Ukuta Open space iliyovamiwa Ocean Road Wavunjwa

Unajua hapa nadhani its good kuonyesha mfano to set a precedent among watu ambao wanachukua vitu vya manufaa ya umma for their own private issues...... (kwahiyo nadhani hicho kiwanja kurudi kuwa open space ni kwa manufaa ya umma) Pili nadhani hata kama jamaa aliuziwa hicho kiwanja which was open space in the first place nadhani some illegality ilitake place.

Good point mkuu but inawezekana amendments zilifanyika wizarani au halmashauri kuwa baadhi ya maeneo ya wazi yauzwe kwa watu wayaendeleze maana serikali imeshindwa kuyahudumia inakuwaje hapo mkuu!!!
 
Wakati wa Nyerere huyu mmiliki angechapwa viboko kwa kuidhalilisha mamlaka ya nchi. Waziri ni muwakilishi wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na chochote anachofanya in good faith kina mamlaka ya rais.

Tofautisha Serikali MAKINI na Serikali ya KISANII! Si unaona mchezo mchafu wa Richmond, DOWANS na TANESCO. Nahisi hata mawakili waliokwenda kututetea ni wawakilishi wa mafisadi! Nchi hii raha tupu!
 
Good point mkuu but inawezekana amendments zilifanyika wizarani au halmashauri kuwa baadhi ya maeneo ya wazi yauzwe kwa watu wayaendeleze maana serikali imeshindwa kuyahudumia inakuwaje hapo mkuu!!!

Hapo tutakuwa tumeumia.....as always......., lakini I hope Tibaijuka ni makini na ameangalia hii issue from dfferent angles....

At the end of the day binafsi nataka nione watu wanawajibishwa no matter the outcomes.... Hapa kuna mtu alifanya kosa na hili sasa limekuwa ni jambo la kawaida Tanzania people mess up and wananchi pick up the pieces.
 
Hapo tutakuwa tumeumia.....as always......., lakini I hope Tibaijuka ni makini na ameangalia hii issue from dfferent angles....

At the end of the day binafsi nataka nione watu wanawajibishwa no matter the outcomes.... Hapa kuna mtu alifanya kosa na hili sasa limekuwa ni jambo la kawaida Tanzania people mess up and wananchi pick up the pieces.

Tuko sawa ila napendelea watu waliohusika wawajibishwe na sio sie wananchi tunawajibishwa. Maana wasipoihandle with care hii ishu is another Dowans.
 
Safi sana mamaa!! Mi sipendi dharau.
Wahindi wanataka kuingia mpaka jikoni!!!
 
Tuko sawa ila napendelea watu waliohusika wawajibishwe na sio sie wananchi tunawajibishwa. Maana wasipoihandle with care hii ishu is another Dowans.

Exactly, hii ingemake sense pamoja na kurudisha viwanja pia wangewatrace down wote waliohusika na waliofaidika katika mpango mzima wa kuuziana even if hawapo tena katika hizo nafasi..Nadhani documents alizonazo mnunuzi zitakuwa na sahihi za baadhi ya waliokuwa behind the deal then it shouldnt been hard kama kweli nia ipo.
 
Baada ya open space karibu na hospitali ya Agha khan kubomolewa ukuta wake na baadaye ukuta wa karibu na Palm Beach i think the next stop ni open space ya Avalon cinema stay tuned, hakuna cha Dowans wala nini ni wasiwasi wenu tu hii issue ni ndogo sana tutaimaliza kimya kimya.
 
Vipi ule ukuta wa kiwanja cha pale Gymkhana karibu na Agha Kahn hospital? Eneo lilikuwa wazi miaka yoote leo kiwanja kinajengwa sijui hospitali au nini?
 
Sheria ni wazi hilo ni eneo wazi, ye yote aliyeruhusu kutoa kibali, na wote waliohusika katika mlolongo huo washtakiwe na kufilisiwa kwa kupindisha sheria na ramani ya mipango miji. Full stop.
 
Tibaijuka ‘ang’ata’ usiku

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 21st December 2010 @ 23:59

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, aliposema atahakikisha watu waliojenga kwenye maeneo ya wazi na yasiyoruhusiwa wavunje wenyewe majengo yaliyopo, hakuwa anatania na wale waliokuwa wakimvimbishia kichwa, watakuwa wamekosea.

Hali hiyo ilidhihirika jana jioni wakati tingatinga la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala mkoani Dar es Salaam, lilipofanya kazi ya kuvunja maeneo ambayo yameanza kujengwa majengo kinyume cha utaratibu na ambayo inaaminika kuwa ni ya wazi au hayaruhusiwi majengo hayo.

