Ukubwa wa msanii unapimwa kwa umaarufu wake na wingi wa viewers YouTube au kuna kigezo gani?

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
May 30, 2021
333
671
Wakuu habari za jioni, unaweza kunambia ukubwa wa msanii unapimwa kwa umaarufu wake na wingi wa viewers YouTube au kuna kigezo gani ambacho wewe unaweza kitumia ukasema huyu msanii ni mkubwa?

Je inawezekana msanii akawa maarufu na asiwe mkubwa au akawa Mkubwa na asiwe maarufu? Toa mfano.

Chanzo cha mada ni maluma ft rayvanny. Kuna watu wanabishana maluma sio msanii mkubwa katika uso wa dunia mwingine naye akajibu kua maluma ana viewers 1 billion unawezaje kusema sio Mkubwa?
 
Ndiyo! Msanii anaweza kuwa maarufu na asiweze kuwa mkubwa mfano; Baba Levo, Country Boy, Sholo Mwamba, Gigy Money and co. Ilhali ni nadra kuwa mkubwa pasi ya umaarufu.

Kuhusiana na Maluma ni moja ya msanii mkubwa tena mkubwa sana ulimwenguni, naweza kusema ni top 100 kwa kuzingatia yafuatayo;-

Idadi ya nyimbo na nyimbo zilizofanya vizuri, takwimu za nyimbo hizo katika streaming platforms, digital distributions na chati mbalimbali za muziki, matamasha, collabs na ukwasi alionao.

Lugha yaweza kuwa kikwazo na wafuasi wa muziki kutoka Africa na hasa Tanzania ndio wanaopata chanagamoto kutokana na kuamini katika UMAREKANI ("Lil Pimp, Lil Child, Lil Shit ametoa ngoma"), kutofuatilia muziki na kufuatilia wasanii.
 
Dah!! Mwamba umeua mpaka umeboa kinyama.
 
Msanii anaweza akawa mkubwa na maarufu sana katika nchi A,
ila katika nchi B akawa hafahamiki hata.
 
Ukubwa wa msanii kwa upande wangu ni vile anavyoweza kutumia fasihi kupitia muziki kufikisha ujumbe unaoweza kuishi vizazi mpaka vizazi..otherwise ni midundo tuuu
 
Wakuu habari za jioni, unaweza kunambia ukubwa wa msanii unapimwa kwa umaarufu wake na wingi wa viewers YouTube au kuna kigezo gani ambacho wewe unaweza kitumia ukasema huyu msanii ni mkubwa?

Je inawezekana msanii akawa maarufu na asiwe mkubwa au akawa Mkubwa na asiwe maarufu? Toa mfano.

Chanzo cha mada ni maluma ft rayvanny. Kuna watu wanabishana maluma sio msanii mkubwa katika uso wa dunia mwingine naye akajibu kua maluma ana viewers 1 billion unawezaje kusema sio Mkubwa?
Maluma ni msanii mkubwa sana kwa ukanda wao huo south america na baadhi ya mataifa yanayozungumza Portuguese na mafanikio ya kimziki anayo kiufupi maluma ni msanii mkubwa sana utakua mwendawazimu useme sio mkubwa labda kama umemjulia alivotoa nyimbo na rayvann
 
Back
Top Bottom