Ukurasa wa sita wa I Can I Will I Must; Je, wajua mzimu wa Nyerere na ujamaa ulimwandama Mengi!

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,368
Natamani niwe naweka kafungu hako kanako zungumzia vichwa vyangu vya habar ila nashindwa kwa sababu siwezi chora kupitia simu please kama kuna mjuzi anaisaidie.

Mzee Mengi anaelezea jinsi mzimu wa ujamaa wa Nyerere ulivyoendelea kumwandama mpaka kupelekea Mwalimu Nyerere kuntaja kwenye vikao vya CCM ambapo alibakia kuwa na nguvu baada ya kupoteza nguvu ya kuwa Rais kwa kustaafu.

Mzee Mengi anasema Nyerere alihofu sana mtu mmoja kuwa tajiri kati ya watu wote kuwa ni hatari kwa Taifa.

Zaidi Mwalimu Nyerere alionesha uwoga sana kwa Mengi kwa kuona kama anaweza kuwa tajiri na nguvu kisiasa kuliko Rais wa nchi.
 
...iliyopelekea mawaziri awamu zote wamuogope Mzee Mengi na Wengine kushauri afilisiwe...LM
 
Hivi hicho kitabu kinaitwa I Can, I Must, I Will au I Can I Will I Must? Maana naona kila mmoja anapachika maneno apendapo huku alama za comma zikisahaulika.
 
...iliyopelekea mawaziri awamu zote wamuogope Mzee Mengi na Wengine kushauri afilisiwe...LM
Wanasiasa wa Tanzania wako radhi mwenzao mweusi afilisiwe lakini mhindi au mzungu awe tajiri kuliko wote.
 
Back
Top Bottom