Jana majengo mawili katika Jiji la Dar es Salaam, kiwanja kilichopo karibu na Hoteli ya Palm Beach, ambacho ndio kwanza kilikuwa kimepandishwa ukuta pamoja na ukuta mwingine uliojengwa jirani na Hospitali ya Aga Khan katika Barabara ya Ocean Road, vilivunjwa jana jioni na askari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Licha ya mmiliki wa kiwanja cha jirani na Hoteli ya Palm Beach, Taher Muccadam kutoa notisi ya siku saba kwa Waziri Profesa Tibaijuka amuombe radhi na kumlipa fidia ya Sh bilioni mbili kwa madai kwamba alimvunjia heshima kwa jamii vinginevyo atamfikisha mahakamani, agizo hilo limepuuzwa.

Badala yake, umma wa wakazi wa Dar es Salaam waliokuwa wakirejea majumbani mwao jana jioni, walishuhudia tingatinga la Manispaa ya Ilala, lenye namba SM 3937, chini ya ulinzi mkali, likifanya kazi ya kuangusha ukuta huo saa moja jioni kabla ya kuhamia ukuta wa jirani na Aga Khan nusu saa baadaye.

Kazi hizo mbili zilifanywa na tingatinga hilo chini ya ulinzi wa askari zaidi ya 50 waliokuwa katika magari mengine manne, Isuzu; Toyota Land Cruiser Hard Top, Toyota Double Cabin na Toyota Nissan Patrol yenye namba za usajili SM 3096, SM 4360 na STJ 5662, mali ya Manispaa ya Ilala.

Mara baada ya kazi hiyo kukamilika katika eneo la Palm Beach, wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo, baadhi yao walisikika wakisema, “huyu ndiye Waziri, siyo viongozi wababaishaji. Watu wanamtisha eti wana vibali kutoka Ikulu, yeye aliwambia hatishiki na vibali vyao.”

Mwingine alisema, “huyu mama (Profesa Tibaijuka) hana mchezo, kama fedha anazo za kutosha, hasumbuliwi na vijisenti…tunahitaji viongozi wenye kusimamia sheria nchini mwetu.”

Mmoja wa viongozi waliosimamia kazi hiyo, hakutaja kutaja jina lake wala kueleza hatua hiyo imefikiwa na nani, akisema, “hatupo hapa kuongea na vyombo vya habari. Kazi mnaiona.”

Kiwanja hicho cha Palm Beach ambacho ni namba 1006 ni kati ya viwanja ambavyo Profesa Tibaijuka alidai kuwa ni cha wazi na kwamba hakiruhusiwi kuwa makazi.

Hivi karibuni, Profesa Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam aliwataka wananchi waliopora viwanja na maeneo ya wazi nchini na kujenga, wajisalimishe kwa mazungumzo, kwa sababu huenda wakaokoa hata matofali kabla hatua zaidi hazijachukuliwa
 
Licha ya mmiliki wa kiwanja cha jirani na Hoteli ya Palm Beach, Taher Muccadam kutoa notisi ya siku saba kwa Waziri Profesa Tibaijuka amuombe radhi na kumlipa fidia ya Sh bilioni mbili kwa madai kwamba alimvunjia heshima kwa jamii vinginevyo atamfikisha mahakamani, agizo hilo limepuuzwa na badala yake kapelekewa tingatinga na ukuta umebomolewa. Mama huyu kiboko.

Kilichobomolewa sio cha huyo Mucaddam, kama sikosei cha Muccdam kipo pembeni ya Palm beach, Ali Hassan Mwinyi Rd. Na hiki kilichobomolewa kipo Ocean Rd.
 
Vyote viwili kwa sasa ni VIFUSI tu!

Very good, huyu muccadama kazowea kutapele nyumba na viwanja vya watu, tene wamchunguze zaidi, watamkuta na madudu kibao. Ni Tapeli la hali ya juu, nasikia mkewe alimkimbia akarudi kwao Kenya kwa kushindwa kuishi na tapeli. Huyo mwanamke alikuwa anaogopa siku watakayoanza kuchukuwa sheria mikononi mwao hao anaewatapeli mumewe, she could be a victim of circumstances, akajiogopea akaamuwa arudi Nairobiii.

Yaani ni mtu wa vitisho kama alivyotaka kufanya kwa mama Tibaijuka, katisha.
 
Isiwe ni nguvu ya soda tu kwa kuanzia sababu kuna open space lukuki zimevamiwa katika maeneo mbali mbali ya huu mji wa dar es salaam ukienda oysterbay, masaki, mikocheni, kinondoni, sinza, mbezi beach na sehemu nyingine ukijumlisha na mikoani tena hususani kwenye viwanja ambavyo vingine vilipaswa kuwa vya michezo
 
Wezi wanapindisha Utaratibu makusudi,
Halafu mzigo wanauangushia Serikalini,
Serikali haina pesa kiwanda cha kuzalisha pesa zaidi
sisi wananchi wavuja jasho na kodi zetu kulipa madeni

Wawajibishwe hao wahuni wanaotufanya tubaki na madeni ya kizembe zembe
kila kukicha.
 
Back
Top Bottom