Mimi nimekulia eneo ambapo buzwagi ipo nakumbuka kipindi tunasoma shule ya msingi tulikuwa tunapita buzwagi hapo na wanafunzi wenzangu tunakwenda kucheza mpira KIJIJI cha jirani cha Mwime ya ILINDI sasa njia hiyo imefungwa na ndipo ulipo mgodi ambao sisi kama wananchi hatuna faida nao hata kidogo tunaloa vumbi kila kukicha ni tabu tupu hapa Kahama dhahabu yetu imegeuka kuwa mauti yetu sasa magonjwa kama kansa yanatunyemelea tumekwisha masikini Tanzania uliyetukuka sasa unanyong'onyea.