Ukubwa wa bunge la jamhuri ya muungano, na serikali ya mapinduzi ni maslahi ya nani?

M

Membensamba

Senior Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
157
Likes
0
Points
33
M

Membensamba

Senior Member
Joined Nov 4, 2010
157 0 33
Idadi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano, na ukubwa wa serikali binafsi unanipa shida kuoanisha faida yake kisiasa na gharama za kuviendesha hasa ninapofikiri umaskini mkubwa wa mwananchi wa kawaida. Sio tu kwamba tuna majimbo mengi mno ya uchaguzi, bali pia viti maalum vingi. Na kama hiyo haitoshi, kuna viti kumi zaidi vya mhe. raisi kujiwekea awapendao!

Huko Zanzibar nako kuna majimbo kila baada ya mtaa kama sio kata. Nchi ndogo, lakini makamu wawili wa raisi. Hebu wanaJF nipigieni hesabu hawa wote: Wabunge wa muungano na wa visiwani, na makamu wawili wa raisi wanagharimiwa sh ngapi kwa mwezi kama mishahara na marupurupu yao ya vikao?

Je gharama hii inalingana na umaskini wa nchi hii? Hivi nafasi yote hiyo (hatujataja ukubwa wa serikali ya muungano) kweli ni kwa maslahi ya taifa au ni njia ya kupeana kazi? Niambieni budget ya ku-run serikali ni sh ngapi kwa mwaka? Na inatoka ndani au ni msaada? Je gharama hiyo ikilinganishwa na budget ya elimu, afya, na kilimo tofauti ni justfiable kweli? Hebu wabunge zungumzeni maswala haya kama kweli mna maslahi ya taifa mioyoni mwenu tuwasikie.
 
M

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2010
Messages
2,511
Likes
13
Points
0
M

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2010
2,511 13 0
Kwanza Nikupongeze ndugu yangu MEMBEMSANGA...
Ni kweli kwamba Idadi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano, na ukubwa wa serikali unatisha.
Mathalani ukichukulia uchumi mdogo wa nchi yetu inatia shaka kama kweli viongozi wetu wanajua wanachokifanya.
Binafsi inanipa shida kuoanisha faida ya ukubwa huu kwa nchi kama yetu
Mfano Kule Zanzibar kuna Wabunge wanaongoza watu chini ya 7000 eti hilo jimbo nalo?????????
Gharama za kuendesha nchi ni kubwa kwa sababu ya ujinga wa serikali ya chama tawala.!!!
Huwa nafikiri kama kweli viongozi wetu wanajali umaskini mkubwa wa mwananchi wa kawaida.
Cha ajabu haikuishia hapo VITI MAALUMU navyo kama njugu??!!!.
Bado vikaongezwa tena viti kumi zaidi vya mkuu wa kaaya. Ili aweke washkaji kama wananchi hawakuwateua

>>>Je gharama hii inalingana na umaskini wa nchi hii?
>>> Je kwa staili hii Maisha bora kwa kila mtanzania yapo?????????
>>> Hivi kweli ni kwa maslahi ya taifa hapo au UFISADI????

Tuchangie wadau nchi ni yetu kodi zetu

>>> au Je wadau hamna uchungu nyie?
Niambieni Basi.
Mbaya zaidi pamoja na yote hayo muheshimiwa anaenda nje kifua mbele kuomba misaada kwa nchi yetu maskini TANZANIA????????????????tuwasikie.
 
M

mbombongafu

Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
61
Likes
0
Points
0
M

mbombongafu

Member
Joined Nov 1, 2010
61 0 0
Idadi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano, na ukubwa wa serikali binafsi unanipa shida kuoanisha faida yake kisiasa na gharama za kuviendesha hasa ninapofikiri umaskini mkubwa wa mwananchi wa kawaida. Sio tu kwamba tuna majimbo mengi mno ya uchaguzi, bali pia viti maalum vingi. Na kama hiyo haitoshi, kuna viti kumi zaidi vya mhe. raisi kujiwekea awapendao!

Huko Zanzibar nako kuna majimbo kila baada ya mtaa kama sio kata. Nchi ndogo, lakini makamu wawili wa raisi. Hebu wanaJF nipigieni hesabu hawa wote: Wabunge wa muungano na wa visiwani, na makamu wawili wa raisi wanagharimiwa sh ngapi kwa mwezi kama mishahara na marupurupu yao ya vikao?

Je gharama hii inalingana na umaskini wa nchi hii? Hivi nafasi yote hiyo (hatujataja ukubwa wa serikali ya muungano) kweli ni kwa maslahi ya taifa au ni njia ya kupeana kazi? Niambieni budget ya ku-run serikali ni sh ngapi kwa mwaka? Na inatoka ndani au ni msaada? Je gharama hiyo ikilinganishwa na budget ya elimu, afya, na kilimo tofauti ni justfiable kweli? Hebu wabunge zungumzeni maswala haya kama kweli mna maslahi ya taifa mioyoni mwenu tuwasikie.
Hii nchi ukianza kuifikiria sana unaweza kunywa sumu ufie mbali unachokiona wewe hata asiyesoma anajua kuwa gharama za uendesheji wa nchi hii ni kubwa si kawaida na hakuna sababu ya msingi ya kuwa kubwa hivyo kwa nini tuwe na wabunge wengi hivi na mawaziri wengi kama hivi na ukishazungumzia viongozi hao unazungumzia pia gharama za kuwatunza hao mishahara magari marupurupu yao na kadhalika.ahalafu tafakari hali ya umaskini uliopo sasa.
 
Forum statistics

Threads 1,235,534
Members 474,641
Posts 29,225,886