Ukusanyaji michango ya harusi sasa hivi mbinde balaa,hapatoshi

Ni bora hizo kamati za harusi wangekuwa wanakaa kupanga bajeti ya kuwasaidia watoto yatima, aidha kuwakusanya watoto wa mitaani kwa kuwaweka sehemu moja na kuwachangia hizo pesa kwani kuna wengine ndoto zao zinakufa kulibgana na kikosa watu wa kuwasaidia hivyo in bora hivyo vikao vya harusi vingekiwa vinakaa kujadili mambo ya msingi kama hayo na sio kufanya harusi za mamiliono kwa kiwaumiza watu na michango isiyo na tija

Sent using Jamii Forums mobile app
Good idea kabisa.
 
Mi nilishaacha kuchangia harusi siku nyingi tu.
Jambo hilo sio lahisi sana kama unavyoliona.
Kuna watu ukiacha kuwachangia kwao unageuka kuwa adui.
Wanachojua ni kuwa lazima uwe na hela ya kuwachangia harusi zao.
Hawaelewi utetezi wowote, wao undugu au urafiki ni kupitia kuchangiana. Usipowachangia, undugu hufa na urafiki ndio umeisha.
Wengi inawalazimu kukopa pesa mahali ili wachangie harusi kwaajiri ya kulinda undugu au urafiki usije ukaingia dosari.
Lengo linakuwa ni kulinda mahusiano ya kijamii nasio kutoa mchango kwa nia ya kufanikisha sherehe za harusi.

Ndivyo hali ilivyo
 
Wakati kiwango cha michango ya harusi inayochangwa na marafiki kikiporomoka kwa kasi nchini, washereheshaji (Ma-MC) wameanza kutumia mashine za kielektroniki za EFD ili kutoa stakabadhi.


Baadhi ya washereheshaji (ma-MC), wameenda mbali na kuwataka wenye kumbi zinazotumika kwa sherehe hizo kutowaruhusu washereheshaji ambao hawatawaonyesha kuwa wanatumia EFD.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa ile ari ya uchangiaji harusi iliyokuwapo miaka ya nyuma imeporomoka kwa kasi kubwa sasa.


Kulingana na uchunguzi huo, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, harusi za kifahari zilizokuwa zikifungwa ni nyingi kulinganisha na miaka miwili iliyopita kutokana na ugumu wa maisha.
Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, bajeti ya chini ya harusi au kumuaga bibi harusi (send off), ilikuwa kati ya Sh5 milioni na Sh7 milioni wakati kiwango cha juu kilikuwa zaidi ya Sh60 milioni.


Hata hivyo, sasa mambo yamekuwa tofauti kwani bajeti za harusi zinazopangwa na wanakamati zinakusanya kati ya asilimia 50 na 75 tena ni kwa wale wenye ndugu wenye uwezo.
Ugumu kukusanya michango
Uchunguzi huo umebaini kati ya kazi ngumu kwa sasa ni ukusanyaji wa ahadi za michango ya harusi, send off au kitchen party kutokana na kile kinachoelezwa kuwa watu ni wagumu kutimiza ahadi zao.


Chanzo kimoja kimedai kuwa kila mtu analia mambo yamebadilika na kwamba unapoonekana unafuatilia sana michango wapo watu ambao hufikia hatua ya kuzuia mawasiliano ya simu.
“Huu usawa wa sasa si kabisa. Kila mtu analia hana hela sasa hizo za kuchangia harusi anazitoa wapi? Ukiona mtu anakuchangia harusi zama hizi mshike sana huyo,” alidokeza mshereheshaji mmoja.


Mkazi wa Pumuwani mjini Moshi, Ewald John alisema anazo kadi tatu za harusi za marafiki wa karibu, lakini ameshindwa kuwachangia kwa sababu hali ya kifedha imekuwa ngumu. “Mimi nina kadi tatu, lakini mbili zimeshapita. Sio kwamba nilikuwa sijui lakini kiukweli sina pesa nafanyaje? Nafikiri Watanzania sasa tubadili aina ya maisha, hii michango haitawezekana,” alisema.


Mshereheshaji mashuhuri nchini, Sijabu Kiata alisema kiujumla hali ya maisha imebadilika na hata harusi zinazofanyika sasa si za gharama kubwa kulinganisha na miaka mitano au 10 iliyopita.
“Watu hawana pesa wala hilo sio suala la kuuliza. Kuna harusi unaenda unakuta inapita round (mzunguko) moja tu ya vinywaji kabla ya chakula na nyingine wakati wa chakula, basi,” alisema.


Wakili wa kujitegemea wa jijini Arusha ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema kama michango ya harusi ingekuwa ya lazima, basi ingebidi watumike madalali kuikusanya.
“Katika kazi mojawapo ngumu kwa sasa ni kukusanya michango ya harusi. Unaweza hata mkapishana kauli na mtu unayeheshimiana naye pale anapokwambia hali ni ngumu. Hali imebadilika,” alisema na kuongeza:


“Huko tunapoelekea itabidi mtu anayetaka kuoa ajiandae mwenyewe na marafiki zake wa karibu, tena unaalika watu wasiozidi 20 mkitoka kanisani mnaenda hotelini mnakula mnarudi nyumbani”.
Mkurugenzi wa Mfinanga Block Supply ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, Hussein Mfinanga alisema kutokana na mabadiliko ya maisha hivi sasa anafikiria kusitisha uchangiaji wa harusi.


“Huko nyuma mtu anakupa kadi na anakwambia kama humchangii kuanzia Sh100,000 basi usimchangie. Sasa hivi peleka kadi na masharti hayo uone kama utachangiwa,” alisema.
Mfinanga alisema siku za nyuma kuna harusi ilikuwa mtu akichanga Sh20,000 anapewa kadi ya mtu mmoja (single) na wale wanaochangia zaidi ya Sh50,000 ndio wanapewa kadi ya watu wawili, akisema hilo litafutika.


Ma-MC, TRA nao watoa neno:

Baadhi ya washereheshaji waliozungumza na Mwananchi jana walipongeza hatua ya Serikali kuwataka waanze kutumia mashine za EFD, lakini wakataka kuwapo mfumo wa kuwabana ma-MC wote.
Kiata alisema japokuwa ni mpango wa Serikali wa kuwataka washereheshaji wote kulipa kodi na kutumia mashine za EFD, utekelezaji wake ni wa kusuasua.
“Mimi nina mashine ya EFD tangu mwaka jana lakini wengi hawana na hii maana yake hawalipi kodi. Hii si sahihi. Ni lazima TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) ije na mfumo unaoeleweka,”alisema.


“Maisha yamebadilika hakuna pesa kabisa unaweza kukaa mwezi mmoja hujapata kazi na bahati mbaya hii kazi imeingiliwa, watu wanashusha bei hawana EFD mashine, ni vurugu tu.”
“TRA waziamuru hizi kumbi zinazotumika kwa hizi sherehe kuhakikisha kuwa kila MC anayeingia katika ukumbi aonyeshe risiti ya EFD aliyomkatia mwenye harusi. Lazima kuwe na usawa.”


Mshereheshaji mwingine, Ntoly Mayombola alisema hakuna MC anayepinga kutumia mashine hizo, lakini tatizo ni ughali wake kulinganisha na vipato vya washereheshaji.
“Tatizo unainunuaje? Unalipwa Sh100,000 au 150,000 au 200,000 lakini tunaambiwa mashine ni zaidi ya Sh700,000. Bado huu mfumo Serikali inatakiwa itoe bure hizo mashine,” alisema Mayombola.
Msimamo wa TRA
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alipongeza hatua ya baadhi ya washereheshaji kuanza kutumia mashine hizo.


“Tunataka (washereheshaji) wote waingie kwenye kutoa risiti za EFD na mwaka jana tulikaa nao na wako willing (tayari) kutumia hizo mashine. Tunaendelea kuwahamasisha wafanye hivyo mapema,” Kayombo.
Kayombo alisema matumizi ya EFD yatawasaidia Ma-MC kupata kazi kwa vile wananchi hivi sasa wana mwamko wa kudai risiti za kielektroniki na kwamba, wasio nazo inawanyima kazi kubwa hasa za Serikali.
Haya mastarehe ya kipuuzi tulijitakia wenyewe, wala hayakuwa ya lazima.Mtu kuoa au kuolewa anahitaji mashahidi wawili,Shehe,Mchungaji au Registrar wa harusi Bomani.The rest ni sifa za kijinga.They were complexes which were unsustainable.
Halafu hawa ma-MC nao,dah,wengine hata wametajirika kwa ajili ya ujinga wetu.Kweli nimeamini wajinga ndio waliwao.
 
