Ukubwa wa melikebu au mwendo wa bahari?

Quemu

JF-Expert Member
Jun 27, 2007
984
128
Hodi hodi wahenga, kijana wenu nna swali,
Kuna jambo lanichenga, akilini natafakari,
Jambo hili la chemba, wawili wanapo vinjari,
ukubwa wa melikebu au mwendo wa bahari?

saizi ya melikebu, wasafiri ushabikia
wengi usogea karibu, pale inapokaribia
wataka kuikarimu, kisha kuitumikia
saizi ya merikebu, au bahari ipigia?

wimbi lichocheapo, nahodha uongeza kwata
wasafiri ujongeapo, ufurahia hiyo chacha
sauti nderemo na vifijo, meno yao ukatakata
bahari yenye mapigo, au merikebu kubwata?

Melikebu ndefuyo, sehemu kubwa ubaki nje
Abiria upandayo, upiga mayowe chonde
melikebu ipepeavyo, nahodha upiga konde
melikebu kubwavyo, au bahari mwendowe?

Bahari mwendowe, ufanikisha safari tamu
Mwendo mdundowe, abiria ushika hatamu
Mapigo yapigawe, hakika hakuna haramu
Bahari mwendowe, au ukubwa merikebu?

Swali naomba jibiwa, ili nipate ujuzi
sana ughalifiwa, pia upata maudhi
naomba kujuwa, kipi nikifungue uzi
Merikebu kubwa, bahari kamakazi​
 
Japo kuwa i wazi ,Swali halijibiwi kwa swali
Ila swali huzaa swali ,kupata jibu isipo budi
Wahenga hawakusema kila mchomo una raha yake mwilini?
Je haikuongezewa Utamu wa pipi ni mate yako mlambaji?
Nini maanake ,ukubwa wa pua si wingi wa makamasi ?
Nani alesema Mkate wa boflo kiboko yake chai!?
Ikasemwa pia Mwanamume hasifiwi kula asilani!
Tamati nafikia ,jibu la swali hutegemea kaulizwa nani
Ukubwa wa tonge maamuzi ya mmezaji.
Kwa wangu uzoefu ,haya ni yangu maoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom