Ukubwa wa Serikali ni tatizo kubwa sana: Sio idadi ya mawaziri pekee! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukubwa wa Serikali ni tatizo kubwa sana: Sio idadi ya mawaziri pekee!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamundu, Jul 9, 2012.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kwa nchi masikini kama Tanzania ukubwa wa serikali ni tatizo kubwa sana kwa maendeleo. Kitu kimoja ambacho watu wengi hawaelewi ni kwamba tunaposema ukubwa wa serikali hatuna maana ya ukubwa wa baraza la mawaziri bali uwingi wa vitu ambavyo serikali ya Tanzania imejihusisha.

  Tuanza na Budget ya serikali je ni kiasi gani cha budget kinanda kwenye shughuli za maendeleo? ni kidogo sana hivyo tunaserekali ambayo kazi yake kubwa ni kujilipa mishahara.

  Serilkali inafanya mengi pamoja na yafuatayo

  1. Ina lipa jeshi lote la Polisi, Magereza, Ulinzi na kuwapa makazi wafanyakazi wote
  2. Madaktari karibu wote ni wa serikali kuanzia kuwasomesha kwa madeni ambayo hayalipwi mpaka kuwapa kazi.
  3. Walimu karibu wote wanalipwa na serikali kuanzia kuwasomesha kwa bure mpaka kuwalipa mpaka wastaafu
  4. Wafanyakazi wote wa miji diwani, wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa, mkurugenzi mkuu n.k
  5. Balozi zote dunia nzima
  6. Vyuo vikuu vyote, shule zote na hospitali zote za serikali
  7. Wabunge wote
  8. Nyumba na majengo yote ya serikali na ukarabati

  Sasa tumekuwa watu wa kulalamika tu lakini hatutafanikiwa kama serikali haitapungua. Je tufanyaje

  Serikali inatakiwa kuajiri kampuni ya kibinafsi ya kuongeza ufanisi wa serikali " Productivity" kama " Price Coopers Waterhouse" waangalie serikali yote na waje na jensi gani wanaweza kuongeza ufanisi kwa kuweka techonology kama za Computers na kuchanganya vitengo ambavyo vinafanya kazi moja. Hii itapunguza wafanyakazi wa serikali kwa kama 50%. Itatusaidia kupata pesa za kulipa vitu muhimu kaa Doctors na Walimu.
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Majuzi serikali ya marekani imetangaza kupunguza baadhi ya departments zao ili kusave hela za walipa kodi sisi hapa ndo kwanza tunaongeza mikoa na wakuu wa wilaya. Sisi nchi maskini gharama zote za uendeshaji wa serikali za nini? Inabidi wataalam kutoka nje waje watuonyeshe jinsi ya kubana matumizi ya pesa za walipa kodi. Kama marekani wanapunguza ukubwa wa serikali zao kwanini nchi maskini ka ya kwetu ndo kwanza tunaongeza? Au kwa sababu inabidi kulipana fidia na kuwapa vyeo maswahiba wanaotusaidia kwenye kampeni za uchaguzi?
   
 3. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Computers wanazo serikalini lakini hawajui kuzitumia kuongeza ufanisi.

  Kuna wale wazee wa miaka 47 wabishi sana hata kujifunza computer na hata wakijifunza wapo slow sana ni afadhali umpe kalamu na karatasi aandike barua kuliko matumizi ya e-mail na internet.

  Cha msingi ni kuwaondoa wazee wote kwakuwa tuna matatizo ya ajira kwa vijana tunatoa wazee 4 unaweka kijana mmoja atalipwa mshahara kama wa mtu mmoja mzee alioondoka na anapewa training ya kutosha unaweza kupunguza gharama kwa 30%. Hata jeshini na idara zingine lazima zijipange pia maana kwa 21st Century kuwa na wanajeshi wengi sio kushinda vita.
   
Loading...