Ukumbi wa SMS

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,845
Kingunge kucharukia wapinzani kwa kutaja watuhumiwa wa ufisadi

Wasemavyo Wasomaji
Tanzania Daima

Gazeti hili sasa linachapisha maoni yenu yanayotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS), kujadili mjadala utakaokuwa unaanzishwa na gazeti hili.

Kwa mfano, mjadala wa sasa unasema: “Kingunge yuko sahihi kucharukia hoja za wapinzani juu ya watuhumiwa wa `kutafuna’ uchumi wa nchi?”

Kwako babu Kingunge, pole sana kwa propaganda za miaka mingi iliyopita, kwani unataka kuturudisha wapi tena wajukuu zako? Labda pengine kwa sababu inadaiwa hauna dini, ndiyo maana unataka kudiriki kutupumbaza juu ya madai ya ufisadi yanayowakabili wakubwa wenzio. Kwa ushauri, babu umezeeka, Watanzania wa leo wana uelewa wa mambo, hivyo acha kusaka shuka, kwani kumeshapambazuka. Kinachoonekana sasa ni kujiaibisha na pia kukiaibisha chama chako – Dk. Emma, safarini Moshi (0752 887 474)

Si ajabu nchi yetu ikawa ya kwanza kwa kupata misaada mingi kutoka mataifa mbalimbali, lakini fedha nyingi zinaliwa na mafisadi wa nchi hii. Ukweli ukidhihiri, uongo hujitenga. Kulikuwa na tatizo gani kuunda kamati ya kuchunguza ubadhirifu kama si kufichiana maovu na kulindana? Iweje leo maprofesa na madaktari waliobobea wakimbilie kwenye siasa badala ya kujikita katika taaluma walizozisotea? Kwa wapinzani wako sahihi kufichua ufisadi. – (0784 688 333)

Mzee Kingunge anapaswa ajue kuwa Watanzania wanaishi maisha magumu kutokana na mfumko wa bei kunakosababishwa na mikataba mibovu inayosainiwa na viongozi na pia kukithiri kwa ufisadi ndani ya serikali ya CCM. Mzee Kingunge akae pembeni awaache vijana wajenge taifa - Najangule, SR, Nachingwea (0755 554 010)

Kingunge jamani anazeeka vibaya, CCM someni nyakati sasa Watanzania wa leo sio wa mwaka 1974, Kikwete miaka miwili umeshindwa kumshauri, amechemsha. Hasira zetu mtaziona mwaka 2010 – Rojamo, Dar (0734 003 512)

Kwa staili hii, mzee Kingunge ni kikwazo cha Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya. Kutumiwa kwake kama mshauriwa kiongozi mkubwa wa nchi ni kama kosa kubwa, kwani anaonekana hana jipya. – Mwango, S.M, Newala (0773 104 830)

Mzee Kingunge hajui kwamba maji ya sasa ni marefu? Ya moto tena yanachemka? Waambiane kwamba, kila atakayeingia ataungua – (0755 351 485)

Hivi mzee Kingunge, ni uwaziri ndio unaokufanya usione rushwa na kelele hizi za ufisadi? Tafadhali wahurumie wajukuu zako kwa sababu enzi zako zinaelekea ukingoni – Swaleh Nau, Babati (0786 474 267)

Kingunde ndio wale wale, anawatetea wenzake ili serikali isionekane ya ajabu. Watu tumechoka, tulimchagua Kikwete kwa moyo wote ili alete mabadiliko, lakini wapi. Kingunge kwao Kilwa kumemshinda, lakini katika masuala ya nchi hataki ufisadi uzungumzwe, ajabu! – (0755 573 372)

Kingunge amelewa madaraka, pia inaelekea ameishiwa sera kutokana na utu uzima. Mtu akitajwa mwizi hatumtetei, tunachunguza madai kwanza. Heri tuhuma za vigogo zichunguzwe hadi ukweli upatikane. Sera za kulindana zimepitwa na wakati. – Bigirwa Mkama wa Ibwera, Bukoba (0713 337 871)

Propaganda chakavu za Kingunge haziwezi kufunika sh trilioni 1.3 zetu zinazodaiwa kutafunwa na mafisadi. Kingunge hawakilishi masilahi ya jimbo lolote ndani ya nchi hii zaidi ya wale waliompa heshima na madaraka asiyoyamudu – (0787 228 666)

Kingune na Warioba wanashangaza kwa kutetea ufisadi. Kama suala ni kuchafuana, mbona katika suala la Balozi Salim kwa kuitwa muuaji na hata kuhojiwa uraia wake wao walikaa kimya? Lakini leo hii wanaonekana kutetea taifa katika suala la ufisadi, wanaonekana wachochezi! Hakika mnamaliza vibaya. Kaeni kimya turudishe nchi kwa wana wa nchi. Hamuwezi kuzuia nguvu ya umma – Sallu Chamungwana (0755 538 720)

Katika hili, Kingunge amekurupuka mithili ya mtu anayetoka usingizini. Ang’atuke asiendelee kujiaibisha, asubiri 2010 aone faida ya kutetea ufisadi. – Jovin J. Mushi, Dar (0713 726 348)

Wamemwaga petroli kwenye moshi unaofuka. Ukweli utasimama hadi haki ipatikane. Huu ni moto usiozimika sasa, Ukweli ni kitu ambacho hakipingwi na wala hakitokomezwi kwa lolote. Nawaasa mashujaa watu wasiogope mkwara wa kupelekwa mahakamani – Chacha wa Sinza (0752 258 873)

