Ukuta kama wa Berlin wajengwa Tanzania kwa pesa za watanzania

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,174
Ukuta kama wa Berlin unajengwa huko Kahama na Kampuni ya kuchimba madini ya Barrick- Buzwagi, ni ukuta wenye ghalama ya juu kuliko unavyofikiri, ni mzunguko wa km zipatazo 80, ninaposema ni wa ghalama ninamaanisha kuwa ni ukuta usiotumia tofali hata kidogo, inatengenezwa ukuta wa kubandika na unabandikwa kwa crane baada ya kuwa unakamilka kwa kila kipande na kwa sasa zimeishajengwa kama km 2, kma unaelekea kahama mjini kutoka shinyanga utauona huo ukuta,

Haijawahi kutokea hata Afrika ukuta mkubwa kuliko huo, sababu ni kuwa kampuni inahisi wataz wanaiba mali zao,
Huku kiampuni ikijenga ukuta huo wa matrion ya pesa wananchi wanaouzunguka mgodi huo wa Buzwagi hawana hata hospitali, shule zinazouzunguka mgodi huo wanafunzi wanakaa chini,wananchi wanaouzunguka mgodi huo hawana hata maji, Wananchi hawana umeme huku mgodi ukiwaka umeme kila siku.

Kibaya zaidi wafanyakazi wanaofanya kazi na kuupatia faida kubwa mgodi huo na kufikia kujenga ukuta huo wa BERLIN kwa matrion ya pesa mshahara wake ni dhaifu na kama ungeweza kupata saraly slips zao ungeshangaa sana kwani bado wana kipato cha 350000 cha enzi za Chiligati huku wakiajiliwa mamia ya wazungu wachomeleaji wa vyuma na mafundi wa kawaida na kulipwa zaidi ya sh milioni 20 kwa mwezi huku kazi wanayofanya ni sawa na wazawa waliopo hapo mgodini,nilipopita kuelekea kahama nilistaajabu sana kwa jinsi huo ukuta unaojengwa kwa ghalama kubwa na baada ya kumuuliza mdogo wangu niliyeenda kumtembelea kahama anafanya kazi pale Buzwagi na kumuuliza kipato chake,niliona saraly slip yake nikashangaa sana, na akaniambia kuwa kuna watu ni mafundi wa kuchomelea tuu vyuma kutoka Afrka kusini wanalipwa zaidi ya sh milion 20 kwa mwezi huku yeye akiambulia kiasi cha 350000 kwa mwezi na wote wanafanya kazi moja,

Hiii ni serikali yangu ila kwa hili nimeamini Tanzania haiko serious na wananchi wake, sikatai kwa kampuni kubwa kama hii ya Barrick kujenga ukuta mkubwa kama huu, swali langu ni dogo tuu,
1. Je hiii kampuni inawajali kimaslahi hao wafanyakazi wanaosababisha wapate hizo faida zote????

2. Je hii kampuni inawapa wananchi wanaouzunguka huu mgodi huduma bora kama afya na elimu kulingana na faida kubwa hii wanayopata????

rejea mkataba wa buzwagi na tanzania kilio hiki kielekezwe kwa wakubwa its shame upon them...

Hivi Mkuu unasema kweli?
Ukuta wa km 80?...Ni kweli wanahitaji kujilinda kwa namna hiyo?
Labda utuambie ni wa material gani kwanza kama si wa tofali!

Lakini kwa namna yoyote, hiyo tofauti ya kipato kati ya kaburu na wabongo inasikitisha!
Naamini kauli mbiu ya MayMosi kuwa Watanzania wanaonekana WATUMWA katika nchi yao wenyewe!

Du mkubwa nashukuru sana kwa habari hii, ngoja nisome tena ntarudi baadae

Hii ndo faida ya kusainia mikataba hotelini Ulaya. Wengi hawakuona madhara yake sasa ndo wanayaona. Jukumu la kujenga shule na zahanati si la makampuni binafsi bali ni la serikali. Na ni serikali hiyo hiyo inayopanga kima cha chini cha mishahara katika sekta mbalimbali. Hawa jamaa hawajaja Bongo kuuza sura, wamekuja kutengeneza faida, na wameshaona tz kuna cheap labour.

Ukuta huo unakadiriwa kugharimu kiasi cha USD 6,000,000.00. Ni bajeti ya wizara ngapi?

Chukua hatua.

Usitake nianze kulia na kuanza kufikiria kwenda kufa nao huko Magogoni ndiko wanakoaimaliza nchi yetu

usife ndg, hapa ni kupambana nao. Wazungu wanatuona mazoba kweli.

usije shangaa kusikia ukuta huu unajengwa na serikali yetu kama sehemu ya input cost ktk uchimbaji madini.Yaani kwa kodi yetu!.

Hivi tungechimba wenyewe na kuuza.Hakika leo tungekuwa mbali kimaendeleo.Gold ipo juu kwa sasa.

usife ndg, hapa ni kupambana nao. Wazungu wanatuona mazoba kweli.

Mkuu unakoseaa....!adui yetu sio mzungu...ni 'viongozi' wetu,watunga sera wetu,wawakilishi wetu bungeni na akina dr Kafumu,JAH HERO....Kuamua kupambana na hawa wazungu ni kupoteza target....Tuamke tujitie ujasiri tupambane na mfumo wetu unaolea na kulinda viongozi wabovu,wasio wazelendo na wasio na uchungu na nchi yetu....WAKATI NI HUU!

Magamba matatu, tafadhali usichanganye kuwa wa TZ wote ni wizi, unaposema "sababu ni kuwa kampuni inahisi wataz wanaiba mali zao" nadhani ungesema wanahisi "wezi" wanaiba mali zao. Na pia sizani kama kwa kuhisi tu wangefanya yote hayo, nna uhakika wameshaibiwa na ndio maana wanafanya hivyo, kujilinda wao nafsi zao na mali zao.

Nadhani wasingekuwa na matatizo ya kuibiwa na mengine ya kiusalama wasingeweka huo ukuta, sioni ubaya wa kujilinda na kujihami. Au ulitaka wawache wazi?

Tanzania nzima ukitembea majumba, maduka, viwanda, vina kila namna ya ulinzi kuzuwia wezi na ujambazi, kuanzia maukuta makubwa makubwa mpaka waya za umeme, walinzi na silaha za kila aina, mbwa, mageti ya chuma, madirisha ya nondo. Au huyaoni hayo? sasa cha ajabu nini ikiwa wanajenga ukuta wa kujilinda?

Kama wewe una kajumba kako ka 20 x 20 na hakana hata mali za million mbili ndani unajilinda kwa ukuta, geti la chuma, waya za umeme, mbwa wa polisi na mlinzi wa kimasai na wa Knight security. Sasa hao wenye vifaa vya mabilion na mali wanayochimba ya matrilion unashangaa nini wakijilinda?

Hivi tunajengewa ukuta kwenye nchi yetu wenyewe?kweli kama ni ujinga umezidi

Unaweza kufa kabla ya siku zako hazijafika ukiendelea kuijadili tz!
Ngoja mie niendelee kula bata huku ufukweni!!

Kama Rais mzima anaweza kuhongwa mavazi na mabwanyenye tunaowaita wawekezaji unategemea nini mkubwa!

Wewe nyumbani kwako hakuna ukuta? mbona Mwadui kuna ukuta hamjasema?

Nyumbani kwangu sijajengewa na wageni.inashangaza kuona wazungu wanajenga ukuta eti kuwazuia wenyeji wasichukue madini.Mwadui huwa nafurahi sana nikisikia WABESHI wameingia kuchukua mawe

Back
Top Bottom