MAGAMBA MATATU
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 646
- 1,174
Ukuta kama wa Berlin unajengwa huko Kahama na Kampuni ya kuchimba madini ya Barrick- Buzwagi, ni ukuta wenye ghalama ya juu kuliko unavyofikiri, ni mzunguko wa km zipatazo 80, ninaposema ni wa ghalama ninamaanisha kuwa ni ukuta usiotumia tofali hata kidogo, inatengenezwa ukuta wa kubandika na unabandikwa kwa crane baada ya kuwa unakamilka kwa kila kipande na kwa sasa zimeishajengwa kama km 2, kma unaelekea kahama mjini kutoka shinyanga utauona huo ukuta,
Haijawahi kutokea hata Afrika ukuta mkubwa kuliko huo, sababu ni kuwa kampuni inahisi wataz wanaiba mali zao,
Huku kiampuni ikijenga ukuta huo wa matrion ya pesa wananchi wanaouzunguka mgodi huo wa Buzwagi hawana hata hospitali, shule zinazouzunguka mgodi huo wanafunzi wanakaa chini,wananchi wanaouzunguka mgodi huo hawana hata maji, Wananchi hawana umeme huku mgodi ukiwaka umeme kila siku.
Kibaya zaidi wafanyakazi wanaofanya kazi na kuupatia faida kubwa mgodi huo na kufikia kujenga ukuta huo wa BERLIN kwa matrion ya pesa mshahara wake ni dhaifu na kama ungeweza kupata saraly slips zao ungeshangaa sana kwani bado wana kipato cha 350000 cha enzi za Chiligati huku wakiajiliwa mamia ya wazungu wachomeleaji wa vyuma na mafundi wa kawaida na kulipwa zaidi ya sh milioni 20 kwa mwezi huku kazi wanayofanya ni sawa na wazawa waliopo hapo mgodini,nilipopita kuelekea kahama nilistaajabu sana kwa jinsi huo ukuta unaojengwa kwa ghalama kubwa na baada ya kumuuliza mdogo wangu niliyeenda kumtembelea kahama anafanya kazi pale Buzwagi na kumuuliza kipato chake,niliona saraly slip yake nikashangaa sana, na akaniambia kuwa kuna watu ni mafundi wa kuchomelea tuu vyuma kutoka Afrka kusini wanalipwa zaidi ya sh milion 20 kwa mwezi huku yeye akiambulia kiasi cha 350000 kwa mwezi na wote wanafanya kazi moja,
Hiii ni serikali yangu ila kwa hili nimeamini Tanzania haiko serious na wananchi wake, sikatai kwa kampuni kubwa kama hii ya Barrick kujenga ukuta mkubwa kama huu, swali langu ni dogo tuu,
1. Je hiii kampuni inawajali kimaslahi hao wafanyakazi wanaosababisha wapate hizo faida zote????
2. Je hii kampuni inawapa wananchi wanaouzunguka huu mgodi huduma bora kama afya na elimu kulingana na faida kubwa hii wanayopata????