Wapinzani wanasema ukweli wa mambo, Kingunge anatetea asichokijua, lakini wenye macho tunajua cha kufanya – Lenana Paresoi (0787 105 558)

Nasema babu Kingunge hayupo sahihi, anajaribu kuwatia wananchi mchanga wa macho wasione uovu unaofanywa na viongozi. Pia simlaumu kwa kuwa uwezo wake kuchanganua mambo unaelekea umefika ukingoni –Enock Amos (0717 790 552)

Kingunge hayupo sahihi na haitatokea kwamba Watanzania tutamwelewa kwani suala linalozungumziwa ni la uhujumu wa uchumi, hufanyika kwa usiri mkubwa hivyo tunamwomba aache propaganda za kisiasa, asimamie masilahi ya nchi kwani bado tunamheshimu – Mkilya Moses (0784 685 370)

Kwa mtazamo wangu, Kingunge ameupotosha umma, pengine ni kwa sababu ya kulewa madaraka na kung’ang’ania serikali. Apumzike – Edwin Tillya, Babati, Manyara (0717 766 608)

Kama hoja ya Slaa si ya ukweli, kwanini wasiende mahakamani? Kingunge na Mkono hawana hoja, heri wangekaa kimya. Wakati wa mabadiliko ni sasa, siyo kesho – Bwigane (0713 285 774)

Kama mwili unazeeka, naamini hata akili nayo huchoka. Kimsingi, mzee Kingunge anastahili kupumzika, kwani busara ya uongozi inaelekea bado ana ile ile ya enzi zake. Ni heri atulie nyumbani, kwani hatupendi ukasuku, asipoangalia atapuuzwa yeye kwanza kabla ya upinzani – Tumbo, Dar (0712 176 060)

Kingunge asilazimishe tui la nazi nilione ni maziwa, kwani hajajibu tuhuma. Kingunge, wakati wa kusemea watu umepitwa na wakati – 0784 691 417)

Mzimu wa Mwembe Yanga umeanza kumtafuna Kingunge. Bila shaka anazima moto, kwa kuhisi huenda naye yumo katika orodha ya kikosi cha akiba. Mzee Kingunge, mvi si kigezo cha busara, lakini asome alama za nyakati - J.D Kagame, Dar (0732 135 063)

Watafuna nchi tumewaona, kama wapinzani ni waongo wapelekeni mahakamani tujue mbivu na mbichi, msijidanganye kwa ziara zenu za kinafiki, zinazolenga kuficha maovu. Mzee Kingunge aache kuwasemea – (0714 515 747)

Mzee Kingunge ana haki ya kutetea ufisadi, pengine naye ni sehemu yao, si unajua usemi wa ‘mwenzio akinyolewa?’ Anadhani naye hatasalimika. Na kweli, ajiandae, kabrasha lake liko tayari. Itakuwa aibu kuharibikiwa ukubwani – Douglas Sallu (0755 538 720)

Kingunge kuna anachokificha, ndiyo maana unajaribu kuwatisha wapinzani, lakini tunasema, huwezi – Hassan Ally, Wete, Pemba (0757 586 658)

Kingunge ana kila sababu ya kutamba. Kwa ufupi, mazingira dhaifu ya sheria mama ndiyo sababu kubwa ya mzaha usiosemeka unaofanywa na CCM na serikali yake, sheria mama lazima itungwe upya – Joffrey Mwamuntu (0787 331 611)

Mzee Kingunge hakuwa sahihi hata kidogo. Kwa asilimia 100, wapinzani wanasema ukweli. Watuhumiwa tunawasubiri mahakamani, naamini hawatatoka salama – A. Mafie, Moshi (0752 403 402)

Namshauri mzee Kingunge asikilize mkanda wa tukio, ili ajitoe huko, kwa sisi tuliofika pale tuhuma zile hazifutiki kwa propaganda, bali kwa hoja. Viva upinzani, ikomboeni nchi hii – Pplema (0754 805 254)

MJADALA MPYA:

Ni sahihi kwa mawaziri kuzunguka mikoani kuchanganua kwa wananchi bajeti ya mwaka wa fedha wa 2007/8?
 
Kingunge kama huamini basi muulize Mungai na laiti wewe ungekuwa katika harakati fulani ungezomewa vibaya sana maana wewe ndiyo mpika majungu mkuu wa ccm ungezomewa hadi ungesahau meno yako bandia mezani. Wajukuu zako wamezaliwa wewe na ccm wamefariki kwa dhiki na umaskini kwa ajili ya njaa na dhiki wewe bado na ccm waachie vijana.
 
naona walotuma sms wote wapo bongo. hivi waliopo nje watume sms kwa simu namba gani?
 
naona walotuma sms wote wapo bongo. hivi waliopo nje watume sms kwa simu namba gani?

Jaribu kuwapigia simu katika namba zilizoorodheshwa hapo chini.

Mtaa wa Mkwepu na Makunganya
Jengo la Bilicanas, Gorofa ya kwanza
S.L.P. 15261, Dar es Salaam
Au piga simu -

+255-22-2126233
+255 713 296 570
+255 732 296 507
+255 754 670 184
+255 773 364 078

Au tuma faksi -

+255-22-2126234
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom