Ukumbi wa Papa: Ndiyo Utambulisho wa yule Nyoka wa Eden?

Nimekuelewa mkuu tatizo sisi binadamu wengi wao hatupendi kusoma kuchambua kwa nini hiki kiko hivi, kwa nini dunia moja na Mungu mmoja na dini zipo zaidi ya 10,000/= duniani kote, tunapenda kushikilia kile tukiaminicho na sio kutafuta tafuta na kujifunza kwa nini hii hiko hivi, hii ndiyo maana tunapenda kutafuniwa na sisi kazi yetu ni kumeza tu, ujiulizi ni nini hiki ninachomeza, Asante mkuu nilikuwa sijui na sasa nimejua nimegain kitu kutoka kwenye mada hii, mimi huwa ninapenda kufanya upembenuvi au kutafiti na kuelewa jambo siyo mtu wa kutafutiwa tu na kupewa halafu wewe unaitikia ndiyo mzee!!
Nasema tena asante mkuu mimi nimezaliwa katoliki na kukulia huko lakini leo nimejifunza kitu kutoka kwenye hekalu hili la Papa. Nasema asante sana na Mungu awe pamoja nawe ni raha sana jamiiforum!!
Pamoja sana mkuu🤝🤝
 
Wasalaam wakuu

Pope Audiance Hall

Paolo VI pia inajulikana kama Jumba la mkutano la Kipapa ni jengo moja kubwa huko Rome kwa Papa, lenye uwezo wa kuchukua watu 6,300, lilitengenezwa kwa saruji iliyoimarishwa vyema na mbunifu wa Italia Pier Luigi Nervi na kukamilika mnamo 1971

Lakini katika Jumba hilo, sanamu na muundo wa jengo hilo ni za kushangaza na watu wakaanza kutilia shaka

View attachment 1717036

Jumba la Wasikilizaji la Papa lilivyoundwa na kufanana kwake na maumbile ya nyoka. muundo huu wa kipekee unaonekana sehemu ya juu tu ndani na nje.

Jumba hili la Wasikilizaji la Paul VI, Lilianza wakati waa Papa Paul wa Sita, ambaye alikuwa kutoka 1963 hadi 1978. Inavyoonekana alikuwa Papa mwenye heshima, ingawa amehusishwa kuficha au kupuuza unyanyasaji wa kijinsia wa wavulana na washirika wa Katoliki kutoka kwa makasisi.
Aliarifiwa kuhusu kashfa hizi katika barua ya Mchungaji Gerald M.C. Fitzgerald mnamo Agosti 1963, na alishauriwa kuchukua hatua kali dhidi ya washenzi hao
Lakini hakuwahi kufanya chochote.

View attachment 1717025

Katika eneo la juu la jengo hilo linasimama kwa sura yake isiyo ya kawaida, ambayo ikachorwa kwa mfanano wa kichwa cha nyoka.

View attachment 1717032

Angalia kufanana kwa sura, paa la kuezekea na ngozi, na macho.

View attachment 1717042

jengo hili Liliundwa na mbunifu wa Kiitaliano aliyeshinda tuzo
bwana Pier Luigi Nervi, jengo hilo limebuniwa na huchukua watu 6300 kwa mkutano na Papa mwenyewe, ambaye huwa anawasilisha tarifa kutoka jukwaani

SANAMU YA YESU YENYE MFANO WA NYOKA

View attachment 1717034

La Resurrezione, sanamu hiyo iliundwa na Pericle Fazzini. na huku wakiweka wazo la Kristo akiinuka kutoka kwenye mlipuko ,mlipuko wa nyuklia. Ndivyo sanamu hiyo ilivyotengenezwa

Cha kushangaza, kutoka kwa pembeni, kwenye kichwa cha Kristo kinaonekana kama kichwa cha nyoka aliye na meno aliyefunua mdomo wake kwa ajili ya kung'ata

Mambo ya ndani ya Ukumbi huu hufanana sana na nyoka, cha kushangaza na meno mawili yaliyowekwa juu ya jukwaa. Wote kutoka kwa jukwaa, na kwa njia ya kuingia ya watazamaji, chumba bila shaka kinafanana na nyoka,

View attachment 1717035

Wengine wamedai watu huandika hii kama mawazo ya udanganyifu, wakionya watu mbali na kuzingatia kwa kina.

Huku wengine wakipinga zaidi kwakuwa ni swala linalogusa Imani Zao

Huku wengi wakihususha Mfumo huo kama heshima na Utambulisho kwa Nyoka alieasisi dhambi kuingia Duniani pale Eden
hii yote ni kutokana na Lawama wanazotupiwa Mapapa na Vatcan juu ya kuwa Controlled chini ya shetani
Huku wakiwa na Vikundi vya Siri siri vilivyo Chini ya Shetani kama Priory of Sion na vinginevyo.

DA'VINCI XV
Nimeisoma vizuri lakini hapo mwenye kosa ni papa, mwenye kosa ni Roman Catholic, au mwenye kosa ni Mbunifu wa jengo?

hii naifananisha na makampuni yanayo deal na utengenezaji wa ramani za nyumba, unaenda kununua ramani ambayo tayari ilisha chorwa japo wanakuelezea lakini huwa hauwezi kuitafakari kwa kina baadhi ya maeneo hata kama kuna vitu wameviweka kwa siri.

hivyo kwangu Mimi naweza kusema, hiyo picha yenye muonekano wa nyoka wao hawakuiweka wala kuichukulia kama taswira ya nyoka ila kwasasa kila mtu akiiona kwakuwa ishakamilika atakuja na majibu yake kama hivo ulivyo elezea.

Leo jaribu ukaichunguze hata nyumba yako na wewe au nyumba ya nyumbani hasa zile nyumba kubwa achana na nyumba mstatili au mraba kisha piga picha mbele na juu then kaa sehem anza kuichunguza utapata taswila ya vitu vingi ambavyo mmiliki wa nyumba hakuvilenga vyenyewe.
 
Always mtu anaona anachotaka kuona, kama ubongo wako umejipanga kuafananisha na nyoka lazima itafanana, akija mwingine akifananisha na kitu kingine itafanana pia. Kuna mada humu inasema kwenye mwezi kuna picha ya mwanamke kabeba mtoto; hicho ndicho kitu ubongo wake umeamua kuona na atakiona kweli. Kuna ile picha ya monalisa iliyochorwa na Davinch, wanasema ni picha ambayo ina all expressions of human feelings; yani ukiitazama kuona kama anafuaha utaiona, ukitaka kuona huzuni utaiona n.k, n.k. Mimi nilikua naiona siku zote but sikuwahi kuona ivo vitu but the day nilivyoambiwa hivyo nikaenda google kuicheki nikiwa na hiyo mentality na kweli niliziona expressions zote, coz ndicho ubongo wangu ulitaka kuona na kuprove.

Mtahangaika sana kuhusu Pope but this will never change a thing; yani hizi stori mnazotoa zote ni marudio hakuna mpya na hiaitatokea; coz Kanisa ni Moja, Takatifu, Katoliki la Mitume. Mungu kaliinua na hakuna wa kulishusha, Period.
Umeongea point nzuri sana mkuu ila ukaharibu kumalizia, umesema kanisa ni moja tu, Takatifu, katoliki la Mitume. Kwa ushahidi upi ndugu yetu toka kwenye vitabu vya mungu au kokote ? Can you tell us please 🙏🏾
 
Tukisema hapa kuna watu watadai tunakashfu imani ya watu ila kanisa katoliki siyo dhehebu sahihi kimaandiko hata huyo nyoka anasadifu ni nani kiongozi wake rejea ktk biblia yule anayetajwa kama nyoka ni nani ukimfahamu basi huyo ndiye
Sawa sio dhehebu sahihi, lipi ni dhehebu sahihi?
 
Pole sana una safari ndefu ya kujifunza ila hujaamua tu. Achana na mambo ya kufikirika, jifunze biblia mbona iko wazi kabisa
Chief's..! Hata katika dini zote tumeambiwa tutafute hata katika biblia unayosoma wameandika kabisa watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa mfano huwezi kujua dini Fulani ina Mila na desturi potofu mpaka uisome ile dini ndio uweze kujua mahali ambapo hakuko sawa..! Naamini katika mungu na dini yoyote najifunza iwe biblia nasoma Qur'an nasoma tamaduni za mabudha najifunza pia.

ama kwa hakika imeandikwa nenda mashariki na magharibi katafute elimu..!
 
Academically
Architect huwa wana kitu kinaitwa concept, si ajabu huyo mbunifu alimtumia nyoka kama concept tu na s swala lingine. Kama n hivyo basi n lazima jengo liwe la mtindo huo ili liendane sawa na hio concept.

Spiritually
Inawezekana kuna kitu kimefichwa nyuma ya huo muundo wa jengo

You see the world the way you are.
The greatest enemy of education is an illusion of knowledge.
 
🤝🤝🤝
 
Yawezekana pia,
 
Yaani mimi Roman Catholic nipo chalii mdogo niliwakataa maana wamechanganya Christianity and tradition rituals...

kwa sasa muwakilishi wetu duniani ni Yesu naye ndo sadaka yetu ya kuteketezwa ambayo Mungu anaipokea.Yote ya kale(tradition rituals) yalikwisha pale msalabani na sasa tunamuabudu Mungu huru maana hatuko watumwa tena chini ya binadamu yoyote(Papa)
 
Naona ukaiput in bracket
 
Always mtu anaona anachotaka kuona, kama ubongo wako umejipanga kuafananisha na nyoka lazima itafanana, akija mwingine akifananisha na kitu kingine itafanana pia. Kuna mada humu inasema kwenye mwezi kuna picha ya mwanamke kabeba mtoto; hicho ndicho kitu ubongo wake umeamua kuona na atakiona kweli. Kuna ile picha ya monalisa iliyochorwa na Davinch, wanasema ni picha ambayo ina all expressions of human feelings; yani ukiitazama kuona kama anafuaha utaiona, ukitaka kuona huzuni utaiona n.k, n.k. Mimi nilikua naiona siku zote but sikuwahi kuona ivo vitu but the day nilivyoambiwa hivyo nikaenda google kuicheki nikiwa na hiyo mentality na kweli niliziona expressions zote, coz ndicho ubongo wangu ulitaka kuona na kuprove.

Mtahangaika sana kuhusu Pope but this will never change a thing; yani hizi stori mnazotoa zote ni marudio hakuna mpya na hiaitatokea; coz Kanisa ni Moja, Takatifu, Katoliki la Mitume. Mungu kaliinua na hakuna wa kulishusha, Period.
Sawa mpinga kristo
 
Nimeisoma vizuri lakini hapo mwenye kosa ni papa, mwenye kosa ni Roman Catholic, au mwenye kosa ni Mbunifu wa jengo?

hii naifananisha na makampuni yanayo deal na utengenezaji wa ramani za nyumba, unaenda kununua ramani ambayo tayari ilisha chorwa japo wanakuelezea lakini huwa hauwezi kuitafakari kwa kina baadhi ya maeneo hata kama kuna vitu wameviweka kwa siri.

hivyo kwangu Mimi naweza kusema, hiyo picha yenye muonekano wa nyoka wao hawakuiweka wala kuichukulia kama taswira ya nyoka ila kwasasa kila mtu akiiona kwakuwa ishakamilika atakuja na majibu yake kama hivo ulivyo elezea.

Leo jaribu ukaichunguze hata nyumba yako na wewe au nyumba ya nyumbani hasa zile nyumba kubwa achana na nyumba mstatili au mraba kisha piga picha mbele na juu then kaa sehem anza kuichunguza utapata taswila ya vitu vingi ambavyo mmiliki wa nyumba hakuvilenga vyenyewe.
binafsi baado naamini ni mpango kabambe, Haiwezekani mpaka Idols za ndani ziwe na figure kama hiyo ya Reptilia

Na hizo si kazi ya muundaji wa jengo , zilikuja baada ya jengo
 
Back
Top Bottom