Funga harusi ya kawaida tu maisha yaendelee,kwani shida nini harusi ikiwa ya kawaida.Huu mtindo wa kuchangishana inabidi ufe.
 
Mi naona kuna tofauti kati ya harusi na sherehe. Harusi inaishia kanisani halafu haina bei kama ikiishia kanisani na sherehe inaishia ukumbini na siku zote sherehe ina gharama kuliko harusi , kaa ukijua hivo.
 
Kutokana na kuibua kwa wimbi la wajasiliamali wanaotumia harusi ,misiba na masherehe mbali mbali kujinufaisha.....nimekata shauri la kutochangia mchango wa sherehe aina yoyote.....

Msiba ni mpaka nimuone marehemu......

Kama ni mgonjwa ni mpaka nimuone mtu live yupo ICU.....
 
Ni harusi za wagalatia tu ndio huwa zina gharama kubwa, Mujahidina hawanaga hizo gharama kubwa. Tunakoelekea wote watafanana.

Hilo la mashine za EFD nadhani haliwezekani, Maana mapatano ya MC na wenye sherehe huwa ni ya kienyeji mno na hakuna bei rasmi ya hizo huduma. Na ukimbana MC alipe kodi atakwambia hajalipwa chochote na wenye sherehe, yeye alikuwa anajitolea tu, maana sherehe ilikuwa ni ya rafiki yake.
 
Mkuu acknowledge source basi ya habari hii.. Inaonekana ni maneno yako.
 
Jambo hilo sio lahisi sana kama unavyoliona.
Kuna watu ukiacha kuwachangia kwao unageuka kuwa adui.
Wanachojua ni kuwa lazima uwe na hela ya kuwachangia harusi zao.
Hawaelewi utetezi wowote, wao undugu au urafiki ni kupitia kuchangiana. Usipowachangia, undugu hufa na urafiki ndio umeisha.
Wengi inawalazimu kukopa pesa mahali ili wachangie harusi kwaajiri ya kulinda undugu au urafiki usije ukaingia dosari.
Lengo linakuwa ni kulinda mahusiano ya kijamii nasio kutoa mchango kwa nia ya kufanikisha sherehe za harusi.

Ndivyo hali ilivyo
Unachosema ni kweli kabisa. Kuna watu hawaongei na mimi kisa sikuwachangia. Mimi nikishasema sina ni sina siwezi kwenda kukopa hela nije nimpe mtu ya mchango wa harusi huo utakuwa upumbavu. Kama undugu/urafiki unapimwa kwa michango ya harusi basi huo utakuwa sio urafiki. Sijui ni kwa nini hatukubaliani na hali tuliyonayo, sijui ni kwa nini mtu asifanye sherehe kulingana na uwezo wake, hali yenyewe ngumu saizi.
 
Wanao oa au kuolewa wanatukasirikia siku hizi kama ikitokea haukushiriki kumchangia harusi yake.
 
Jambo hilo sio lahisi sana kama unavyoliona.
Kuna watu ukiacha kuwachangia kwao unageuka kuwa adui.
Wanachojua ni kuwa lazima uwe na hela ya kuwachangia harusi zao.
Hawaelewi utetezi wowote, wao undugu au urafiki ni kupitia kuchangiana. Usipowachangia, undugu hufa na urafiki ndio umeisha.
Wengi inawalazimu kukopa pesa mahali ili wachangie harusi kwaajiri ya kulinda undugu au urafiki usije ukaingia dosari.
Lengo linakuwa ni kulinda mahusiano ya kijamii nasio kutoa mchango kwa nia ya kufanikisha sherehe za harusi.

Ndivyo hali ilivyo
Na usipotoa mchango unatengwa na wewe siku likikufika watu wanakusa moja kwa moja nadhani lengo hasa licha ya sherehe nikukutanisha watu pamoja
 
Back
Top Bottom