani, nimepita sasa hivi hapa Palm Beach hotel. Pako wazi yaani panapendeza kama zamani. Mwambieni huyo Mkadamu aondoe kifusi chake hapo sasa kilaleta uchafu na watu wanakosa pa kupark magari

Si unaona jinsi serikali ikiamua kulinda haki na kusimamia sheria mambo yanavyokuwa mazuri eee?

Akina magufuli na Maige waendelee tu kuhutubia waandishi wa habari
 
avatar14388_4.gif



(copied from chipukizi)
 
Isije kuwa ni maelewano na Sirikali hawa jamaa wabomolewe halafu walipwe fidia kubwa baadae maana:
  • Huyu Muccadam alionyesha jeuri ya hali ya juu sana
  • Ndio wafadhili wakuu wa CCM
  • Sirikali inataka kuonesha iko kazini
  • Yale maghorofa ya Sea Cliff ilikuwaje?
 
big up mama Tibaijuka.. hamna scary game hapo ardhi ni mali ya serikali,

Nangojea maeneo ya wazi yaliyochukuliwa na CCM itakuwaje manake wamechukua yote na wanafanya parkin za magari
 
Katika kuusaka ukombozi wa nchi hii, gharama si kitu cha kukwepeka kabisa.
So I will boldly say....screw the so called "consequential costs" if that's what it takes to get there!!

I fully second this mama's move (I mean for starters). Full recognition ya efforts zake however ita-materialise pale tu atakapokwenda an extra mile.....play hard ball with all those culprits serikalini. Au nao wanalindwa na JK (ref wikileaks/Hosea)??

Hit'em hard where it hurts and they will let go!
 
Nimepita hapo saa moja na nusu usiku, yaani dakika chache zilizopita. Askari wa Jiji na polisi jumla hawapungui 100. Magari matano yamepark upande wa baharini yameeasha taa kumulika upande wa pili wa barabara kuliko na ukuta ambao unavunjwa na tingatinga.

Eneo hili liko baada ya hospitali ya agha khan karibu na uwanja wa golf. Kulikuwepo amani na utulivu, askari wamejipanga imara na tingatinga likiendelea kubomoa huo ukuta tartiiibu, kwa uhakika. Askari wawili walikuwa bize wakiharakisha magari kupita kasi, hivyo sikuweza kupiga picha


Hongera sana mama kwa kuanza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM vizuri
 
Naona watu washaanza kushabikia haya mambo ya rule of the junglelakini pamoja na jazba na ushabiki uliopo hebu turudi nyuma na kujiuliza maswali yafuatayo:

1. Why huo ubomoaji ufanyike usiku wa manane? Wanaogopa nini mchana? Unataka tingatinga litimbe town mchana? Foleni lake utaliweza achilia mbali foleni ya kila siku ya kawaida hapa tingatinga tano na magari ya polisi na mgambo wa jiji, kilichofanyika ni busara kuepusha usumbufu kwani wangebomoa mchana kungetokea nini, matokeo yangekua the same

2. Why tibaijuka au ofisi yake haikutoa clarification yoyote on allegations alizozitoa taher? Hivi unataka kuongea na fisadi wakati amri ilikwishatolewa kitambo na Mkapa kufuta uuzwaji wa kiwanja hicho, Wajua ardhi ni mali ya serikali na ina haki ya kuamua kubadilisha matumizi anytime if necessary?

3. What if taher was right na tibaijuka was wrong, je ni pesa za nani zitalipa hiyo fidia? Kama kutakuwa na issue ya fidia basi na Tibaijuka anahusika sidhani kama anafanya asilolijua na nina amini wizara yake ina wanasheria wanao mshauri, najua wasiwasi wako ni mambo ya Dowans do you know Tanesco ili hire lawyers so that kind of ruling will be offered in order to benefit the so called mafisadi this is why will not pay it

Just curious


Kamata tano Tibaijuka sijajua kama ni nguvu ya soda au this will be till 2015
 
Hapo juu niliuliza kwamba Amatus Liyumba alishitakiwa kwa kosa gani. nadhani ama sikueleweka au mimi sikujieleza vema.

Namaanisha hivi, kwa nini serikali inakuwa na double stds kwamba liyumba ameshitakiwa na kufungwa kwa kutumia madaraka vibaya na kusababishia serikali hasara lakini a lot of others are still at large?

Lukuvi alikurupuka na Maafisa Ardhi wa manispaa za dar na baadhi ya watu wachache wakafikishwa mahakamani. Sijui kama hizo kesi bado zipo.

Huyu mama akitaka kumaliza hili tatizo awafungulie mashtaka watendaji wa wizara yake ambao ndio walifanya ufisadi huu kwa miaka yote. Maafisa ardhi wa halmashauri wasingeweza kufanikisha haya mambo bila idhini ya watendaji wa wizara.

tena tumeona katika jeuri za Mkaadamu alipokuwa anamlazimisha mama yetu mtanzania halisi amuombe radhi. alikuwa anatoa vielelezo vya ikulu!!!!!!

Mama Tiba, tunasema hii ni hatua ya kwanza tu uliyofanya jana. Ili tuweze kuona kwamba kweli una nia ya kukata mzizi wa fitna, tafadhali wafikishe maofisa wa wizara yako mahakamani na au uwafukuze kazi kwa manufaa ya umma. Pili uvunje majengo kwenye maeneo mengine yote ya wazi hapa Dar. Inawezekana kabisa kama hiyo nia yako ni njema.
 
Nimepita hapo saa moja na nusu usiku, yaani dakika chache zilizopita. Askari wa Jiji na polisi jumla hawapungui 100. Magari matano yamepark upande wa baharini yameeasha taa kumulika upande wa pili wa barabara kuliko na ukuta ambao unavunjwa na tingatinga.

Eneo hili liko baada ya hospitali ya agha khan karibu na uwanja wa golf. Kulikuwepo amani na utulivu, askari wamejipanga imara na tingatinga likiendelea kubomoa huo ukuta tartiiibu, kwa uhakika. Askari wawili walikuwa bize wakiharakisha magari kupita kasi, hivyo sikuweza kupiga picha



Big up Mama watanzania wote tupo pamoja na wewe, ila tunaomba watu waliohusika na huo uchafu watajwe jamii yote iwatambue na sheria ichukue mkondo wake na hawa wakina kuchi kuchi hot hai wawajibishwe. mtu hawezi kukurupuka na kumpa siku Mheshimwa Waziri amuombe msamaha wakati yeye ndiye mwenye makosa kwakua yeye ana pesa au ni mhindi
 
nafikiri kama mama huyu atafanya inavyotakiwa kweli tutapata nafuu tukumbuke ngoyai lowasa alisafisha kidogo habari za open space nakumbuka hata keko tulisaidiwa na yeye lakini leo hii imejengwa petrol station na mwarabu wa bakery mama pigana halafu nisaidieni ili nipeleke maoni yangu kwa mama nitumie address gani ambayo haitakabwa na kupeperushwa kabla ya kuipata?
 
wanawake tunaweza,,,

HONGERA SANA MAMA

TUPO NYUMA YAKO TUNAKUOMBEA
Naona tukiendelea hivi sasa tutakuwa tunaelekea kwenye sexism....... Hongera Tibaijuka.... (her sex does not matter)... na hii ni evidence tosha kwamba viti maalumu vifutwe....... havina maana.
 
hivi jamani ukuta si sehemu ndogo tu...inaweza kuweka hata garden..nifahamisheni,..mi nadhani kuna nyumba nyingi za kubomoa especiaaly waliovamia open spaces
 
Back
Top Bottom