Ukusanyaji wa taarifa za anuani za makazi na kutoza kodi ya viwanja na nyumba. Je, wananchi wameandaliwa?

Lanlady

JF-Expert Member
Feb 27, 2019
1,421
4,729
Kwakuwa suala la maendeleo halisubiri muda, na kiongozi wa taifa Rais Samia alisema wazi kwamba hatuwezi kwenda tofauti na dunia inavyotaka. Swali lililopo kwa sasa, kuhusiana na ugawaji na ukusanyaji wa taarifa za anuani za makazi kwa ajili ya sensa; ni je, wananchi wamepewa elimu ya kutosha?

Swali hili ni kutokana na tetesi au taarifa zisizo rasmi sana, kwamba lengo kuu wa ugawaji huu wa maeneo ni pamoja na kukusanya kodi ya viwanja au nyumba. Baadhi ya wananchi wanadai kuambiwa kulipia tsh 130,000/= ili kuweka alama za mpaka (bicon) kwa maeneo husika ndani ya siku 90.

Je, wananchi wameandaliwa kukabiliana na hali hii? Au ndio kama ilivyokuwa kwa tozo za miamala, kwamba atakayeona hawezi aamie nchi jirani?
 
Hiyo 130,00 ilikua ndio malipo kabla ya vita ya Urusi na Ukraine, I'm sure saizi itakua imepanda kidogo hadi walau 210,000
teh...Mama anaupiga mwingi zaidi...😂
 
Back
Top Bottom