Ukusanyaji kodi, matumizi uongozi wa sasa na tunakoelekea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukusanyaji kodi, matumizi uongozi wa sasa na tunakoelekea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Profesa, Dec 17, 2011.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Hakuna Serikali inayoweza kuendelea bila kukusanya Kodi. Hata Mafanikio tunayoyazungumzia ya Mzee Ben, ni ukusanyaji na usimamizi mzuri wa Kodi. Kipindi hicho tulishaanza kuzoea utamaduni mzuri wa kulipa kodi, na kupima makusanyo na kushuhudia uwazi wa mipango ya matumizi ya kodi. Nakumbuka kila robo ya mwaka kulikuwa na taarifa mbalimbali za serikali na halmashauri za mapato na matumizi (Kwa bahati mbaya si wengi waliokuwa wanaelewa kilichoandikwa, ingawa kilikuwa kizuri na cha wazi, ila cha kitaalamu mno kwa mtu wa kawaida kuelewa). Tulishuhudia halmashauri zikishindana kukusanya kodi na kupanga na kusimamia matumizi mazuri na hata baadhi yao kupewa tuzo. Tulishuhudia hotuba za v/kiongozi wetu kila mwezi au mara kwa mara wakitukumbusha na kutupa hata mwelekeo wa makusanyo, mafanikio na malengo yanayokusudiwa. Tulishuhudia v/kiongozi wetu akinena kwa jeuri kabisa... 'tutajenga miundo mbinu yetu kwa fedha zetu wenyewe' na kweli tunaona majengo, barabara, vifaa n.k. vipya na vyenye ubora vilivyoibuka kwa kasi sana ndani ya mfumo wa serikali (achilia mbali na michango ya wafadhili ambayo inasemekana ni imani yao ilipoongezeka wakahamishia misaada serikalini). Tulishuhudia wafanyakazi wakitoka sekta binafsi na kuhamia seta ya uma. na tena na tena na tena....

  Nimeyamiss haya nimeyamiiss wana JF. Sijui kama ni mimi au vipi lakini sioni serikali ikisimamia uchumi na hata kuhangaika kuifanya nchi yetu ijitegemee... bila aibu wanajivunia walivyo wataalamu wa kuomba misaada kama vile ni mambu-mbu-mbu wa Ukoloni mambo leo... Haya mambo ya sijui magari ya kifahari, posho sijui nini yasingekuwa hoja kwa serikali yenye uchumi imara na yenye kutoa huduma nzuri na za kutosha kwa wananchi wake bila ubaguzi wowote... na fursa sawa za kiuchumi dah... nimemizi miss sera hizi (ingawa nilisita kuziamini ila sasa nina nafasi ya kuzitafakari na kufananisha, labda mambo yangekuwa mazuri zaidi ningeeendelea kuponda sera zile)... ah!

  Yaani sina uhakika kama raia wa nchi hii aliyenacho na asiyenacho wanapata fursa sawa ya matibabu, Elimu, Chakula bora, ulinzi dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji n.k.
  Naililia nchi yangu napata shida sioni huko tunakoenda naona ukungu nisaidieni jamani....

  Tuwalaumu wanasiasa au wataalamu?
   
Loading...